Je, Lissu anajijenga ili kugombea Urais 2020?

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,982
45,898
Hii ni kama strategy ya UKAWA kujenga mgombea wake kwa mwaka 2020, baada ya kuone appointment ya Katibu mkuu kukosa mwito ndani na nje ya muunganiko huo.

Kauli na matendo ya Lissu yanaonyesha muelekeo wa kujijenga kisiasa kwa lengo la kugombea nafasi hiyo.

Ikumbukwe kwamba bado kuna pingamizi za ndani kwa ndani UKAWA kama Lowassa atasimama kwa tiketi hiyo ifikapo uchaguzi mkuu, hii ni kutokana na yeye kuzidi kupungua ushawishi ukilinganisha na kipindi cha uchaguzi wa 2020.

Saikolojia ya mwanadamu unaonyesha kwamba mtu anayekipinga kitu flani sana either anakipenda sana au anahisi kama aliyenacho hastahili kuwa nacho isipokua yeye.

Saikolojia hii ndogo inapelekea wengi wetu kuanza kunyanyua kope za macho na kujiuliza nia halisi ya Lissu baada ya kuona na kusikia haya aliyoyafanya hivi karibuni.

Je, huu ndio mwanzo wa safari ya kugombea nafasi hiyo 2020, na mwendelezo wa matukio toka kwa mwanasiasa huyo?

Kama uongozi ulioko madarakani hivi sasa unaweza kuliongoza taifa hili, Pamoja na tofauti kubwa iliyopo juu ya uzingatiaji sheria na katiba ya nchi na bado kuna wananchi wanasifia basi kamanda LISSU ni hazina pekee ya taifa hili ambayo haina wa kufanana nae.

Ni msomi, jasiri, ana akili, amajiini, mi mkweli,hadanganyiki, ni mtendaji safi, ni mwanasiasa safi. Kwa hakika huyu mtu sina kiongozi wa kumfananisha xndani ya taifa hili. Namuombea uzima tele Mungu aendelee kumwongoza vema katika harakati zake za kutetea haki za wanyonge.

Kama Rais tuliyenaye kwa sasa atafanikiwa kulifikisha taifa kama alivyoahidi, akatekeleza ahadi zake kama alivyoahidi basi kiumbe pekee anayefanana naye kwa misimamo na kiutendaji japo kuna tofauti ya intelligence ni Tundu Lissu Pekee.

Kwa wasiofahamu ni kwamba Tundu LISSU ni mbunge pekee Tanzania ambaye wakati wa uchaguzi wa October 2015 CCM walipeleka nguvu kubwa sana kwakwe kuliko hata wengine ya mgombea Urais, Lakini poja na hujuma zote, pamoja na aliyekua akipambana nae ni ndugu yake Tundu Lissu alichomoa.

Mwaka 2010 wakati wa uchaguzi aliyekua mgombea Urais kupitia CCM wakati huo Rais mustaafu JM. Kikwete aliuambia umma wwatanzania kua "Ni bora Dr Slaa kushinda kiti cha Urais kuliko Tundu Lissu kushinda ubunge".Haya sio maneno yangu,yalikua maneno ya Kikwete! Kikwete alikua kawaida,hakua akitania bali alinena ukweli wa moyo wake,alisema alichokifahamu na alichokiona kwa Tundu LISSU.Nadhani angekua ni mwanaCCM wakati huo sijui JK angempa cheo gani ndani ya serikali yake.

Ukubali ukatae Tundu Lissu baada ya Magufuli ndiye kichwa pekee cha kuliongoza taifa hili, kama wananchi wataipenda aina ya utawala wa Rais Magufuli pasina shaka kabisa kwa umahiri na umakini wa Lissu Chadema waanze kukiweka chama kimaandalizi katika mkao wa kuliongoza taifa hili.Sioni kabisa mtu wa aina LISSU katika taifa hili.

Jamani mimi hua najiuliza sana, hivi ni mpaka sasa ni nani wa kusimama na Mh Tundu Lissu kwenye kitu cha Urais akapambana nae akamshinda? Tuwe waungwa kuusema ukweli ni nani anaweza kushindana na Lisuu kwa nafasi yeyote ile?

Tupate katiba mpya na bora, tupate tume huru ya uchaguzi na mwisho Chadema watazame wakati tulionao na mahitaji ya sasa,zaidi ya hapo sina la kuongezea.Nimalizie kwa kumtakia kaka yangu Tundu Lissu kila lakheri na Mungu amuongoze na awe salama ndani ya mikono ya polisi kwa sasa, aendeleze mapambano tuko nyuma yake na pia figisu figisu anazozipata atambue kua ni mapito haya.
 
Hiyo ni nafasi ya kudumu ya Edo kila mtu anafahamu hilo ndani ya Chadema.

Kama Tundu ana mawazo hayo ayafute kabisa hatutaki vurugu.

Yeyote atakayethubutu kuchukua fomu ya urais 2020 ndani ya chadema zaidi ya Lowasa tutamfukuza uanachama.

hahahhahahaha...Unajidanganya...mlisema hivo hivo kwa slaa
 
Hiyo ni nafasi ya kudumu ya Edo kila mtu anafahamu hilo ndani ya Chadema.

Kama Tundu ana mawazo hayo ayafute kabisa hatutaki vurugu.

Yeyote atakayethubutu kuchukua fomu ya urais 2020 ndani ya chadema zaidi ya Lowasa tutamfukuza uanachama.
Pia tutampoteza kabisaaaa:D bado tuna deni la kumlipa Edo, tumekula vingi na bado tunakula hivyo itakuwa hatujamtendea haki.
 
Hiyo ni nafasi ya kudumu ya Edo kila mtu anafahamu hilo ndani ya Chadema.

Kama Tundu ana mawazo hayo ayafute kabisa hatutaki vurugu.

Yeyote atakayethubutu kuchukua fomu ya urais 2020 ndani ya Chadema zaidi ya Lowasa tutamfukuza uanachama.
Acha hizo kwani wewe ni mungu?! Ski RIP ataendelea au unadhani cye wa hko lmba ambao zenj wameifny yao?!
 
Mbona lumumbu mwenzako yaani lizabon juzi alisema ukawa tunamjenga zitto..inamaana hapo lumumba siku hizi hamjadiliani kabla ya kupost kama zamani?
 
Hivi Ukawa mtaongeza vyama shiriki au hivyo vinne vimetosha? Vipi ACT-Wazalendo wanatamani kujiunga nafasi IPO? Nikijua hilo nitajibu swali la mtoa mada.
 
Back
Top Bottom