Je, Makonda kavunja mwiko?

Je, Makonda kavunja mwiko?

Kuwa na adabu bibi unawezaje kusema makonda ni shujaa wakati uchunguz wa vyombo husika haujaleta majibu kuwa tuhuma yake ina ukweli au la na hata ikiwa itaonekana kuna ukweli basi wa kuprove kuwa sirro na kaganda wanatuhuma ni mahakama na si vinginevyo.Unampaje mtu credit wkt ishu haijawa proved au huo udas uliopewa unakufanya uendelee kujipendekeza ww.

Salaam.

Hapa hatuongeleai wala hatuchambui kama kuna ukweli au uongo kwa aliyosema Makonda, hapa tunaongelea ile kuweza kutamka tu aliyoyatamka, kwangu mimi ni ushujaa tosha.
 
Afrika kwa ujumla na hususan Tanzania (baada ya Uhuru) Polisi wamekuwa ni watu wa kuogopewa na jamii kama vile nyoka.

Nnakumbuka miaka ya mwanzoni mwa nchi yetu kupata Uhuru Polisi walikuwa ni watu wanaopendwa na jamii, enzi hizo ilikuwa utawakuta polisi wa Kizungu, Kihindi, Kiarabu na Kiafrika.

Kama watoto, kila mmoja wetu alikuwa anatamani siku moja awe askari Polisi. Kilichotupelekea kuwa hivyo ni jinsi enzi hizo polisi walivyokuwa na upole kwa watoto, nnakumbuka wakija mashuleni kutupa mafunzo ya kila aina na kutueleza vipi tuwe raia wema wenye kusaidia wengine. Nnakumbuka pia polisi wakituvusha barabara kwa upole na ingawa magari yalikuwa si mengi.

Nnachokikumbuka zaidi kwa polisi wa siku hizo ni tabasamu zao, awe wa kiume au wa kike (wa kike walikuwa wachache sana), ilikuwa siku zote nikiwaona polisi amma njiani amma wakija mashuleni walikuwa na tabasamu lisilokwisha na wenye nyuso za furaha kiasi cha kukufanya uliye karibu nao uwe na amani.

Hayo yaliisha mara tu baada ya kutangazwa azimio la Arusha.

Baada ya hapo mpaka hii leo, Polisi wamekuwa ni watu wasiocheka na watu, polisi imekuwa ndiyo tishio kwa watoto, mtoto wako akikosa ukimtajia polisi basi anaingiwa na uoga.

Jee, tumejiuliza kwanini? Mimi nna-majibu mengi sana kuhusu hilo lakini nnawaachia wachangia mada nanyi mjinafasi na kutoa dukuduku lenu kwa mtazamo wenu.

Paul Makonda, ameweza kuwasema polisi hadharani, tena kinaga ubaga. Mwiko ambao hata wakubwa zaidi ya Makonda kwenye uongozi wameshindwa kuuvunja kwa hapa kwetu Tanzania na nchi nyingi za Kiafrika kwa ujumla. Jee, kwanini?

Binafsi nnaona kitendo cha Makonda ni cha kishujaa sana. Wewe jee?

Nnaomba tuchangie hii mada huku tukielekeza maoni yetu kwa viongozi wa nchi pamoja na viongozi wa majeshi ya polisi kwa nia ya kuitaka polisi iwe rafiki zaidi wa wananchi na iwe ni kwa ajili ya wananchi na si kwa ajili ya viongozi wa nchi au watawala wa nchi pekee.
Yani Makonda kafanya mageuzi makubwa sana tena mno...angewasema hivi hivi bila kuwa na ushahidi kuwa yeye alifuatwa na kuhogwa ningesema mnafiki na mzandiki.Lakini kasema wazi wazi kuwa yeye alifuatwa na kumegewa taarifa na ka kikundi ka watu kumi wampe mgao wa milioni 50 kwa mwezi ili akae kimya swala la shisha yeye akakataa..

Swali la msingi ambalo ndio kiini cha Makonda ..ni kuwa kama waliweza kwenda kwake yeye Mkubwa watashindwa nii kwenda kwa wadogo zke yeye ambao ndio wenye jukumu la kuwakamata wao waliokwenda kwake..[Logic] Na walikwenda kwake kama kutanua wigo wa kunyamazisha.Kama yeye alifikiwa na amesema hadharani kwanini wao washindwe kusema hadharani kuwa HATUKUFIKIWA? na kama walifikiwa wasema nao WALIFIKIWA na MGAO waliukataaa...na ndio maana zoezi la SHISHA lilifanikiwa na hivyo swala la SHISHA kuwa ipo mtaani ni uongo...hivyo Mh Waziri Mkuu anapombana Mkuu wa MKoa taarifa alizonazo si kweli na taarifa anazozitoa Makonda hazina uhalisia hivyo katika kuwajibika kwa Jamhuri wao taarifa zao ndizo sahihi.

Rais Magufuli na Mh Waziri Mkuu wana kazi...nzito lakini nafurahi wanajua nii wanachotaka kutupatia na wasiogope kuwaludisha Watuumishi wa Umma Mitaani kwa kuwanyima KAZI ikiwa na kufungwa kuna husu wafungwe sie Watanzania tutajifunza kuwa Tunataka Taifa makini..na utii wa sheria bila kujali nani ana nafasi gani...awe tajiri ama masikini.
 
Mkuu mbona hizo ni tuhuma tu? Kuna ushahidi wowote mpaka sasa kwamba Siro kapokea rushwa?
Kweli ni tuhuma ila tuache kusema Makonda anatafuta sifa, kana kwamba huyo Siro ni Mungu hawezi kuchukua rushwa! Nchi hii kuna watu na heshima zao wameliabisha taifa!
 
Hivi CHADEMA ni nani?kwahiyo nami kwa uchangiaji wangu umeshaniita CDM?Jukwaa hili kuna kipengele cha kuweka status yako kichama?Unamjuaje mtu kama ni CDM?Amekupa kadi yake ya uanachama?Unajadili kitoto sana,toa hoja sio kupiga mipasho tu.Hii ni JF sio facebook
Sijui tunabishana nini? Au unataka nilete coment zako za humu kuonesha uchadema wako?
 
Hekima au Busara ndiyo nadhani vimekosekana!

Kumtuhumu mtu hadharani bila ya unachokituhumu kuthibitishwa na taasisi husika ni tatizo, vipi ikija kuthibitika siyo kweli kwa tuhuma za RC dhidi ya Siro?

Kwakuwa amemtuhumu Siro hadharani, Siro ange jihudhuru ama angeondolewa nafasi yake ili kupisha uchunguzi.

Ushujaa wa RC ungeanza na yeye kwataja kwa majina "hadaharani" wale woote waliojaribu kumuhonga na kuweka bayana tuhuma zake kwa Siro na jeshi la polisi!

RC kwa nafasi yake, ange[peleka tuhuma zake pahala husika na zikisibitika haikuwa mbaya kuzisema hadharani, lakini kwa sasa wakazi woote wa Dar na Tz kwa ujumla tunaaminishwa kutokuwa na imani na jeshi la polisi hadi pale itakapo thibitika vinginevyo.
 
Afrika kwa ujumla na hususan Tanzania (baada ya Uhuru) Polisi wamekuwa ni watu wa kuogopewa na jamii kama vile nyoka.

Nnakumbuka miaka ya mwanzoni mwa nchi yetu kupata Uhuru Polisi walikuwa ni watu wanaopendwa na jamii, enzi hizo ilikuwa utawakuta polisi wa Kizungu, Kihindi, Kiarabu na Kiafrika.

Kama watoto, kila mmoja wetu alikuwa anatamani siku moja awe askari Polisi. Kilichotupelekea kuwa hivyo ni jinsi enzi hizo polisi walivyokuwa na upole kwa watoto, nnakumbuka wakija mashuleni kutupa mafunzo ya kila aina na kutueleza vipi tuwe raia wema wenye kusaidia wengine. Nnakumbuka pia polisi wakituvusha barabara kwa upole na ingawa magari yalikuwa si mengi.

Nnachokikumbuka zaidi kwa polisi wa siku hizo ni tabasamu zao, awe wa kiume au wa kike (wa kike walikuwa wachache sana), ilikuwa siku zote nikiwaona polisi amma njiani amma wakija mashuleni walikuwa na tabasamu lisilokwisha na wenye nyuso za furaha kiasi cha kukufanya uliye karibu nao uwe na amani.

Hayo yaliisha mara tu baada ya kutangazwa azimio la Arusha.

Baada ya hapo mpaka hii leo, Polisi wamekuwa ni watu wasiocheka na watu, polisi imekuwa ndiyo tishio kwa watoto, mtoto wako akikosa ukimtajia polisi basi anaingiwa na uoga.

Jee, tumejiuliza kwanini? Mimi nna-majibu mengi sana kuhusu hilo lakini nnawaachia wachangia mada nanyi mjinafasi na kutoa dukuduku lenu kwa mtazamo wenu.

Paul Makonda, ameweza kuwasema polisi hadharani, tena kinaga ubaga. Mwiko ambao hata wakubwa zaidi ya Makonda kwenye uongozi wameshindwa kuuvunja kwa hapa kwetu Tanzania na nchi nyingi za Kiafrika kwa ujumla. Jee, kwanini?

Binafsi nnaona kitendo cha Makonda ni cha kishujaa sana. Wewe jee?

Nnaomba tuchangie hii mada huku tukielekeza maoni yetu kwa viongozi wa nchi pamoja na viongozi wa majeshi ya polisi kwa nia ya kuitaka polisi iwe rafiki zaidi wa wananchi na iwe ni kwa ajili ya wananchi na si kwa ajili ya viongozi wa nchi au watawala wa nchi pekee.

Binafsi ningemwona shujaa kama angewataja hadharani hao wafanya biashara wa @5M, na atake mienendo yao ichunguzwe ili kubaini uhusika wao kuwatia polisi kigugumizi! Rushwa ni kosa la jinai kwa anayetoa na kwa anayepokea, ila yeye alielekea kuwarushia polisi tuhuma kisiasa ili yeye "apone" na sio kutaka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya jinai husika!
 
Ni kitendo cha kishujaa sana. Jwtz nao wako kikaangoni, askari wake wengi wanajifanya wababe kwa raia na barabarani, ukiwahoji wanaweza kukuchangia kukupiga, wanajenga ukuta na raia! Nidhamu ya uoga dhidi yao ma wananchi ndo kilichopo katikati!
Ni kama ugomvi wa wachawi. Hata wakigombana bado kila mmoja akikupatia anakudhuru vilevile. Hata hivyo RC kusubiri hadhara/matukio ni tabia/utamaduni mbaya, sio ushujaa.
 
Mbowe ana nguvu kuliko rais na dola?!!?
Hongera Mbowe.
Ndioaana JPM kaamua maandamano na mikitano "ikafanywe" Hai, tunatakiwa tufanye kazi sio kuamdamana nchi nzima, nafikiri umenielewa!
 
Huyu bwana mdogo anafanya mambo utadhani hakuna kesho.
 
Ila Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, mi itendeke namna hapo, sio bure!!!
 
Moderator kwanini umeondoa "e" moja kwenye neno Jee, nililoandika kwenye kichwa cha habari?

Tafadhali irudishe.

Hiyo "Je," yako uliyoiweka ni kosa la kimatamshi.

cc
Duu!! Wewe Bi. Mkubwa kweli kiboko. Inaonekana moderators bado hawajakufahamu vizuri. Wape darsa ili wasiokufahamu waweze kukufahamu vizuri.
 
Binafsi ningemwona shujaa kama angewataja hadharani hao wafanya biashara wa @5M, na atake mienendo yao ichunguzwe ili kubaini uhusika wao kuwatia polisi kigugumizi! Rushwa ni kosa la jinai kwa anayetoa na kwa anayepokea, ila yeye alielekea kuwarushia polisi tuhuma kisiasa ili yeye "apone" na sio kutaka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya jinai husika!
Kuwataka haitoshi. Angewakamata ingeeleweka. Tunajuaje kama si yeye aliyewaomba hao watu kila mmoja wao awe anampatia sh 5m kila mwezi. Iliposhindikana ndipo anatoka hadharani kulalamika. Makonda siyo malaika. Anashiba na kupata njaa.
 
Mimi naona kama ni utovu wa nidhamu, kimaadili ya kazi hakutakiwa kujimbizana na wakubwa zake hadharani.

PM na Sirro wana hadhi zao angewafuata ofisini au angesubiri vikao husika.

Sitetei upande kwa vile binafsi sina imani na jeshi la polisi wala Makonda mwenyewe kutokana na tabia zake.

Ila nachoweza kusema tabia hii ikiachwa isiendelee kuna siku atamtuhumu hadharani Mkuu wa Majeshi kuwa anashirikiana na nchi jirani kuhujumu nchi na kuleta taharuki.
Huo ndio mwanzo wa mwisho wa Mh Kondakta.
 
Afrika kwa ujumla na hususan Tanzania (baada ya Uhuru) Polisi wamekuwa ni watu wa kuogopewa na jamii kama vile nyoka.

Nnakumbuka miaka ya mwanzoni mwa nchi yetu kupata Uhuru Polisi walikuwa ni watu wanaopendwa na jamii, enzi hizo ilikuwa utawakuta polisi wa Kizungu, Kihindi, Kiarabu na Kiafrika.

Kama watoto, kila mmoja wetu alikuwa anatamani siku moja awe askari Polisi. Kilichotupelekea kuwa hivyo ni jinsi enzi hizo polisi walivyokuwa na upole kwa watoto, nnakumbuka wakija mashuleni kutupa mafunzo ya kila aina na kutueleza vipi tuwe raia wema wenye kusaidia wengine. Nnakumbuka pia polisi wakituvusha barabara kwa upole na ingawa magari yalikuwa si mengi.

Nnachokikumbuka zaidi kwa polisi wa siku hizo ni tabasamu zao, awe wa kiume au wa kike (wa kike walikuwa wachache sana), ilikuwa siku zote nikiwaona polisi amma njiani amma wakija mashuleni walikuwa na tabasamu lisilokwisha na wenye nyuso za furaha kiasi cha kukufanya uliye karibu nao uwe na amani.

Hayo yaliisha mara tu baada ya kutangazwa azimio la Arusha.

Baada ya hapo mpaka hii leo, Polisi wamekuwa ni watu wasiocheka na watu, polisi imekuwa ndiyo tishio kwa watoto, mtoto wako akikosa ukimtajia polisi basi anaingiwa na uoga.

Jee, tumejiuliza kwanini? Mimi nna-majibu mengi sana kuhusu hilo lakini nnawaachia wachangia mada nanyi mjinafasi na kutoa dukuduku lenu kwa mtazamo wenu.

Paul Makonda, ameweza kuwasema polisi hadharani, tena kinaga ubaga. Mwiko ambao hata wakubwa zaidi ya Makonda kwenye uongozi wameshindwa kuuvunja kwa hapa kwetu Tanzania na nchi nyingi za Kiafrika kwa ujumla. Jee, kwanini?

Binafsi nnaona kitendo cha Makonda ni cha kishujaa sana. Wewe jee?

Nnaomba tuchangie hii mada huku tukielekeza maoni yetu kwa viongozi wa nchi pamoja na viongozi wa majeshi ya polisi kwa nia ya kuitaka polisi iwe rafiki zaidi wa wananchi na iwe ni kwa ajili ya wananchi na si kwa ajili ya viongozi wa nchi au watawala wa nchi pekee.

binafsi siungi mkono hoja yako kabisa.

itakuwa ni makosa makubwa sana kama tunaweza kuwa na viongozi ambao wanashindwa kutoa maelekezo kwa watu walioko chini yoa na wakawasimamia kutekekeleza maelekezo hayo na badala yake kiongozi anaibuka na hoja ambayo ambayo kaifikiria yeye peke yake na anatumia mikutano kutangaza hoja na kujaribu kutafuta mbinu zozote kuwashawishi watu walioko juu kushinikiza wazo lake au kuonyesha kukwama kwa wazo ni makosa ya wengine.

sijasema yeye aliyetoa tuhuma alitumia njia hii, ila najiuliza alikuwa na uhakika kuwa aliyemtuhumu kafanya kosa hilo au yeye katafuta hoja ya kisiasa kwenye jukwaa.

hatuwezi kupiga hatua hatua kwa njia hii na hii ni njia ambayo kiongozi anawagawa wafuasi walioko chini yake.

mimi naamini kama kiongozi ni kosa kubwa kusimama kusimama kwenye jukwaa kumtuhumu mtu aliyeko chini yako au aliyeko juu yako. kama kunajambo huridhiki nalo lichukulie hatua katika taratibu za serikali.

iawapo wananchi wameleta malalamiko hayo ndiyo unaweza kuwaahidikuyashughulikia na ukibaini uzembe ndio unaweza kusimama kwenye majukwaa kuwaeleza wananchi hatua mlizochukua.

kwangu mimi naona hili ni kosa kubwa na ambalo linatakiwa kuwafundisha wote wanaolifuatilia kuwa.
1. kama kiongozi unatakiwa kukaa na watendaji wako mkajadili hoja kwa kuangalia tatizo na mtalitatuaje.
2. mkishajadili nakukubaliana ndio kongozi anaweza kusimama kwenyejukwaa kutoa sumary ya kile walichokubaliana kama kuoa maagizo. labda liwetukio la emergency lilitukia ghafla na linahitaji maamuzi.
3. kongzi kazi yake sikuongea kwenye majukwaa tu. anaka na watu wake wanapanga, anasimamai watu walioko chini yake kuhakikisha wanatekeleza na anatumia majukwaa kuhamasisha utekelezaji.
4. Timu moja moja hamuwezi kulaumiana uwanjani mkapata mafanikio. ukiona timu wanaanza kulaumiana uwanjani basi mara zote huwa wanatoka kwenye mchezo na ni mwanzo wa kufungwa. ukiwa uwanjani kazi yako ni kucheza yanatukia yakiwa chni yako chukua hatua na yaliyoko juu yako yaripoti sehemu husika kwa taratibu za kiofisi. yupo kocha pembeni anayetazama nani kafanya makosa yeye ndiye atajua nani wa kumuwajibisha na nani wa kumuacha.
 
Back
Top Bottom