mngony
JF-Expert Member
- Jul 27, 2012
- 5,222
- 6,412
Sote tunajua kuwa tatizo la ajira ni kubwa nchini na sekta binafsi (rasmi na zisizo rasmi) zimeajiri watu wengi hasa vijana kuliko serikali kwa ujumla.
Ghafla tu wanazifunga, hata kuwakumbusha, kuwapa maelekezo au kutoa onyo. Kwani tunamkomoa nani? Serikali inakomoa Raia wake?
Kutojua sheria sio kigezo cha kuvunja sheri ila kwanini isitumike busara kuliko kufungia biashara na kuathiri ajira za vijana wengi, hapo kuna wahudumu, kuna bodaboda, kuna wafanya usafi, kuna walinzi n.k
Maisha yenyewe ni magumu tayari kwa vijana wengi na mnazidi kuyafanya ya we mugumu zaidi kwa makusudi. Halafu hao hao mtataka 2025 wawape ridhaa, wakati mnazidi kuwaumiza hata pale wanapojitahidi kujikwamua kupitia sekta zisizo rasmi.
Serikali inatakiwa kushawishi ukuaji wa sekta binafsi huku ukizikumbusha kufuata sheria ma taratibu za nchi ili kutoa fursa za ajira watanzania wengi.
Au labda kuna tusiyoyajua ya siri yaliyojificha chini ya maamuzi haya.
Tofauti na hapo hizo ni kukomoana kuhujumu serikali kwa kutengeneza taharuki kwa kundi kubwa la vijana waliokuwa wakitegemea hizo sekta zisizo rasmi kwa ajili ya kipato chao cha kila siku na pia kutengeneza mazingira ya rushwa ili wamiliki waweze kuendelea na huduma.
Na chondechonde RC wa DSM na Mkurugenzi baraza la NEMC, mlitoa kauli kuwa na nyumba za ibada nazo zinapiga kelele na kudai malalamiko ya watu yamekuwa makubwa, hilo ni suala nyeti mno BUSARA ni kitu kikubwa katika kukabiliana na matatizo yanayohusu sehemu kubwa ya jamii, kitu ambacho baraza la NEMC limeonekana kutokuwa nacho kwa makusudi.
Hivi huwa mnakaa na kujadili athari za maamuzi yenu kwa jamii? Hamjali taharuki mnayoweza kuzua kwa maamuzi ya kukurupuka?