kuna sources zingine zinasema hata uingereza ana share yake marekani
Ukisoma Memoir za Marehemu Cecil Rhodes wakati ana miaka 23 alipendekeza Uingereza ivamie Marekani na kuifanya tena Koloni. Aliamini kwamba Waingereza (Anglo-Saxons) ndiyo jamii ya watu bora kabisa duniani. Hata akasema kwamba Uingereza ikitawala dunia kutakuwa na amani.
Lakini ukisoma Memoir zake za ukubwani utakuja kujua kwamba Rhodes aliachana na ndoto zake mfu baada ya kuona haitawezekana kirahisi. Alisema tu, njia bora ya kuwafanya Wamarekani wasiwe mbali na waingereza ni kujenga shirikisho la mataifa makubwa ambayo yatakuwa na mtizamo moja kwenye masuala ya kidunia.
Aliamua kuwapa ufadhili wanafunzi wengi wa Marekani hasa waliokuwa na uwezo mkubwa wa kuwa viongozi wa baadae.
Wengi walisoma chuo cha Oxford na Cambridge hivyo wakajengwa kwa mtizamo wa Uingereza. Ambao hata leo unaitwa ANGLO-AMERICA PERVIEW OF THE WORLD.
Hata alipokufa aliacha pesa (Trust Fund) kwa ajili ya kuendeleza huo mpango wake na ulichangia sana kuunganisha sera za Marekani na Uingereza.
Kabla ya vita ya Pili ya dunia The Rockefeller Foundation ilimuita mwana mkakati mashughuli duniani kutoka Uingereza anayeitwa Sir Halford Mckinder ili wapange mikakati ya siasa za Marekani baada ya vita ya dunia. Huyu jamaa ndiye aliyewafundisha siasa Henry Kissinger na Zbigniew Brzezinski.
Uingereza mpaka leo ana hisa Marekani kuanzia kwenye sera ya mambo ya nje na hata kiuchumi.
Suala la kujiuliza ni kwanini Waingereza na Wamarekani ndiyo walihangaika sana kuwasomesha Watanzania pindi baada ya kupata uhuru kupitia The Rockerfeller Foundation na Cecil Rhodes Trust Fund?
Wakina Mahiga, Chenge, Justinian Rweyemamu na n.k walisoma kwa kupitia hizo njia.
Yote hii ni kuweka hisa kwenye sera za mambo ya nje za Tanzania na nchi za Afrika.