Gift mzalendo
JF-Expert Member
- Dec 13, 2019
- 1,006
- 1,171
Heshima kwenu wanajukwaa,
Kwanza nitangulize shukrani kwa vyama vya upinzani ambavyo vimeendelea kuonyesha ushindani kwa chama tawala.
Ndugu wanajukwaa moja ya Jambo ambalo naamini, ni kwamba watanzania au kawaida binadamu wanapenda sana mabadiliko kwa Kila eneo. Katika hulka hii ya binadamu hubadilisha kwa lengo la kupata kitu Bora zaidi ya kile alichonacho na huku ndiko tunapata neno maendeleo.
Kabla ya kubadili huhitaji yafutayo
1.Kuamini kuwa atapata kitu Bora zaidi ya kile alichonacho
2.Kile kitu kitampa Unafuu wa maisha yake kwa kiwango gani zaidi
3.Uimara wa kitu kipya
4.Kudumu kwa muda gani
Moja ya maswali ambayo naamini watu wengi wanajiuliza
Je, tukiwapa upinzani nchi wataweza kuhandle nchi na mifumo yake yote?
Je, mifumo ya vyama upinzani ina uwezo wa kusimamia mifumo mingine ya nchi?
Je, ina uimara kiasi gani ya kusimamia nchi na mifumo yake bila mifumo yake yenyewe kubomoka (collapse)?
Je, imeandaa watu wake kwa kiasi gani ambao watakuwa mbadala was viongozi waliopo na kuleta mabadiliko?
Nikiri tu Mimi Ni muumini wa mifumo imara na muumini wa vyama vingi vinavyoshindana kwa sera na hoja. Ni miongoni mwa watu wanaotamani kuona tunakuwa na vyama mbadala ambavyo vinabadilishana madaraka Kila inapobidi, ili kuleta ushindani wa kimaendeleo. Leo kinaongoza chama A kikiboronga kinaongoza B nk.
Maoni yangu
Moja vyama vya viimarishe mifumo yao Kwanza, nafikiri tunaona vyama vikishindwa kubeba hata baadhi ya wanachama wao wanaohamia wenye umaaeufu.
Pili viimarishe demokrasia yao ya ndani.
Tatu viweke mpango wa kuimarisha uchumi wake, kwa kuwa na vyanzo halali vya mapato, Hili nasisitiza hi Ni moja ya sababu kuu ya kufa kwa vyama vya upinzani na hata kuharibu misimamo ya viongozi wake na kuonekana kituko.
Nne vyama viwe na mfumo wake wa kuandaa viongozi na watendaji wake.
Tano wekeni kando ubinafsi mtuundie umoja wa vyama madhubuti au chama kimoja Cha upinzani
Imarisheni na kupanua mifumo yenu tuamanisheni wananchi mtakuwa mbadala wa chama kilichopo.
Wananchi wawape ridhaa kuongoza
Hayo ni maoni yangu machache