Je, Lissu anajijenga ili kugombea Urais 2020?

Je, Lissu anajijenga ili kugombea Urais 2020?

Yeye ni mbunge wa Kule Singida...tupatie mfano wa jinsi alivyobadili maisha ya wapiga kura wake kiuchumi, kielimu, na kidemokrasia hadi atiliwe mfano wa kuigwa....kubwabwaja, uanaharakati na kukosoa kila jambo si kigezo cha uongozi bora!
Yaani wewe Unamzungumzia Lissu kwa habari ya jimbo? We vipi wewe? Nenda Ikungi kajionee usisimuliwe. Hii ni namba nyingine ijadiliwe kwa level ya kitaifa na sio jimbo. Pole sana mkuu.
 
Lisu yuko vizuri ila bado mihemko inamsumbua ,akiweza kudeal na mihemko yake basi ni hazina kubwa ,nakumbuka wakati wa uchaguzi Zanzibar ulipofutwa ,yeye alisema haya ni maasi na hakuna namna nyingine zaidi ya kuingia barabarani ,ni kweli kilichofanyika Zanzibar hakikuwa sawa ila pia ilihitajika busara kubwa sana badala ya mihemko ,
Kufahamu ukweli wa mambo ni kuwa na akili, lakini kufahamu ni wakati upi uyazungumze hayo mambo ni busara.
Hapa kaka Lissu ndipo anapwaya balaa.
Anaweza kuingiza nchi kwenye balaa kama akija kuwa kiongozi mkubwa kama raisi, waziri mkuu au hata mwanasheria mkuu.

Ila uwezo wa kichwani na uzalendo, Tundu ni balaa.I got give him that.
 
Kama uongozi ulioko madarakani hivi sasa unaweza kuliongoza taifa hili, Pamoja na tofauti kubwa iliyopo juu ya uzingatiaji sheria na katiba ya nchi na bado kuna wananchi wanasifia basi kamanda LISSU ni hazina pekee ya taifa hili ambayo haina wa kufanana nae.

Ni msomi, jasiri, ana akili, amajiini, mi mkweli,hadanganyiki, ni mtendaji safi, ni mwanasiasa safi. Kwa hakika huyu mtu sina kiongozi wa kumfananisha xndani ya taifa hili. Namuombea uzima tele Mungu aendelee kumwongoza vema katika harakati zake za kutetea haki za wanyonge.

Kama Rais tuliyenaye kwa sasa atafanikiwa kulifikisha taifa kama alivyoahidi, akatekeleza ahadi zake kama alivyoahidi basi kiumbe pekee anayefanana naye kwa misimamo na kiutendaji japo kuna tofauti ya intelligence ni Tundu Lissu Pekee.

Kwa wasiofahamu ni kwamba Tundu LISSU ni mbunge pekee Tanzania ambaye wakati wa uchaguzi wa October 2015 CCM walipeleka nguvu kubwa sana kwakwe kuliko hata wengine ya mgombea Urais, Lakini poja na hujuma zote, pamoja na aliyekua akipambana nae ni ndugu yake Tundu Lissu alichomoa.

Mwaka 2010 wakati wa uchaguzi aliyekua mgombea Urais kupitia CCM wakati huo Rais mustaafu JM. Kikwete aliuambia umma wwatanzania kua "Ni bora Dr Slaa kushinda kiti cha Urais kuliko Tundu Lissu kushinda ubunge".Haya sio maneno yangu,yalikua maneno ya Kikwete! Kikwete alikua kawaida,hakua akitania bali alinena ukweli wa moyo wake,alisema alichokifahamu na alichokiona kwa Tundu LISSU.Nadhani angekua ni mwanaCCM wakati huo sijui JK angempa cheo gani ndani ya serikali yake.

Ukubali ukatae Tundu Lissu baada ya Magufuli ndiye kichwa pekee cha kuliongoza taifa hili, kama wananchi wataipenda aina ya utawala wa Rais Magufuli pasina shaka kabisa kwa umahiri na umakini wa Lissu Chadema waanze kukiweka chama kimaandalizi katika mkao wa kuliongoza taifa hili.Sioni kabisa mtu wa aina LISSU katika taifa hili.

Jamani mimi hua najiuliza sana, hivi ni mpaka sasa ni nani wa kusimama na Mh Tundu Lissu kwenye kitu cha Urais akapambana nae akamshinda? Tuwe waungwa kuusema ukweli ni nani anaweza kushindana na Lisuu kwa nafasi yeyote ile?

Tupate katiba mpya na bora, tupate tume huru ya uchaguzi na mwisho Chadema watazame wakati tulionao na mahitaji ya sasa,zaidi ya hapo sina la kuongezea.Nimalizie kwa kumtakia kaka yangu Tundu Lissu kila lakheri na Mungu amuongoze na awe salama ndani ya mikono ya polisi kwa sasa, aendeleze mapambano tuko nyuma yake na pia figisu figisu anazozipata atambue kua ni mapito haya.

Tufikie Maridhiano kama Taifa Mheshimiwa JPM apeleke mswada bungeni ili Bunge lilidhie TAL awe Waziri Mkuu!; Hapo tz itakuwa TZ....
 
Kufahamu ukweli wa mambo ni kuwa na akili, lakini kufahamu ni wakati upi uyazungumze hayo mambo ni busara.
Hapa kaka Lissu ndipo anapwaya balaa.
Anaweza kuingiza nchi kwenye balaa kama akija kuwa kiongozi mkubwa kama raisi, waziri mkuu au hata mwanasheria mkuu.

Ila uwezo wa kichwani na uzalendo, Tundu ni balaa.I got give him that.
Lisuu ana akili sana! angekua hivyo hayo tungeyaona jimboni kwake.Hebu jaribu kumtofautisha Lissu na kina kamanda Lemma.
 
Ni bora wewe unasema ukweli.
lissu ana talanta ya ukombozi kwa taifa hili, em tuache kidogo masuala ya ushabiki wa vyama na tusimamie ukweli juu ya huyu muheshimiwa,..yeye ndie alieibua mambo mbalimbali , tukumbuke issue ya tegeta escrow jamaa alivyoibua mazito,, mmesahau na mikataba fake anayoweka hadharani? kwa kweli hata bungeni lissu asipokuepo bunge huwa linapwaya na kukosa mvuto....napenda sana ukweli wa lissu kikweli hata sisi CCM baadhi yetu tunatambua lissu ni msema kweli
 
Kufahamu ukweli wa mambo ni kuwa na akili, lakini kufahamu ni wakati upi uyazungumze hayo mambo ni busara.
Hapa kaka Lissu ndipo anapwaya balaa.
Anaweza kuingiza nchi kwenye balaa kama akija kuwa kiongozi mkubwa kama raisi, waziri mkuu au hata mwanasheria mkuu.

Ila uwezo wa kichwani na uzalendo, Tundu ni balaa.I got give him that.
Nakubaliana na wewe kabisa bro kinacho msumbua Lisu ni nini cha kusema na wakati upi pia wa kusema ,ambayo ndio busara yenyewe ,ni hazina kubwa sana Lisu akiweza kurekebisha hilo ,
 
Manyumbu bana. Mkikutana wenyewe mna hoja za kipuuzi puuzi mno. Hivi mgonjwa wa mirembe atapewa nchi na nani aongoze. Labda akaongoze mifugo huko
 
namkubali sana !!
1-hayumbi kwenye hoja !
2-anatumia akili vizuri !
3-uwezo mkubwa wa kujenga hoja
4-haogopi wajingawajinga wenye IQ ndogo
5-hanunuliki
6-mwenye msimamo
7-ni mwenye maono
8-kaisaidia sana CCM kuiamsha kwamba imejaa mafisadi,sasa wanatumbuana
9-habahatishi
 
Nakubaliana na wewe kabisa bro kinacho msumbua Lisu ni nini cha kusema na wakati upi pia wa kusema ,ambayo ndio busara yenyewe ,ni hazina kubwa sana Lisu akiweza kurekebisha hilo ,
lissu ni taahira. Acha kuremba remba
 
namkubali sana !!
1-hayumbi kwenye hoja !
2-anatumia akili vizuri !
3-uwezo mkubwa wa kujenga hoja
4-haogopi wajingawajinga wenye IQ ndogo
5-hanunuliki
6-mwenye msimamo
7-ni mwenye maono
8-kaisaidia sana CCM kuiamsha kwamba imejaa mafisadi,sasa wanatumbuana
9-habahatishi
njaa ndio inayokutuma kuandika huu utumbo ee
 
Lissu nilishamsifia ingawa Mimi sipendi tena CHADEMA kwa ujio wa Lowassa but Lissu ni mwanasiasa Mwenye high continues capacity growing politically graph!! Uwa namwelewa sana huyu jamaa
 
Back
Top Bottom