Je, mtu huyu nimfungulie kesi ya aina gani?

Pole sana.
Hana Haki wala Hakuna cha kubugi wala kuchelewa. Afterall baada ya msiba hukuwa sawa kwa kufiwa.
Tafuta mwanasheria. Mirathi ipi wanayotaka kuigawanya wakati mmewe upo.
Zile mali alizochuma dada yao peke yake hizo ndio wao wakae vikao vyao , wewe wape ushirikiano tu.
Ameqeka kufuri kwenye nyumba yako kavunje uendelee .
Mchukulie RB kwake akamatwe kwa kuingia na kupoteza vitu ndani y hiyo nyumba
 
Hapana mkuu
Unajua kwanini nimekwambia vile? Kwasabb huna akili kabsa jambo jepesi kama hili unashindwaje kuchukua hatua? Mali za mkeo ni zako na watoto wenu lkn wewe upo tu unatembea umebeba kichwa kama mzigo.

Kama watoto unaishi nao maana yake hata Kama ungekuwa huna ndoa na huyo marehefu bado Mali zingekuwa ni za watoto wa marehemu ambao ni wako pia.

Wewe ni mjinga , ndiyo narudia tena wewe ni mjinga huyo shemeji yako ameshakuona fala ndiyo maana ameamua kufanya atakavyo.

Kifupi mali zote za marehemu alizochuma kabla na baada ya ndoa mwenye haki nazo kwa 100% ni watoto wake.

Kama bado hujui cha kufanya hao wanao wamesha kosa wazazi wote wawili.
 
Una makosa mengi ulifanya mkuu

1. Kosa la kwanza
Kununua kiwanja Cha ukweni kwako

2. Kosa la pili,
Kujenga kwenye kiwanja Cha ukweni

3. Kosa la tatu,
Kumruhusu shemej yako kusimamia ujenzi

4. Kosa la nne,
Kumruhusu shemej yako kusimamia Kodi za wapangaji

5. Kosa la tano,
Kuruhusu shemej yako kua msimamizi wa mirathi

Nnachokiona hapa,
Hata kabla ya mkeo hajafariki,
Haukua na power yoyote ya kimaamuzi kwenye familia yako Kama baba wa familia

Kingine,
Hata baada ya mkeo kufariki,
Bado inaonyesha unakosa power ya kimaamuzi Kama baba wa familia yako.
 
Kwa picha la haraka haraka,
Mkeo alikukamata ukakamatika haswa haswa Kias Cha hao shemej na wake zako kukudharau kiasi Cha kuoana wewe na familia yenu nzima hamuwezi kusimamia wala kujisimamia kwny mirathi ya familia yako.

Huenda washaona hujiwezi kiuchumi Wala kifedha Kias Cha kusimamia Mali zile.
Na hili Probably linasababishwa una uchumi mdg kuliko wake zako au ushalishwa limbwata. Wanakumudu.

Bila kukaza na kuonyesha makucha halisi ya kiume.

Trust me,
utapoteza kila kitu na kufurushwa Kama mbwa kwenye familia yako mbele ya wanao.
 
Hatujui kulikuwa na mazingira gani ikawa hivyo lakini huenda kuna sababu ingawa simshauri aanike kila kiyu humu.

Yeye akajieleze kinagaubaga kwa Mwanasheria wajue kwa kuanzia.
Ukute alitelekeza mke wakat wa kuuguza
Maana ukifanya hivyo asee nguvu ya kudai ya mbeleni inakuwa ndogo
 
Kufiwa na mke si jambo rahisi kaka,hata mimi huwa najiuliza nilikubalije?I wish ungekuwepo siku hiyo,maybe ungekuwa msaada kwangu,nahitaji kutoka hapa sasa,msaada tafadhali.
Wewe msaada umeshapewa na wanajamvi tayari.

Wamekueleza kuwa tafuta mwanasheria uanzishe kesi mahakamani.

Tena kipengele cha kwanza kiwe ni kutengua usimamizi wa mirathi wa huyo jamaa, maana ni batili kisheria hastahili.

Cha pili abanwe kurejesha hayo makodi na rasilimali zingine alizojimilikisha bila ridhaa yako.

Ukweli ulioongea humu, usije ukaubeba kuupeleka mahakamani ukiwa ghafi, kaa na wanasheria wauchambue vizuri kabla ya kufunguliwa jalada.

Sidhani kama kuna msaada mwingine wa maana zaidi utaopata toka kwa wanajamvi zaidi ya ushauri wa msaada wa kisheria.

Na humu kuna miluzi mingi waweza kupoteza uelekeo kwa ushauri potofu pia.

Shaurika lakini mwisho wa siku, "changanya na zako".
 
Hapo nakubali kweli nilibugi,ila kutokana na hali niliyokuwa nayo wakati huo sikufikiria athari ambayo ingeweza kujitokeza baadaye,na tayari tatizo limejitokeza,ndiyo maana leo nipo hapa kuomba busara zenu ndugu zangu ili nijikwamue kutoka hapa,mbaya zaidi kuna vyumba vingine nilianza kuvijenga baada ya msiba,kwenye eneo hilohilo,na vipo kwenye hatua za ukamilishaji,ila amepiga makofuli vyote,kwa hiyo hata siwezi kuviendeleza,msaada jamani.
Wee jamaa mbona kama una mafanikio ila kilazaaa kinomaa Yani unakubali msimamizi wa mirathi awe Mtu mwingine na wew upo hai... shule shulee shuleee..
 
Nimekiri kukosea,nafanyaje sasa?mahakamani sitapata suluhisho?
Mahakamani nenda ukaeleze kwamba msimamizi wa mirathi anafanya tofauti ili atenguliwe au muwe wasimamizi wawili (wewe na yeye). Hyo inawezekana na nilishaona kwenye familia ambayo baba alioa mke zaidi ya mmoja wote wakawa hawaaminiani
 
Wee jamaa mbona kama una mafanikio ila kilazaaa kinomaa Yani unakubali msimamizi wa mirathi awe Mtu mwingine na wew upo hai... shule shulee shuleee..
Huyu jamaa anatia aibu Sana,

Inaonekana familia ya mke imeona kabisa jamaa hafai kusimamia Mali zilizoachwa na marehemu mkewe au vipi?

Kwanza ulionaga wapi MKE anafariki kinakaa kikao Cha mirathi?

Nnachojua mke akishafariki automatically Mali zote zinabaki chini ya mume, na ndo anacontroll kila kitu. Na hakuna mahojiano.

Sasa Huyu mwenzetu atwambie,
Kwenye hiyo familia Alikua marioo analelewa au vipi?
 
yanii simple mbona kwanza huyo bado hajawa msimamizi wa mirathi kisheria itakuwa bado hajaapa mahakamani hivyo nenda serikali ya mtaa kalalamike huko anaitwa then mkane na tumia hizo sababu kuwa huna imani nae kuwa hukubaliani na kile kikao cha familia then kiitishwe kikao kingine pindua meza akisogelea nyumba zako muitie mwizi.
 
Hapo nakubali kweli nilibugi,ila kutokana na hali niliyokuwa nayo wakati huo sikufikiria athari ambayo ingeweza kujitokeza baadaye,na tayari tatizo limejitokeza,ndiyo maana leo nipo hapa kuomba busara zenu ndugu zangu ili nijikwamue kutoka hapa,mbaya zaidi kuna vyumba vingine nilianza kuvijenga baada ya msiba,kwenye eneo hilohilo,na vipo kwenye hatua za ukamilishaji,ila amepiga makofuli vyote,kwa hiyo hata siwezi kuviendeleza,msaada jamani.
Mkuu,

Huu Ni mwendelezo wako kupuuzia baadhi ya mambo ya kimaamuzi Kama baba wa familia ili uonekane nice guy kwa mkeo na wakweo.

Nikisoma mlolongo mzima naona Hii mbegu ya hovyo uliipanda Tangu mkeo akiwa hai.

Mimi shemej zangu kwanza wananiogopa sana na hawanizoei kipumbavu.

Kwenye mambo ya kimaamuzi Lazima kwanza wajopange, wachutame ndo tukae meza moja..

Cha kufanya kwasasa,
Hebu uvae uanaume na onesha makucha yako Kama baba wa familia ile.

MAana tukisema uonyeshe makucha Kama mrithi Ni aibu Hii, MWANAUME huwezi kusema unapigania mirath ya mkeo.

Hili hata watoto wako wa kuwazaa lazma watakushangaa, "Huyu baba yetu vipi?"
 
Unajua kwanini nimekwambia vile? Kwasabb huna akili kabsa jambo jepesi kama hili unashindwaje kuchukua hatua? Mali za mkeo ni zako na watoto wenu lkn wewe upo tu unatembea umebeba kichwa kama mzigo.

Kama watoto unaishi nao maana yake hata Kama ungekuwa huna ndoa na huyo marehefu bado Mali zingekuwa ni za watoto wa marehemu ambao ni wako pia.

Wewe ni mjinga , ndiyo narudia tena wewe ni mjinga huyo shemeji yako ameshakuona fala ndiyo maana ameamua kufanya atakavyo.

Kifupi mali zote za marehemu alizochuma kabla na baada ya ndoa mwenye haki nazo kwa 100% ni watoto wake.

Kama bado hujui cha kufanya hao wanao wamesha kosa wazazi wote wawili.
Aisee,ujinga nimeukubali,mengine ntayashughulikia accordingly,asante mkuu.
 
Kuliko kuoa ndo ntafute Acha niendelee kupata mahitaji matatu muhimu kwa binadamu inayobaki nile mma nimwagilie moyo makesi kama haya unaeza jikuta unaumaliza mwendo kabla haujaisha
 
Mkuu UMUGHAKA ni mke wangu wa ndoa kabisa,ndoa ya kanisani,na vyeti via ndoa ninavyo,tumejaaliwa watoto wawili,wote wapo shule na vyeti vyao vya kuzaliwa ninavyo,mke wangu tulimzika nyumbani kwangu,hapa hapa ninapoishi sasa.
Pole sana kwa kumpoteza mke wako, na pia kwa changamoto unazopitia. Nilichojifunza kwenye hili tatizo lako, ni kwamba hamkuwa na serikali moja! Na ndiyo maana kumetokea hizo changamoto kwenye usimamizi wa hizo mali.

Kiufupi hakukutakiwa kuwa na mali za mke, au mali za mwanaume; mfano hivyo viwanja!!! Mali zote zilitakiwa za wote! Na hivyo wewe kama mume wa marehemu ulistahili kabisa kuwa msimamizi wa mirathi ya mke wako.

Na hiyo mirathi ilitakiwa igawanywe kwa kuwapa watoto zaidi mali za mama yao, halafu wewe na wazazi wa marehemu mngefuatia kwenye huo mgao. Hao ndugu wa marehemu, hawakuwa na ulazima wa kusimamia, wala kupata mirathi.

Ushauri; itisha kikao cha ndugu wa pande zote mbili ili mjadiliane, na kufikia muafaka. Kugombania mali za marehemu, siyo poa kabisa.
 
Back
Top Bottom