Je, mmiliki halali wa Mtoto ni Baba au Mama? Au wote wawili?

Habari?

Nauliza hivo kwa sababu nimekuwa nikisikia hizi kauli kutoka kwa wanaume "kama unaondoka nenda lakini usiondoke na MTOTO WANGU" .

Ina maana nyie wanaume ndio wamiliki wa mtoto aliyezaliwa na mama hana haki na huyo mtoto?. Kwanini msiseme "mtoto wetu"?

Habari Sheillah Sheillah, iko hivi!!!

Inategemea na mukhtadha wa mazungumzo, yaani mlikuwa mnazungumza nini kuhusu huyo mtoto, mfano.

Kimila, Kwa makabila mengi ya kiafrika likiwemo na la kwangu, mtoto anakuwa mali ya Mama ikiwa amezaliwa nje ya ndoa yaani Baba wa mtoto huyo hajulikani rasmi nyumbani kwa wazazi wa mwanamke. Mtoto huyo ataanza kutambulika rasmi kuwa ni wa Baba pale Baba huyo atakapoenda ukweni kujitambulisha kuwa ndiye aliyempa mimba binti yao na kuwa tayari kulipa faini na mambo mengine atakayoelezwa.

Kijamii, Mtoto ni wa jamii nzima (Jamii = Serikali) pale anapokuwa anaishi iwe na wazazi wote au mmoja ndiyo maana huwezi kuamua kumuua mwanao na serikali ikakuacha eti kwa kuwa umemzaa wewe, lazima ushitakiwe.

Kisayansi mtoto ni wa Baba kwa kuwa ndiye anayetoa mbegu ambayo huenda kukutana na yai la Mama na hatimaye mimba kutungwa (ni kama vile shambani mwenye mbegu ndiye huotesha mazao). Lakini pia Mwanaume kupitia mwili wake ndiye anayeweza kuamua ni mtoto jinsia gani azaliwe (invorluntary action) maana yeye ana "X" na "Y" lakini mwanamke ana "X" na "X" hivyo kisayansi Mwanaume amepewa mamlaka hayo. Mwanamke ni msaidizi wa mwanaume hivyo katika ndoa hata yeye ni mali ya Baba (anamilikiwa na Mume)

Inapotokea wazazi kutengana sheria imeweka busara kuwa watoto wadogo wataishi na mama yao kwa kuwa kisayansi mama ndiye mwenye matiti yanayotoa maziwa kuwezesha watoto kupata chakula chao (kama ni wachanga) lakini pia kwa mihangaiko ya Wanaume si rahisi kuishi na mtoto mdogo. Ndiyo maana wao (wababa) sheria zinawabana kutoa fedha za matunzo zaidi. Mwanamke ni mzazi msaidizi lakini mzazi mkuu ni Baba.

Binafsi nahisi MUNGU aliwapa umiliki Wanaume ili kuwafunga wasikimbie majukumu kama jogoo anavyokimbia majukumu mtetea akiangua vifaranga.

NB: Wanaume wasiojitambua ndiyo hukimbia majukumu.
 
Back
Top Bottom