Je, Marekani ni Koloni la Wayahudi? Pima mwenyewe

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
20,897
63,783
"Every time we do something you tell me America will do this and will do that. I want to tell you something very clear: Don't worry about American pressure on Israel. We, the Jewish people control America, and the American knows it"- Former Israel Prime Minister Ariel Sharon, October 3, 2001, to Shimon Perez, as reported on Kol Yisrael radio.

Mwaka 1967 Israel iko kwenye vita kali dhidi ya mataifa ya kiarabu yakiongozwa na Misri (Six-days War). Wayahudi wakaona kuwa watazidiwa na kupigwa , wakaamua kwenda kulipua Manowari kubwa ya kivita ya Marekani (USS LIBERTY) . Shambulizi lilikuwa la majini na angani; ndege aina ya Mirage za mfaransa na makombora ya majini zililipua mabomu kwa zaidi ya masaa mawili.
Wanajeshi 34 walikufa huku 174 wakiwa majeruhi. Yote haya yalidhaniwa kuwa yamefanywa na serikali ya Misri kwasababu ilikuwa na ugomvi na Marekani.

Ikumbukwe manowari hiyo ilikuwa na bendera ya Marekani kwenye mlingoti wake kama Mkataba wa Sheria za baharini wa mwaka 1982 (UNCLOS) unavyotaka. Serikali ya Marekani inasema mlingoti ulikuwa na urefu wa mita 8 kiasi cha kufanya bendera ionekane kwa mbali hata na watu kutoka angani. Jambo jema kabisa ni kwamba siku hiyo hali ya hewa ilikuwa shwari kutoweza kuwazuia wanajeshi wa kiyahudi kuitambua hiyo manowari.

Kifupi tu kwenye Vitabu ya kufundishia wanajeshi (MILITARY MANUAL) kuna kitu kinaitwa Collateral Damage Estimate Methodology (CDE) , ni mbinu ambayo kila kamanda wa jeshi anatakiwa kujua. Ndani ya CDE kuna vitu viwili vikubwa MISSION and BALLISTIC; kwenye MISSION tunaangalia aina ya shambulizi unalotakiwa kufanya, mazingira , raia, shabaha n.k.
Upande wa BALLISTIC tunaangalia silaha zitakazotumika kufanikisha shambulizi. Kamanda huwezi kuruhusiwa kufanya shambulizi bila kujiridhisha na hivi vitu.

Mkataba wa pili wa Geneva (Second Geneva Convention) wa mwaka 1949 unaohusiana na Vita vya majini katika Ibara ya 18 inasema baada ya kufanya shambulizi la vita dhidi ya chombo cha adui ni lazima ufanye kila uwezalo kuwakusanya ikiwa pamoja na kuwaokoa na mara tu kuwafanya wawe mateka wa kivita. Hili halina mjadala kwasababu kila nchi ya dunia hii imesaini huu mkataba wa kimataifa na kutotii kutaleta kosa la uhalifu wa kivita.

Sasa jeshi la Israel liliyajua haya yote lakini wao walianza na kulipua njia za mawasiliano za manowari hiyo. Mosi, kwenye CDE kuna nyaraka za mawasiliano zilivuja zikionyesha jinsi gani rubani wa kiyahudi akisema kwamba Manowari ni ya Marekani na aliuliza mara tatu lakini akaambiwa wewe lipua. Pili, kwenye sheria za vita wanajeshi wakiwa wanazama hurusiwi kuwaacha wafe kwenye maji, lakini wayahudi baada ya kulipua waliendelea kulipua mitumbwi na pantoni ndogo walizopanda wanajeshi wa Marekani ili kunusuru maisha yao.

Wanajeshi wengi walilikufa wakiwa wanajaribu kutoroka lakini wachache walifanikiwa kupata antenna ya dharura na kutuma ujumbe wa hali ya hatari (Distress Signal). Maiti zilikutwa na matundu mengi ya risasi kama chujio. Kwa kifupi walipondwa sana.

Baada ya taarifa kufika Washington DC, wakati huo raisi akiwa ni Lyndon B. Johnson. Ndege zenye silaha za kinyuklia zilipewa amri ziende zikadondoshe mabomu Cairo kwenye mji mkuu wa Misri. Taarifa rasmi zilifika karibu na dakika za mwisho kwamba shambulizi limetoka Tel Aviv na siyo Cairo, hivyo jamhuri ya Mafarao wa Misri ikapona kimiujiza.

Mengi yalisemwa lakini Israel ikasema kwamba lile ni shambulizi la bahati mbaya, kwasababu wao walidhani kuwa ile ilikuwa ni manowari ya Misri El Quseir. Lakini maswali yalikuwa ni kwanini Isrel ilibandua alama za bendera yake kwenye meli na makombora yake kinyume kabisa na tamaduni za vita?
Swali jingine ni kwamba manowari ya Misri El Quseir ni ya mwaka 1920 hata kabla ya Misri kupata uhuru toka kwa wazungu na kibaya zaidi ilikuwa ni ndogo mara nne ukilinganisha na U.S.S Liberty na cha kusikitisha ilikuwa siyo manowari ya kivita.

Zifuatazo ndizo kauli zilizotolewa na watu wakubwa kwenye serikali ya Marekani:

" I was never satisfied with the Israel explanation. Through diplomatic channels we refused to accept their explanations. I didn't believe them then, and i don't believe them to this day. The attack was outrageous"- Dean Rusk, U.S Secretary of State

" The evidence was clear. Both Admiral Kidd and I believed with certainty that this attack was a deliberate effort to sink an American ship and murder its entire crew. Not only did the Israelis attack the ship with napalm, gunfire and missiles. Israel torpedo boats machine gunned three life boats that had been launched in an attempt by the crew to save the most seriously wounded- A war Crime." - Captain Ward Boston, U.S.S Liberty investigation crew.

" Few in Washington believed that the ship had not being identified as an American naval vessel"- C.I.A chief Richard Helms

Hizi nikuu ni chache tu na zinaonyesha ni jinsi gani Wamarekani hawakufurahsihwa na hicho kitendo kiovu cha serikali ya Israel. Yote yalisema na hata raisi alionesha kutoridhishwa nacho lakini mwishoni shinikizo lilivyokuwa kubwa bwana Lyndon B. Johnson akasema mbele ya Ummah wa dunia kwamba "We cannot shame our ally" na aliendelea kupeleka misaada mingi ya kijeshi huko Israeli.

Kwa mtizamo wa juu mtu unaweza kusema hiki ni kitendo cha kisiasa tu, na kisingeweza kuleta madhara makubwa hata kama kingefanikiwa. Ikumbukwe tu miaka mitano nyuma ya SIX-DAYS WAR: Mwaka 1962 dunia ilitaka kushuhudia vita vya kinyuklia ambavyo vingeanzia Cuba, baina ya NATO na WARSAW PACT. Wataalamu wanasema vingekuwa ni vita vya tatu vya dunia, lakini Mungu aliepushia mbali kabisa.

Misri ya chini ya Jenerali Gamal Nasser ilikuwa na urafiki mkubwa sana na Jamhuri ya Kisovyeti ya Urusi kama ilivyokuwa CUBA. Marekani angelipua Cairo kwa silaha za Kinyuklia na kuua mamilioni ya watu kimakosa unategemea naye angekuwa salama?
Lakini kitendo kama hichi alikifanya Japan mwaka 1941 pale Hawaii, aliomba msamaha na kukubali kusalimu amri lakini Harry Truman alilipua Hiroshima na Nagasaki. Uzuri kipindi kile Moscow , Washington na London walikuwa upande moja hivyo haikuleta tatizo sana.

Nimalize kwa kusema hebu pima mwenyewe uangalie kama kauli ya Ariel Sharon ina ukweli wowote.
Tukipata wasaha tena tutamzungumzia raisi Richard Nixon , Skandali ya Water Gate na ugomvi wake na wayahudi na tutapitia vitu alivyosema kuhusu wao. Maoni ya F.B.I juu ya Shambulio la Kigaidi la tarehe 11 mwezi Septemba. Ugomvi wa Wayahudi na Raisi Kennedy, Roosevelt na Harry Truman.

Kwa kuelewa zaidi hebu pitia hii link:The Day Israel Attacked America
Ni filamu maalum iliyotengenezwa na kituo cha habari cha Al-Jazeera.
Hii historia imefichwa na mara nyingi Wamarekani huwa hawapendi kuizungumzia.

Kupitia chaneli ya youtube:


Tafadhali naomba tujadili bila mihemko ya kidini.......................

Young Malcom.

CC: MSEZA MKULU , Consigliere , Bukyanagandi , mchambawima1 , Dotworld
 
Exactly mkuu! ni mtumishi wa Mungu huyu bwana,amewachambua sana mkuu

Nathaniel amekulia kwenye familia ya Kiyahudi baadae ndiye akajiunga na kanisa la Orthodox.
Anawafahamu sana Wayahudi japo kuna vitu sikubaliani naye, lakini ni mtu mkweli sana na anampenda Mungu.
 
Ni kweli!
We ukiangalia waliopelekea mpaka wayahudi wakapata ile ardhi ni Marekani. Uchumi wa Marekani inaongozwa na wayahudi... Kwanini wasiwanyenyekee?
Wayahudi walibarikiwa akili saana ndo kinachowafanya Marekani wawang'ang'anie.
 
Kwani wewe KOLONI unaliewaje mkubwa?
Koloni ni Eneo au nchi iliyo chini ya utawala wa nchi nyingine(nchi mama) Iliyo mbali!!
Na Mara nyingi nchi hiyo huwa haina muwakilishi wake huru wa kimataifa( no independent international representative) na utawala wake wa juu huwa hushinikizwa au kuwekwa na Nchi mama!!
Sasa kwa kigezo hicho Marekani haiwez kuwa koloni LA Israel labda kinyume
Kwani Kijeshi marekani inanguvu Mara kadhaa kwa Israel na mambo mengi ya kisiasa kuhusu Israel imekua ikipata msaada kutoka kwa Marekani!!
Sabab moja ya kusema Marekan haikuchukua hatua dhidi ya uvamizi wa Israel ambao Israel iliufanya haitoshi kutoa conclusion rahis hivo!!
Ikumbukwe Israel na marekani wana uhusiano mzuri wa kidipromasia hivo Yawezekana ilijiridhisha na utetezi wa Israel
 
vitu gani mkuu,nipe faida

Kwamba Wayahudi ndiyo chanzo cha matatizo ya dunia na kumomonyoka kwa maadili ya Marekani.
Hili halijakaa sawa hata kidogo. Nakubali Wayahudi wana ushawishi mkubwa sana kwenye siasa ya Marekani na kweli wameharibu sana ile nchi; lakini ukweli utabaki kwamba Marekani imeanza kuharibika baada ya kupata uhuru.
Ubaguzi wa rangi, biashara ya utumwa, kupenda kumwaga damu za watu, ubaguzi wa kidini na kujali pesa kuliko utu vilikuwepo hata kabla ya Federal Reserve na Wall Street.
 
Back
Top Bottom