Je, MSD na Brig. Gabriel Mhidize, Itawezekana?

Je, MSD na Brig. Gabriel Mhidize, Itawezekana?

Ni kweli MSD au GPSA sio taasisi rahisi kabisa, ni ngumu na zina temptation nyingi sana na ni rahisi sana kutumika na wanasiasa wa juu. Ikiwemo na Waziri mwenyewe.

Ndio maana wengi wanashauri, kama Bwanakunu ameondolewa, basi kuna haja ya Ummy mwalimu nae kuchunguzwa. Hawa watu walifanya kazi kwa karibu sana: na moja ya findings katika Special auditing iliyofanyika MSD ni uhusiano wao kati ya Bahari Pharmacy, Ummy na Bwanakunu.

Sina shaka na taasisi ya Usalama juu ya kumpatia Rais taarifa sahihi. Ukisoma pia taarifa ya CAG, Assad ya mwaka 2018/19 utaona ameelezea vyema kuwa kuna upotevu wa pesa zaidi ya Bilion 30 ambazo hazijulikani zilipo na wala hazina nyaraka.

JPM ni Rais mwenye akili sana; atakuja kueleweka baada ya kuondoka madarakani. Mambo haya enzi ya JK yalikuwa yanamalizwa kishikaji unless kama umegusa maslaha yake ndio atakuondoa.

Mradi wa Delivery Pack alizokuwa anazitangaza Bwanakunu, ni mradi wa mtu binafsi kwa kushirikiana na Bahari Pharmacy na asilimia 90 ya vituo vya Afya walikuwa hawataki kabisa kununua huo upuuzi lakini ilikuwa ni lazima upewe na utozwe pesa kupitia akaunti yako kwa barua ya Ummy mwalimu.

Aidha, Ummy Mwalim na Bwanakunu na katibu Afya Dr. Zainabu wamefeli sana katika suala la COVID 19. Wao ndio sababu ya Watz kupigwa kwenye Sanitizer na Barakoa.

fikiria; kitu kama Sanitizer MSD imeshindwa kukidhi mahitaji ya wananchi: Nilishangaa sana Bwanakunu alipotangaza kuwa anatoa Sanitizer lita 350, 000 kutoka nje ya nchi.

Unaagiza lita 350,000 kati ya watu milioni 60 na Waziri wa Afya yupo amekaa kimya ! Katibu wa Afya yupo na amekaa kimya, Naibu waziri yupo na amekaa kimya, halafu tunamuona JPM mbaya. Hii safu yote ilipaswa kuondolewa.

Unaagiza Sanitizer nje ya nchi wakati tuna local manufacturers nyingi sana na hata hao MSD wenyewe wangekuwa wamejipanga kwa kushirikiana na Wizara ya Afya wangeweza kutengeneza Sanitizer. Zaidi ya lita Mil 5. Wameajiri Famasia, wanakazi gani

Ummy yupo busy sana; je kuna mtu anajua yupo busy na kazi gani? Mimi sijui.

Nimeridhika na uteuzi wa JPM juu ya Gabriel, kwanza ni Doctor( japo ilitakiwa awe Pharmacist lakini tofauti ni ndogo sana).

Nina elewa kwa undani nidhamu ya wanajeshi, tazama hiyo picha utaelewa ninachomaanisha.

View attachment 1440740

pamoja na hilo Brigedia atambue kwamba haitokuwa rahisi kuongoza taasisi kama MSD, haitokuwa rahisi hata kidogo, MSD ni taasisi yenye malalamiko na utendaji mmbovu kuwahi kutokea. Tangu na Tangu na kabla hata ya Bwanakunu.
View attachment 1440741

Kwa uzoefu wangu wa Global Health Supply Chain, nina mshauri yafuatayo ndugu Brig. General Dr Gabriel Mhidize;

1. Apendekeze kupanguliwa safu ya wakurugenzi, hasa Kurugenzi ya Ugavi, Kurugenzi ya Manunuzi na Kurugenzi ya Rasilimali watu. Akiendelea kufanya kazi na wakurugenzi hao, atatumbuliwa mapema kabisa

2. Akae na wakongwe wa MSD secretly wamsaidie kujua wale wote wanaohusika na dili fake; akishawajua awafanyie auditing pamoja na kuwahamisha au kuwasimamisha kazi.

3. Managers wa kanda, hawa ndio tatizo kubwa; Na hawa hawa ndio ninavyodhani wamemuangusha Bwanakunu,
View attachment 1440743
wachunguzwe Wote ikiwezekana tafuta watu utakaoweza kufanya nao kazi

4. Pata muda wa miezi 6 kusoma supply chain ya MSD, hili ni muhimu sana ili wasije kukuambukiza udokozi

5. Usiwe mtu wa kukaa ofisini tu, Tembelea ghala zote mara kwa mara na uwasikilize kwa makini watendaji wa warehouses, hao ndio wanamajibu sahihi ya MSD.

6. Malalamiko ya watu kuajiriwa kwa kujuana na kwa connections bila kufuata utaratibu wa utumishi usiyapuuze. Ni suala lipo na limelalamikiwa na wadau, rejea uzi hapo chini.

7. Kuwa karibu na Hospitali zote kubwa nchini Tanzania, jua mahitaji yao ya msingi. Kuna pesa nyingi sana zinapotea kwa hizi Hospitali kununua dawa nje ya MSD simply MSD haina uwezo wa kukidhi mahitaji yao.

8. kuwa makini sana na documents. Huenda waliomtoa Bwanakunu ni watu wa Bwanakunu.
View attachment 1440745

9. Weka macho sana warehouse , Finance na Manunuzi. Hiyo ndio MSD .

Ninaamini Utaweza na sina shaka juu ya Uteuzi wa JPM.

Nidhamu yenu huonekana hadi kwenye picha.
View attachment 1440746

Nitumainie kuona mabadiliko ya namna hii yafanyike na GPSA.
View attachment 1440740
Chanzo cha picha- MSD social media, nipashe online.

>>>>>>Nyuzi nyingine hapo chini zenye malalamiko ya muda mrefu kuhusu MSD na uteuzi wa Bwanakunu mwaka 2015 uliopenyezwa na kina Sefue bila ya kuangalia medical knowledge na Pharmaceutical Management skills za huyu bwana. MSD imepata jina sana kipindi cha uongozi wake; lakini ni kipindi ambacho kimekuwa na Great Depression kwenye upatikanaji wa dawa muhimu kuwahi kutokea huku Rais akiwapa dau la Bil 280.

1. Rais Magufuli amteua Brigedia Jenerali Gabriel Sauli Mhidize kuwa Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD)
Rais Magufuli amteua Brigedia Jenerali Gabriel Sauli Mhidize kuwa Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) - JamiiForums

2. Laurean Rugambwa - Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mteule wa Rais
Laurean Rugambwa - Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mteule wa Rais - JamiiForums


Tarehe 5, Mei 2020.



Mk54

Ulianza kama mtu mwenye point lakini inaonekana huna lolote zaidi ya majungu na fitina na chuki binafsi....umejificha nyuma ya MSD ili uweze kumshambulia Ummy


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Unaushahidi au unamsingizia tu duh jamani sijawahi kuona nchi ya kufitiniana kama hii !?!!

What do you mean kufitiana ? Wewe ndio unaushahidi wa kubisha. Kijana; hatufanyi mchezo hapa
 
Ulianza kama mtu mwenye point lakini inaonekana huna lolote zaidi ya majungu na fitina na chuki binafsi....umejificha nyuma ya MSD ili uweze kumshambulia Ummy


Sent from my iPhone using JamiiForums

Nothing personal. Usinishambulie, shambulia hoja.
 
MSD has been with such kind of Leaders; I know hence i have been there back then. Directorate ambayo imekuwa inafanya vizuri na hakuna uhuni mwingi ni IT chini ya Isaya Mzoro ambaye amestaafu na sasa yuko Bwanamdogo Pascal; Kidoogo na AuditThe rest of Directorate zimekuwa changamoto kwenye utendaji, zaidi sana mambo ya Uchafu wa kigongono since back then.

Tuangalie huyu mpya. Na Maguful ameshawaambia MSD inafanya biashara ya dawa . Inauza dawa tena kwa bei juu kuliko mtaani, halafu inataka serikali iwape fedha kila mwaka. Kitendo cha kumuweka Gabriel maana yake hakuna deni linalodaiwa kwa serikali.

Sasa waelewe wasipojipanga watakufa njaa. Serikali imesha disburse more than 200 B, wajiendeshe si wanauza dawa. Wanawataalamu wengi, wawatumie : sio kuwaweka wataalam Kwenye maa —-Excel na kupika pika data tu za uongo uongo; eti dawa zinapatikana asilimia 90, huku unasema unaidai serikali, are these people mad!!!

Hata USA upatikanaji wa dawa sio asilimia 90, ijekuwa TZ? Unaona kabisa these people were not serious.

MSD: Mh.JPM, mpaka sasa hatujapokea fedha za Serikali!

JPM: je upatikanaji wa dawa MSD ni asilimia ngapi?

MSD: ni asilimia 90 Mzee

JPM: Yaani una asilimia 90 ya dawa zako unasema hujapata fedha ? Je hizo dawa asilimia 90 ukiuza unapata shillings ngapi?

MSD: kama Bil 50 mzee

JPM : Asilimia 10 iliyopungua inathamani kiasi gani ?

MSD; Kama bili 15 mzee

JPM; Kwahiyo jumla ya fedha ya dawa unazohitaji ni bili 65 , lakin Mbona mpaka sasa nimeleta bil 180, halafu unasema unatudai na tukuongezee fedha?

MSD:: mmh mmh mmh

JPM: nitakuletea special audit , matokeo utayapenda.
 
MSD has been with such kind of Leaders; I know hence i have been there back then. Directorate ambayo imekuwa inafanya vizuri na hakuna uhuni mwingi ni IT chini ya Isaya Mzoro ambaye amestaafu na sasa yuko Bwanamdogo Pascal; Kidoogo na AuditThe rest of Directorate zimekuwa changamoto kwenye utendaji, zaidi sana mambo ya Uchafu wa kigongono since back then.
Tatizo la zinaa na uasherati litupiwe macho pale MSD
 
Naona kuna watu washatumbuliwa,JF ikitumika vizuri ni source nzuri sana.
 
IMG_2160.jpg
 
Ulianza kama mtu mwenye point lakini inaonekana huna lolote zaidi ya majungu na fitina na chuki binafsi....umejificha nyuma ya MSD ili uweze kumshambulia Ummy


Sent from my iPhone using JamiiForums

Vipi bado ni Personal attack au ?
 
Tunapoandika haya mambo sio wakati wote kila mtu yupo kwa ajili ya personal attack.

Wakati mwingine ni uzalendo uliokithiri. Step inayofuata kwa sasa ni GPSA. Pale napo akae mjeshi maana hizi procuring entity zina laana ya asili.

Brigedia Gabriel Sauli ni wakati wako wa kuangalia watu utakaoweza kufanya nao kazi.

Ni hatari kuendelea na wakurugenzi uliowakuta kwa sababu kuu mbili;

1. Wanaweza kutumika kuhakikisha unashindwa maana hapo kuna laana ya asili.
2. Wengi wamekaa ofisini muda mrefu bila mafanikio chanya; hakuna kitu kipya zaidi ya porojo porojo na ujanja ujanja tu , hivo hakuna watakachoweza kukusaidia kifanyike; zaidi watakuambia ngoja tuone kama ataweza. Kwa maana hiyo; kata huo uzi wote weka watu wapya wakiwa na akili ya Inawezekana.

Takukuru mambo ya kukamata watu na Mahakamani hawafiki nadhani tuache drama; watu wanatakiwa kuwajibishwa ili kuleta nidhamu katika utumishi wa umma.

Mnatakiwa kuwaanika kwenye public jamii ione namna Magufuli JPM anavyo kazi ngumu ya kubadili taifa hilo. Drama za kukamata watu na kumaliza kimya kimya ; na nyie tutawaundia tume ya uchunguzi hivyo kuweni makini.

Haiwezekani mtu mmoja awe na Bilioni ya hela huku yeye ni mtumishi wa umma. Rais anatoa dhamana kwa wazawa badala yake wazawa ndio wanakuwa mstari wa mbele kuhujumu. Kuna haja ya ku Track account zao zote hadi zile za fedha za kigeni.

Tanzania sasa rushwa basi. Maskini wasome.
 
Mkuu umeandika mazuri sana ila hapa ndipo umeharibu. MSD sio shirika la kuongozwa na Mfamasia tu. Mtu yeyote anaweza kulisimamia. Tena medical doctor kama yuko vizuri anaweza ongoza kwa ufanisi zaidi ya mfamasia.

MSD hawasambazi dawa tu, wanasambaza hadi vifaa vya maabara, mionzi n.k ambavyo mtumiaji mkuu ni daktari ambaye ana uelewa wake mkuu zaidi kuliko mfamasia. Lakini pia huyo daktari hata anajua dawa zipi zinahitajika. Sitaki tujikite kwenye hili, lakini msomi yeyote anaweza ongoza MSD.

Upo sahihi
 
Umeshindwa kutoa ushahidi zaidi ya kuharibu credibility ya JF. Hivi mtu mwenye akili timamu anaweza kuja na hoja za userengeti boys? Hapo ulionyesha utoto uliokithiri.

Vipi bado ni utoto ; haya nenda page ya Takukuru
 
Back
Top Bottom