Lissu ni kama martin Luther wa marekani
Hawafanani hata kidogo.
King alikuwa ni pastor, civil right leader na mwanaharakati kupinga ubaguzi wa mtu mweusi na vita zinazoanzishwa na USA duniani kote kwa interest zao huku zikisababisha maafa makubwa na vifo kwa wasio na hatia.
King hakuwa mwanasiasa, alikuwa huru daima kipaji na uwezo wake mkubwa katika kutoa speech(ukisikiliza speech zake ni kama mwalimu anayefundisha) misimamo yake thabiti isiyoyumba katika kutekeleza alichokuwa akikipigania vilifanya awe kipenzi cha wengi wamarekani na wasio wamarekani kuanzia watoto, vijana, wote wazee weusi na weupe.
Hatimaye aliuawa kwa kupigwa risasi lakini falsafa na matendo yake yanaendelea kuishi hata leo.
Tundu Lissu ni mwanasiasa mwenye uwezo mkubwa kwenye ujenzi wa hoja huku akitumia taaluma yake ya sheria kama msingi wa hoja zake na niwe tu muwazi kwa hili anaonekana kufanya vizuri na hoja zake kuwa na nguvu sana miongoni mwa wanaomsikiliza.
Lissu naye ana uwezo mkubwa kwenye kuzungumza na kushawishi kwa hoja zake, ana wengi wanaompenda lakini utofauti na King ni kuwa Lissu anaupande sababu ni mwanasiasa na hivyo yuko upande fulani hapa pia niwe muwazi na misimamo yake huwa inayumba hana misimamo thabiti kama Martin Luther King.
Uwezo wa King kwenye kutoa speech haufanani na ule wa Lissu huyo King alikuwa na uwezo mkubwa sana sikiliza speech zake utakubaliana na mimi kama hukuwahi kusiikilza.
Hayo niloandika yanaonesha ni kwa kiasi utakuwa unakosea kumfananisha civil right leader Martin Luther King JR. na Tundu Lissu(Mb).