Je, kwa mujibu wa Bernard Membe, vyombo vya usalama na ulinzi havifanyi kazi kwa mujibu wa sheria?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,349
6,476
Katika mahojiano kati ya Mhe. B. C. Membe na Sammy Awami wa BBC Swahili, alisikika akijibu swali linalohusu vyombo vya usalama na ulinzi vya dola kuingilia masuala ya uchaguzi wa kisiasa; mfano, Urais, Wabunge na Madiwani na kuharibu usawa katika uwanja huo.

Akiwa kama 'kachero mbobezi na mwandamizi mstaafu', alisema vyombo hivyo ufuata 'tune' ya Rais. Yaani utendaji wake uendana na Rais aliyepo madarakani. Akiwa mzoefu na kazi hiyo, sina shaka na jibu lake ambalo limeniletea swali, je, vyombo hivi havifuati sheria na kanuni? Je, sheria zake no 'boya' tu? Kama basis ya utendaji wake ni Rais, je state yetu ipo sawa kweli?

 
Ni kweli, vyombo vya dola ni vya mwenye dola, polisi wanaozuia mikutano leo, ndio juzi walikuwa wanaruhusu operation sangara.
 
Kwa nini akubadili huu mfumo akiwa madarakani kama waziri na pia kachero mbobezi?
 
Huyu si inasemekana alikuwa mtu mzito kule kwa wasiojulikana? Mchango wake ulikuwa upi kubadili huo mfumo mbovu?
 
Umeonaaa... Wakiambiwa watengeneze katiba mpya wakiwa madarakan hawatak wakitemwa nje wanaanza kulia lia

Separation of power hakuna wanafikir watadumu milele

Ngoja Mimi niendelee kula maisha huku ughaibuni huko mtaletewa mwili wangu tuu muuzike
Haya mambo yanaudhi Sana
 
Huyu si inasemekana alikuwa mtu mzito kule kwa wasiojulikana? Mchango wake ulikuwa upi kubadili huo mfumo mbovu?

Ubinafsi ilikuwa ni kikwazo. Wakati akiwa huko alikuwa ananufaika na hiyo hali, kwa sasa yeye ni Muhanga ndio maana analia. Hiyo inaitwa mwisho wa ubaya.
 
Back
Top Bottom