Je, Lissu anajijenga ili kugombea Urais 2020?

Je, Lissu anajijenga ili kugombea Urais 2020?

Hahahaaaa! Acha kuongea vice versa.kwani watu wa hivyo ni wa kutafuta?
kweli ndani ya CHADEMA ni yeye tu wengine wahuni na DJ na wasaniii, Lissu ndiye afadhari kidogo"mwenye chongo ni mfalume kwa vipofu''
 
Lisu yuko vizuri ila bado mihemko inamsumbua ,akiweza kudeal na mihemko yake basi ni hazina kubwa ,nakumbuka wakati wa uchaguzi Zanzibar ulipofutwa ,yeye alisema haya ni maasi na hakuna namna nyingine zaidi ya kuingia barabarani ,ni kweli kilichofanyika Zanzibar hakikuwa sawa ila pia ilihitajika busara kubwa sana badala ya mihemko ,
 
chadema mgombea wetu 2020 ni lowasa hao wengne ni wenu. #CDM 2020 twende na lowaxa#
 
Tundu Lisu kiherehere sana ,acha aisome Namba.

Kama Mwenye chama Mzee Mtei amesema Magufuli ni kama Nyerere.
Wewe kibavicha unapinga who are you??

Wapigwe tu, maana hamna namna
Mkuu,kuna sehemu nimezifuma procedures za kumkata ng'ombe mkia na wala asihisi maumivu yoyote..nikusaidie??
 
Kwa mtazamo wangu Lissu ajafikia uwezo wa kuliongoza taifa hili, kigezo cha sheria sio sifa pekee, kumbukeni alishawah kuisaliti kauli yake juu ya lossawa.
 
Kwa mtazamo wangu Lissu ajafikia uwezo wa kuliongoza taifa hili, kigezo cha sheria sio sifa pekee, kumbukeni alishawah kuisaliti kauli yake juu ya lossawa.
Mkuu usichekeshe watu humu bure. Soma uzi mpaka mwisho uelewe kwanza.
 
Ahamie CCM labda atakuwa Rais
Ungesoma Uzi uelewe. Itafika mahali mtu anakubalika mpaka wezi wa kura wataogopa, umma utadai mshindi wao,taifa zima litamjua mshindi na huko ndiko tunakoelekea.
 
Kama uongozi ulioko madarakani hivi sasa unaweza kuliongoza taifa hili, Pamoja na tofauti kubwa iliyopo juu ya uzingatiaji sheria na katiba ya nchi na bado kuna wananchi wanasifia basi kamanda LISSU ni hazina pekee ya taifa hili ambayo haina wa kufanana nae.

Ni msomi, jasiri, ana akili, amajiini, mi mkweli,hadanganyiki, ni mtendaji safi, ni mwanasiasa safi. Kwa hakika huyu mtu sina kiongozi wa kumfananisha xndani ya taifa hili. Namuombea uzima tele Mungu aendelee kumwongoza vema katika harakati zake za kutetea haki za wanyonge.

Kama Rais tuliyenaye kwa sasa atafanikiwa kulifikisha taifa kama alivyoahidi, akatekeleza ahadi zake kama alivyoahidi basi kiumbe pekee anayefanana naye kwa misimamo na kiutendaji japo kuna tofauti ya intelligence ni Tundu Lissu Pekee.

Kwa wasiofahamu ni kwamba Tundu LISSU ni mbunge pekee Tanzania ambaye wakati wa uchaguzi wa October 2015 CCM walipeleka nguvu kubwa sana kwakwe kuliko hata wengine ya mgombea Urais, Lakini poja na hujuma zote, pamoja na aliyekua akipambana nae ni ndugu yake Tundu Lissu alichomoa.

Mwaka 2010 wakati wa uchaguzi aliyekua mgombea Urais kupitia CCM wakati huo Rais mustaafu JM. Kikwete aliuambia umma wwatanzania kua "Ni bora Dr Slaa kushinda kiti cha Urais kuliko Tundu Lissu kushinda ubunge".Haya sio maneno yangu,yalikua maneno ya Kikwete! Kikwete alikua kawaida,hakua akitania bali alinena ukweli wa moyo wake,alisema alichokifahamu na alichokiona kwa Tundu LISSU.Nadhani angekua ni mwanaCCM wakati huo sijui JK angempa cheo gani ndani ya serikali yake.

Ukubali ukatae Tundu Lissu baada ya Magufuli ndiye kichwa pekee cha kuliongoza taifa hili, kama wananchi wataipenda aina ya utawala wa Rais Magufuli pasina shaka kabisa kwa umahiri na umakini wa Lissu Chadema waanze kukiweka chama kimaandalizi katika mkao wa kuliongoza taifa hili.Sioni kabisa mtu wa aina LISSU katika taifa hili.

Jamani mimi hua najiuliza sana, hivi ni mpaka sasa ni nani wa kusimama na Mh Tundu Lissu kwenye kitu cha Urais akapambana nae akamshinda? Tuwe waungwa kuusema ukweli ni nani anaweza kushindana na Lisuu kwa nafasi yeyote ile?

Tupate katiba mpya na bora, tupate tume huru ya uchaguzi na mwisho Chadema watazame wakati tulionao na mahitaji ya sasa,zaidi ya hapo sina la kuongezea.Nimalizie kwa kumtakia kaka yangu Tundu Lissu kila lakheri na Mungu amuongoze na awe salama ndani ya mikono ya polisi kwa sasa, aendeleze mapambano tuko nyuma yake na pia figisu figisu anazozipata atambue kua ni mapito haya.

Yeye ni mbunge wa Kule Singida...tupatie mfano wa jinsi alivyobadili maisha ya wapiga kura wake kiuchumi, kielimu, na kidemokrasia hadi atiliwe mfano wa kuigwa....kubwabwaja, uanaharakati na kukosoa kila jambo si kigezo cha uongozi bora!
 
Taifa hili Lissu hawezi kuliongoza kama vile ambavyo EL hawezi kuliongoza na katu hatokuwa kiongozi wa taifa hili. Kwenye familia zao sawa , ila sio Taifa hili.
Sawa Mkuu,lakini effects ya shughuli zao ni dhahiri ilishavuka level ya familia
 
Yeye ni mbunge wa Kule Singida...tupatie mfano wa jinsi alivyobadili maisha ya wapiga kura wake kiuchumi, kielimu, na kidemokrasia hadi atiliwe mfano wa kuigwa....kubwabwaja, uanaharakati na kukosoa kila jambo si kigezo cha uongozi bora!
kwani nanihii amefanya nini chato?
 
Back
Top Bottom