Je, Lissu anajijenga ili kugombea Urais 2020?

Je, Lissu anajijenga ili kugombea Urais 2020?

Hatimaye.....
Anajisumbua tu. Anajua fika hana sifa za kugombea ubunge, achilia mbali uraisi kwa kosa la kukiuka maadili ya viongozi wa umma kama ilivyobainishwa na spika. Alifungua kesi mahakama kuu kupinga suala hilo akashindwa. Akakata rufaa mahakama ya rufaa akashindwa!
 
Anajisumbua tu. Anajua fika hana sifa za kugombea ubunge, achilia mbali uraisi kwa kosa la kukiuka maadili ya viongozi wa umma kama ilivyobainishwa na spika. Alifungua kesi mahakama kuu kupinga suala hilo akashindwa. Akakata rufaa mahakama ya rufaa akashindwa!
ngoja tuone hatma yake
 
Kama uropokaji Ungekuwa kigezo cha kuukosa urais !! Basi Tz kwa sasa isingekuwa na kiongozi!!! Lissu yuko vizuri kuliko unaowaabudu [emoji87] [emoji85]
Mropokaji na hana hoja za msingi. Kwa mtu makini huwezi kulalamika serikali kukusana kodi. Wakati kodi ndio uti wa mgongo wa serikali.
 
Hii ni kama strategy ya ukawa kujenga mgombea wake kwa mwaka 2020, baada ya kuone appointment ya Katibu mkuu kukosa mwito ndani na nje ya muunganiko huo.

Kauli na matendo ya Lisu yanaonyesha muelekeo wa kujijenga kisiasa kwa lengo la kugombea nafasi hiyo.

Ikumbukwe kwamba bado kuna pingamizi za ndani kwa ndani ukawa kama Lowasa atasimama kwa tiketi hiyo ifikapo uchaguzi mkuu, hii ni kutokana na yeye kuzidi kupungua ushawisi ukilinganisha na kipindi cha uchaguzi wa 2020.

Saikolojia ya mwanadamu unaonyesha kwamba mtu anayekipinga kitu flani sana either anakipenda sana au anahisi kama aliyenacho hastahili kuwa nacho isipokua yeye.

Saikolojia hii ndogo inapelekea wengi wetu kuanza kunyanyua kope za macho na kujiuliza nia halisi ya Lisu baada ya kuona na kusikia haya aliyoyafanya hivi karibuni.

Je, huu ndio mwanzo wa safari ya kugombea nafasi hiyo 2020, na mwendelezo wa matukio toka kwa mwanasiasa huyo?
Ulikuwa sahihi.
 
Mkuu kwa mda mfupi ambao Lissu yupo hapa nchini, nimesikiliza hotuba zake na nilichokibaini ni kuwa binadamu huyo anahitaji washauri wazuri sana wa saikolojia. Vinginevyo atagombea urais kwa mwaka huu na hatarudia tena kugombea kwani thani yake itashuka sana.

1. Mda wote amekuwa ni mtu wa kutaka huruma ya kupewa nchi kwa sababu tu alipigwa risasi. Haelezei sababu ya yeye kupigwa risasi. Na hii inapelekea watu kuamini yanayosemwa kuwa alikuwa akiisaliti nchi ndiyo maana ya kushambuliwa.

2. Ameonyesha chuki ya wazi kwa JPM hii inawapelekea wengi kufikilia ya kuwa lengo lake ni apate uraisi ili alipe kisasi kwa JPM na siyo kutuletea maendeleo. Adui yako asijue kama na wewe ni adui yako.

3. Amekuwa akikosoa kwa nguvu zote miladi mikubwa iliyoanzishwa na JPM pasipo kuelezea mbadala wake.

4. Ana asili ya dharau ambayo inatakiwa ashauliwe kuificha. Aache kujisifia uelewa. Watu ndiyo wanajua kuwa wewe una uelewa lakini wewe huwezi kujielewa kwa kina. Na mtu mwenye kujisifia kuhusu uelewa kuwa yeye ana uelewa sana daimu huwa hapokei ushauri toka kwa mtu. Kwani anajiona kuwa uelewa anawazidi watu wote.

4. Ashauriwe aonyeshe heshima hata kidogo kwa raisi wa nchi kwani ndiye kiongozi mkuu wa nchi. Maneno ya mtaani KAMA HAMHESHIMU RAIS RAIA WA KAWAIDA ATAKUHESHIMU?
Ni sahihi kabisa mkuu.
 
Safari inakaribia kufikia ukingoni.
 
Yaani Lissu awe Rais wa nchi hii? Uko serious kijana!!
Kwani kuwa rais wa Tanzania ni ajabu..Obama anakuwa raisi wa marekani from nowhere..sembuse Tundu Lissu who is a household name..acheni kujiona kuwa raisi ni kitu kigumu au haliwezekani au hana huo uwezo .......msijitekenye bureee....do not underestimate the power and the will of Tundu lissu and Tanzanians as well...Watanzania sio wajinga
 
Safari ya Tundu Lisu Kuwania Urais imefikia tamati.

Tundu kaangushwa na Dr. John Joseph Magufuli aliyepata Kura Milioni kumi na Mbili , huku Tundu Lisu akipata kura Milioni Moja na Laki tisa.

Je , mwisho wa safari moja ndio mwanzo wa nyingine??

2025 ina siri gani??

Tusubiri na kuona yatayojiri.
 
Back
Top Bottom