Je, mmiliki halali wa Mtoto ni Baba au Mama? Au wote wawili?

Habari?.

Nauliza hivo kwa sababu nimekuwa nikisikia hizi kauli kutoka kwa wanaume "kama unaondoka nenda lakini usiondoke na MTOTO WANGU" .

Ina maana nyie wanaume ndio wamiliki wa mtoto aliyezaliwa na mama hana haki na huyo mtoto?. Kwanini msiseme "mtoto wetu"?
Ukiingiza kadi kwenye atm machine ikatoa pesa je pesa ni za atm au ww ulieingiza iyo kadi?
 
1. Kama kuna umiliki wa mtoto, then mmiliki wake ni mama kwa sababu mtoto anapozaliwa huwa ameunganika naye kupitia 'umbilical cord' na hutungwa na hukua ndani ya mfuko wa uzazi wa mama na hatimaye huzaliwa naye.
2. Ukiacha 1, mtoto ni wa wazazi wote wawili kwa sababu hakuna anayeweza kumpata akiwa peke yake - mpaka wote wawili 'wakutane kimwili na waweze kutoa kwa mwanaume mbegu hai na kwa mwanamke yai' ambayo huzaa 'foetus' na hatimaye kuwa mtoto.
 
Ukiingiza kadi kwenye atm machine ikatoa pesa je pesa ni za atm au ww ulieingiza iyo kadi?
Huu mfano naona siyo kabisa! Ukiingiza kadi kwenye ATM ikitoa pesa, pesa ni zako. Lakini kati ya 'mtu' anayeingiza 'kadi' kwenye 'ATM mashine' na kisha pesa kutoka, mfumo wake siyo sawa na baba na mama kumzaa mtoto. Kwa nini? Kwa sababu siyo wote wanaooana wanabahatika kupata watoto. Uzazi siyo automatic hivyo na kama baba ndiye mwenye mtoto basi angeweza hata kumpata kutoka kwenye jiwe, mti, udongo au hata kutoka kwa kuku, bata, mbuzi, nyati etc.
 
Hiyo dhana kuiondoa ni ngumu maana siku zote inaonekana mwanaume ndie anaeendeleza ukoo wake na mwanamke anatumiwa kuendeleza ukoo wa mtu mwingine.

Hii inapelekea mtoto kuonekana ni wa mwanaume zaidi ukiachilia matrelinial societies ambapo kwa bongo zipo chache
Mtoto anamilikiwa na wote.
Bila baba na mama kuungana hakuna mtoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiasili mtoto ni wababa yaani Mwanaume. Mwanamke hana mtoto bali huzaa watoto.

Siku hizi mtoto ni mali ya jamii yaani serikali.

Binafsi, mtoto ni mali ya Baba ikiwa baba anatimiza majuku yake. Pia mtoto ni mali ya mama ikiwa Mama anatimiza majukumu yake.

Kindoa, mtoto ni mali ya Baba ikiwa mama yupo ndani ya ndoa, alitoa mahari na kufunga ndoa. Mtoto ni mali ya mama ikiwa mama hakufunga ndoa na Baba.

Ikiwa mwanaume umemzalisha binti wa watu kisha akazaa mtoto, yule mtoto atakuwa wa mama yaani upande wa kiukeni, mpaka pale Mwanaume utakapoenda kumkomboa huyo mtoto kwao mwanamke kulingana na utamaduni husika wa kwao mwanamke.

Wanawake wengi siku hizi wanamiliki watoto kwani wengi walizalishwa alafu wanaume wakawatelekeza bila ndoa wala matunzo.
 
Huu mfano naona siyo kabisa! Ukiingiza kadi kwenye ATM ikitoa pesa, pesa ni zako. Lakini kati ya 'mtu' anayeingiza 'kadi' kwenye 'ATM mashine' na kisha pesa kutoka, mfumo wake siyo sawa na baba na mama kumzaa mtoto. Kwa nini? Kwa sababu siyo wote wanaooana wanabahatika kupata watoto. Uzazi siyo automatic hivyo na kama baba ndiye mwenye mtoto basi angeweza hata kumpata kutoka kwenye jiwe, mti, udongo au hata kutoka kwa kuku, bata, mbuzi, nyati etc.
Ata kwenye atm sio mara zote pesa itatoka, kuna saa inakataa. Kifupi mtoto ni mali ya baba
 
Ata kwenye atm sio mara zote pesa itatoka, kuna saa inakataa. Kifupi mtoto ni mali ya baba
Kama ni mali ya baba si angempata sehemu yoyote ambayo angeweza kumpata? Kwa nini iwe kwa mwanamke tu? Mtoto ni wa wazazi wote wawili, lakini kama tukisema ni wa mzazi mmojawapo basi ni wa yule anayekaa naye muda mrefu tumboni na pia aliyeunganika naye katika mfumo wa kula na kuvuta hewa akiwa bado hajazaliwa.
 
Lazima ang'ang'anie kwa sababu ni mwanae na wewe ukitaka mng'ang'anie ni mwanao pia.
Hilo neno mwanangu lisikutishe.hata wewe unaweza ukamwita tu.
Utakuwa una gubu wewe maana hata sijaona sababu ya msingi hapo.
Kweli haujaona sababu ya msingi?
 
Upo sahihi

Very correct.

Ila kwa jinsi wanawake wanavyokuja na hivi movements za feminism,mzee,the whole world will be feminine.

Feminism is a big problem!
Yeap mbaya zaidi ni kwa wengine wanaoidaka juu kwa juu pasipo kuelewa ina maana gani !!

Wengi wanafikiria ni kubadilisha gender roles ama kumfanya mwanamke kuwa juu ya mwanaume kuliko kutengeneza equal access to available opportunities
 
Mtoto anamilikiwa na wote.
Bila baba na mama kuungana hakuna mtoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo ni kibailojia ila ukirudi kijamii mtoto ni mali ya ukoo wa baba na ndio maana anachukua ubin wa baba yake na hata mwanamke akishaolewa anabadili ubin wake kwenda kwa ukoo wa mwanaume, Hii inaamaanisha kashachukuliwa ili kuendekeza ukoo wa mwanaume hivyo, hata watoto pia inakuwa the same...
 
Kuchukua ubin wa baba haimaanishi kwamba mtoto Ni wa Baba pekeyake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom