Je, Lissu anajijenga ili kugombea Urais 2020?

Je, Lissu anajijenga ili kugombea Urais 2020?

Kuwa na akili hakumfanyi mtu kuwa kiongozi mzuri,
La sivyo basi wakina Newton na Einstein wangekuwa watawala wazuri.
Kujua sheria siyo kuwajua Watanzania lazima tuweze tofautisha hapo.
Lissu apunguze mihemko na afanye siasa kama mwenzake Zitto Kabwe mbona atafika mbali tu.
Sio kigezo kimoja pekee soma na mengine usihemke uone kama sio Rais wako ajaye.
 
Hana uwezo wa kuongoza Tanzania,kujua sheria sio kigezo cha kuongoza nchi.Usituaminishe kwa hilo.
Kama kaweza magupome atashindwa lissu? tena lissu ataweza mara 1000000 ya magu
 
Mnazidi Kumuogopa Lissu. Kwa uwezo na akili na ulegendari Lissu anafaa kuwa hata Rais wa Mataifa makubwa kama Amerka, Uingereza, Ufaransa, Japan, Uchina na kwingineko
 
Hii ni kama strategy ya ukawa kujenga mgombea wake kwa mwaka 2020, baada ya kuone appointment ya Katibu mkuu kukosa mwito ndani na nje ya muunganiko huo.

Kauli na matendo ya Lisu yanaonyesha muelekeo wa kujijenga kisiasa kwa lengo la kugombea nafasi hiyo.

Ikumbukwe kwamba bado kuna pingamizi za ndani kwa ndani ukawa kama Lowasa atasimama kwa tiketi hiyo ifikapo uchaguzi mkuu, hii ni kutokana na yeye kuzidi kupungua ushawisi ukilinganisha na kipindi cha uchaguzi wa 2020.

Saikolojia ya mwanadamu unaonyesha kwamba mtu anayekipinga kitu flani sana either anakipenda sana au anahisi kama aliyenacho hastahili kuwa nacho isipokua yeye.

Saikolojia hii ndogo inapelekea wengi wetu kuanza kunyanyua kope za macho na kujiuliza nia halisi ya Lisu baada ya kuona na kusikia haya aliyoyafanya hivi karibuni.

Je, huu ndio mwanzo wa safari ya kugombea nafasi hiyo 2020, na mwendelezo wa matukio toka kwa mwanasiasa huyo?
JK mwenyewe alisema ni bora Tundu lissu kuwa Rais kuliko kuwa mbunge bungeni...muda huo JPM alikuwa waziri wa ujenzi...TAFAKARI
 
Natafuta maoni ya mnyika kuhusu magufuli msaada tafadhali
 
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, ni kauli ambayo rais Magufuli hupenda kuitamka majukwaani. Nami narudia usemi huu kuwa msema kweli ni mpenzi wa Mungu, ingawa Mungu pekee ndiye anayejua ni kwa kiasi gani tunachosema kinashabihiana na tunayotenda kumpendeza Mungu. Nchi yetu ina wananchi wenye vipaji tele. Mh Tundu Lissu anakipaji cha pekee kinachoweza kusaidia nchi yetu kupaa kiuchumi kwa kuwa na mikataba mizuri kati yetu kama nchi na wadau wengine katika kuiletea nchi yetu maendeleo.

Ni juu ya rais Magufuli kuvitumia vipawa vya mwananchi huu wa Tanzania Tundu Lissu, badala ya kupoteza fursa za kutumia hazina hii. Ni vema serikali yote ya CCM ielewe kuwa siasa si uadai. Wote, wanasiasa na wasiowanasiasa, wana-CCM na wale wa vyama mbadala, wote ni wananchi hamna haja ya kugombania fito wakati tunajenga nyumba moja.
 
Kwani yeye haoni wivu kuzidiwa akili nA lissu?
 
Back
Top Bottom