Je, MSD na Brig. Gabriel Mhidize, Itawezekana?

Je, MSD na Brig. Gabriel Mhidize, Itawezekana?

Ni kweli MSD au GPSA sio taasisi rahisi kabisa, ni ngumu na zina temptation nyingi sana na ni rahisi sana kutumika na wanasiasa wa juu. Ikiwemo na Waziri mwenyewe.

Baada ya katibu mkuu hazina kumng’ata sikio JPM juu ya matumizi mabaya ya fedha za umma katika Bohari kuu ya dawa huku taasisi ikiendeshwa kingono na kuajiri kikanda na kujuana; JPM aka NGUVU , aliamua kufanya special auditing pale BOHARI: na moja ya findings katika Special auditing iliyofanyika MSD ni uhusiano kati ya Bahari Pharmacy, Ummy na Bwanakunu pamoja na wizi wa manunuzi ya dawa unaoitia Taifa hasara ya Billions huku vituo vya afya vikikosa Hata panadol.

Sina shaka na taasisi ya Usalama juu ya kumpatia Rais taarifa sahihi. Ukisoma pia taarifa ya CAG, Assad ya mwaka 2018/19 utaona ameelezea vyema kuwa kuna upotevu wa pesa zaidi ya Bilion 30 ambazo hazijulikani zilipo na wala hazina nyaraka.

JPM ni Rais mwenye akili sana; atakuja kueleweka baada ya kuondoka madarakani. Mambo haya enzi ya JK yalikuwa yanamalizwa kishikaji unless kama umegusa maslaha yake ndio ataondoka

Nimeridhika na uteuzi wa JPM juu ya Gabriel, kwanza ni Doctor( japo ilitakiwa awe Pharmacist lakini tofauti ni ndogo sana).

Nina elewa kwa undani nidhamu ya wanajeshi, tazama hiyo picha utaelewa ninachomaanisha.

View attachment 1440740

pamoja na hilo Brigedia atambue kwamba haitokuwa rahisi kuongoza taasisi kama MSD, haitokuwa rahisi hata kidogo, MSD ni taasisi yenye malalamiko na utendaji mmbovu kuwahi kutokea. Tangu na Tangu na kabla hata ya Bwanakunu.
View attachment 1440741

Kwa uzoefu wangu wa Global Health Supply Chain, nina mshauri yafuatayo ndugu Brig. General Dr Gabriel Mhidize;

1. Apendekeze kupanguliwa safu ya wakurugenzi, hasa Kurugenzi ya Ugavi, Kurugenzi ya Manunuzi na Kurugenzi ya Rasilimali watu ambayo ndio inaongoza kuajiri mabogus kwa minajili ya kujuana na kikanda. Afaham kuwa Akiendelea kufanya kazi na wakurugenzi hao, atatumbuliwa mapema kabisa kwa Sababu watamuangusha. Kwanza kwa nini mtu akae ofisini miaka 10 ? Mtu kama huyo hawezi kuwa na mawazo mapya zaidi ya uzoefu, ondoa hizo takataka zote.

2. Akae na wakongwe wa MSD secretly wamsaidie kujua wale wote wanaohusika na dili fake; akishawajua awafanyie auditing pamoja na kuwahamisha au kuwasimamisha kazi.

3. Managers wa kanda, hawa ndio tatizo kubwa; Na hawa hawa ndio ninavyodhani wamemuangusha Bwanakunu,
View attachment 1440743
wachunguzwe Wote ikiwezekana tafuta watu utakaoweza kufanya nao kazi changanya na wajeshi humo humo

4. Pata muda wa miezi 6 kusoma supply chain ya MSD, hili ni muhimu sana ili wasije kukuambukiza UDOKOZI NA DILI FAKE, NA UKANDA.

5. Usiwe mtu wa kukaa ofisini tu, Tembelea ghala zote mara kwa mara na uwasikilize kwa makini watendaji wa warehouses, hao ndio wanamajibu sahihi ya MSD.

6. Malalamiko ya watu kuajiriwa kwa kujuana na kwa connections bila kufuata utaratibu wa utumishi usiyapuuze. Ni suala lipo na limelalamikiwa na wadau, na ndio chanzo cha utendaji mmbovu MSD, rejea uzi hapo chini.

7. Kuwa karibu na Hospitali zote kubwa nchini Tanzania, jua mahitaji yao ya msingi. Kuna pesa nyingi sana zinapotea kwa hizi Hospitali kununua dawa nje ya MSD simply MSD haina uwezo wa kukidhi mahitaji yao.

8. kuwa makini sana na documents. Huenda waliomtoa Bwanakunu ni watu wa Bwanakunu.
View attachment 1440745

9. Weka macho sana warehouse , Finance na Manunuzi. Hiyo ndio MSD .

Ninaamini Utaweza na sina shaka juu ya Uteuzi wa JPM. Hapa Kazi Tu , JPM ndio Rais wangu na anawakilisha mioyo ya watanzania wengi , JPM aka NGUVU

Nidhamu yenu huonekana hadi kwenye picha.
View attachment 1440746

Nitumainie kuona mabadiliko ya namna hii yafanyike na GPSA.
View attachment 1440740
Chanzo cha picha- MSD social media, nipashe online.

1. Rais Magufuli amteua Brigedia Jenerali Gabriel Sauli Mhidize kuwa Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD)
Rais Magufuli amteua Brigedia Jenerali Gabriel Sauli Mhidize kuwa Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) - JamiiForums

2. Laurean Rugambwa - Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mteule wa Rais
Laurean Rugambwa - Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mteule wa Rais - JamiiForums

Tarehe 5, Mei 2020.

Mk54
Majungu at work.
Kwanza ati ondoa wakurugenzi waliokaa miaka 10.
Pili utuendeleze na kutusikia sisi wazoefu.!
MAN, jungu la maskahi hilo.Cha maana hata mleta mada futilia mnali
 
Mgodini ajali ni nyingi mwaka huu nimepeleka majeruhi mountmeru,mmoja sasa ni marehemu dawa hakuna inabidi ukanunue mjini,hakuna jipya sasa hivi tumerudi kcmc ndio uhakika

Pamoja na kuwekwa Mjeshi; Nasema hivi serikali itafute Mbadala wa MSD.

Haitokuja kutokea MSD kukidhi mahitaji ya vituo vyote vya Afya na Hospital. It has been proven failure beyond the reasonable doubts. Na Ukweli ni kwamba MSD is very busy place lakini je ubize wao una impact gani katika upatikanaji wa Dawa ? Zero ! Matokeo yake wanaiba dawa hizo hizo.

MSD ivunjwe; MJESHI nae anaonekana ana shindwa. Yaani miaka yangu 5 ya Halmashauri, sijawahi kuona umuhimu wa MSD. Asilimia kubwa ya Dawa tulikuwa tunanunua Mtaani.
 
Huyu Vick sifa yake kubwa anajua robbing sana kapiga pesa sana za ma supplier , mtu wa njama njama sana aliifanya msd kama ya kikanda akamponza muhaya bure eti naskia kapewa shavu bodi ya korosho jamani muwe waangalifu nyie wa utumishi

Ndiyo kaenda huku ?

Bodi ya Korosho ni Shavu? Anaenda kufanya nini , Bodi yenyewe haina hela na imeshakufa. Mimi ndio manaa niliwahi kuacha utumishi wa umma. Mtu kama huyo amepiga sana now arudi home akasimamie miradi yake, kuna seniors position wengi , wapandishwe hao. Sio mtu mmoja azunguke kwenye taasisi hadi afie madarakani

Ndio maana nasema hata huu utumbuaji nao ni jipu
 
Mleta maada msimamo wako bado ni ule ule?

Waziri amesema kuna watu wanataka kumuangusha Mjeshi. Ila Sitegemei kuona mabadiliko yoyote chini ya Mjeshi kama mpaka leo Waziri anaonesha wasiwasi Na MSD.

Wanasema anajaza sana wanajeshi; suali la maana ni je , hao anaowajaza wanauwezo. ?

Awe makini na hili maana Utumishi wa Umma Una taratibu zake; Na wanajeshi huwa sio watu permanent kwenye taasisi. Je mabadiliko anayoyafanya ni endelevu au ndio hivo hivo tu
 
Huyo mchepuko wa dada ya Korona Bwanakunu bado yupo gerezani mpaka leo? Jamaa tajiri sana yaani akitoka ni kutanua tu. Nchi hii bana

Shida ni nchi au watu?
Huyo kwenye picha ni wewe ?
 
Waziri amesema kuna watu wanataka kumuangusha Mjeshi. Ila Sitegemei kuona mabadiliko yoyote chini ya Mjeshi kama mpaka leo Waziri anaonesha wasiwasi Na MSD.

Wanasema anajaza sana wanajeshi; suali la maana ni je , hao anaowajaza wanauwezo. ?

Awe makini na hili maana Utumishi wa Umma Una taratibu zake; Na wanajeshi huwa sio watu permanent kwenye taasisi. Je mabadiliko anayoyafanya ni endelevu au ndio hivo hivo tu
Msd huyu bwana anaiweza, kikubwa tu madeni yote ya msd yalipwe ili msd nae awalipe wanao mdai ndio hali itatulia. Pia waendelee kuipanga msd kimkakati, KUNA uozo Sana wa staffing pale msd. Watu wanapangwa kazi wasizo na ujuzi nazo kisa kubebana HR team ovyo kabisa pale wapowapo tu inatakiwa kusafisha hiyo idara. Sasa kapelekwa hr director mpya yule wa madili katolewa, huyu mpya awahamishe hivyo vidada pale hawana upeo kabisa, KUNA mmoja anaitwa Siku yeye anafanyaga kazi Kama analazimishwa, useless kabisa wahamishiwe taasisi zingine maana ndio wamepanga watu wao , vyeo vya kupendelea , HAMISHA BILA HIVYO HALI HAITABADILIKA, PIA INTERNAL AUDITOR inaishi kimazoea , Idara ya tehama hivyo hivyo hazina msaada zaidi ya hasara tu, wananunua mifumo ya hovyo kabisa ya kidilidili bar code, hcm etc yote kwa mabilioni na haifanyi kazi kiufanisi. Hcm epicor portal ilikuwa hacked na taarifa zake hazina usalama,bado wamelirudisha mnaendelea nalo. Safisha
 
Yupo nje. Nchi ilijaa waongo na wazandiki. Kwanini mliwazushia hawa watu?
 
Je MSD inashida gani? Huyu nae si tulimuamini?

Imekuaje anafanya madudu ?
 
Yupo nje. Nchi ilijaa waongo na wazandiki. Kwanini mliwazushia hawa watu?

Walimuondoa bwanakunu wakaleta wajeshi . Binafsi sijawahi kuamini utendaji wa wajeshi.

Huwa wakienda mahali wanajiona wao wazalendo
 
Msd huyu bwana anaiweza, kikubwa tu madeni yote ya msd yalipwe ili msd nae awalipe wanao mdai ndio hali itatulia. Pia waendelee kuipanga msd kimkakati, KUNA uozo Sana wa staffing pale msd. Watu wanapangwa kazi wasizo na ujuzi nazo kisa kubebana HR team ovyo kabisa pale wapowapo tu inatakiwa kusafisha hiyo idara. Sasa kapelekwa hr director mpya yule wa madili katolewa, huyu mpya awahamishe hivyo vidada pale hawana upeo kabisa, KUNA mmoja anaitwa Siku yeye anafanyaga kazi Kama analazimishwa, useless kabisa wahamishiwe taasisi zingine maana ndio wamepanga watu wao , vyeo vya kupendelea , HAMISHA BILA HIVYO HALI HAITABADILIKA, PIA INTERNAL AUDITOR inaishi kimazoea , Idara ya tehama hivyo hivyo hazina msaada zaidi ya hasara tu, wananunua mifumo ya hovyo kabisa ya kidilidili bar code, hcm etc yote kwa mabilioni na haifanyi kazi kiufanisi. Hcm epicor portal ilikuwa hacked na taarifa zake hazina usalama,bado wamelirudisha mnaendelea nalo. Safisha

Je ameiweza ?
 
Waziri amesema kuna watu wanataka kumuangusha Mjeshi. Ila Sitegemei kuona mabadiliko yoyote chini ya Mjeshi kama mpaka leo Waziri anaonesha wasiwasi Na MSD.

Wanasema anajaza sana wanajeshi; suali la maana ni je , hao anaowajaza wanauwezo. ?

Awe makini na hili maana Utumishi wa Umma Una taratibu zake; Na wanajeshi huwa sio watu permanent kwenye taasisi. Je mabadiliko anayoyafanya ni endelevu au ndio hivo hivo tu

Mjeshi hakuwahi kuwa na uwezo. Msd hakununui risasi
 
Ndiyo kaenda huku ?

Bodi ya Korosho ni Shavu? Anaenda kufanya nini , Bodi yenyewe haina hela na imeshakufa. Mimi ndio manaa niliwahi kuacha utumishi wa umma. Mtu kama huyo amepiga sana now arudi home akasimamie miradi yake, kuna seniors position wengi , wapandishwe hao. Sio mtu mmoja azunguke kwenye taasisi hadi afie madarakani

Ndio maana nasema hata huu utumbuaji nao ni jipu

Kabisa
 
Back
Top Bottom