Je, kuwa na mtoto ni lazima?

Je, kuwa na mtoto ni lazima?

flamini

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2015
Posts
598
Reaction score
797
Habari zenu wadau,

Nilikua nahitaji mitazamo yenu kuhusu kuzaa watoto, je kuna ulazima wa kuwa na mtoto hapa duniani hata kama umeoa? Binafsi mimi sipendi watoto na sina mpango wa kupata mtoto hata kama nikioa nitatafuta ambaye mgumba au mwenye malengo kama yangu.

Sababu kuu ya kufanya hivo ni kua watoto ni energy, time and money consuming plus wanaleta stress tu, nataka maisha ya kua free sitaki majukumu yanaoweza kunihold back katika mambo yangu. Je, jamii inalichukuliaje swala hili? Naamini sipo peke yangu mwenye mawazo kama haya.

Karibuni wadau mtoe mitazamo yenu
 
Mmh sikhlaumu lakini najaribu kufikir kama baba na mama yako wangekuwa na mawazo kama yako!!!!!
kila mtu ana priority na goals zake katika maisha,mimi nimechoose hivo..watoto wa ndugu wapo kibao wa kusaidia but mimi kama mimi i choose not to have kids
 
Nimeshakutana na watu dizaini yako, haswa huko Marekani kuna watu hawazai sio kwamba hawana kizazi ila wanaona watoto ni usumbufu.

Wanaishia kuwa na mbwa kama watoto. Wengine wanathamini sana kazi zao kuliko kuzaa.

Ila mimi kwangu mtoto ni faraja yangu, yaani nisingekuwa na mtoto sijui ingekuwaje?

Hivyo fuata moyo wako, ila usichukie watoto. Jitahidi kupenda watoto wa jirani na ndugu zako, hata kama huna mpango wa kuwa baba.
 
thank you,atleast umenielewa,.na simaanishi nachukia watoto ila nachukia kua na jukumu la kua na mtoto..mimi ni mtu wa kutotulia sehemu moja,napenda kutembea na napenda niwe naweza kuishi sehemu yoyote bila kua na kitu cha kunihold back
 
Heri yako wewe unayejitambua.

Kuzaa watoto na kushindwa kuwahudumia na kuishia kuwatwisha wengine mzigo wako si sawa hata kidogo.

Au kuzaa watoto na kuishia kutokuwapenda kwa kuwatendea vibaya nayo si sawa.

Unakuta jitu limezaa mtoto lakini hata halimjali...halimpendi....mtoto kila siku anasumbuliwa na sonona kwa sababu hapati mapenzi ya mzazi au wazazi.

Ya nini kuleta kiumbe hapa duniani halafu unakitelekeza? Mijitu ya namna hiyo ina mioyo ya ajabu kweli.

Ni heri kutokuzaa kabisa kuliko kuzaa na kushindwa kutizimiza wajibu wako kama mzazi.

Inauma sana kuona vitoto visivyo na hatia yoyote ile vikihangaika hapa duniani.

Hakuna mtoto anayeomba kuzaliwa na mzazi wake.

Nawachukia kwa nguvu zangu zote wazazi watelekezaji.
 
Na watoto wa wazazi dizaini hiyo ndo wanakuja kuwa troublemakers wakubwa
na wengine criminals kabisa
 
ni kweli mkuu,inauma sana nikiona hivo tena mtu anasema anataka kuacha jina hapa duniani akifa..
 
Kabala hatujasonga mbele popote mkuu ningependa nifahamu umri wako, maana unajua mawazo kama haya huwa yanaendana na umri pamoja na majukumu uliyonayo kwa mda husika,

i hope after 3 up to 5 five years utakuwa umebadilisha muelekeo kama utakuwa bado productive, asikuambie mtu mtoto analeta raha kwenye famili hata akiwa moja, unataka kunambia wewe utakaa na mwenzwako tena kwenye ndoa

let say 25 years to come bila mtoto kama matasa vile, sjui labda wewe au huyo utakaemuoa awe mgumba, maana hata wagumba wenye wanataka watoto
 
Kuwa na watoto si lazima mkuu ni chaguo lako binafsi.Dhumuni la kuwa na watoto ni kuendeleza kizazi tulichonacho na kukamilisha dhumuni zima la maisha.Ulizaliwa na ni dhumuni na wewe uzae na wanao wazae na hii ni kwa viumbe hai wote.Ili genes zisipotee na upate wa kurithi mirathi yako.

Walio wengi wanaona kuzaa ni pride ili na wewe upate wadhifa wa kuitwa mzazi lakini si kila mwanaadamu anakidhi fani hii.Kama wewe binafsi unatambua huoni furaha ya kuwa na mtoto/watoto then huna haja ya kuwa nao.

Watoto hutupa furaha ya maisha na malengo ya kuishi,hutupa sababu ya kufikiria kesho na motisha ya kupambana na changamoto tofauti za kila siku.Kwangu mimi mwanangu ni dira yangu!
 
Kuwa na watoto si lazima mkuu ni chaguo lako binafsi.Dhumuni la kuwa na watoto ni kuendeleza kizazi tulichonacho na kukamilisha dhumuni zima la maisha.Ulizaliwa na ni dhumuni na wewe uzae na wanao wazae na hii ni kwa viumbe hai wote.Ili genes zisipotee na upate wa kurithi mirathi yako.

Walio wengi wanaona kuzaa ni pride ili na wewe upate wadhifa wa kuitwa mzazi lakini si kila mwanaadamu anakidhi fani hii.Kama wewe binafsi unatambua huoni furaha ya kuwa na mtoto/watoto then huna haja ya kuwa nao.

Watoto hutupa furaha ya maisha na malengo ya kuishi,hutupa sababu ya kufikiria kesho na motivation ya kupambana na changamoto tofauti za kila siku.Kwangu mm mwanangu ni dira yangu!

Stranger wangu una busara always! Napenda sana watoto, kuna wakati hata nimekuwa napitiliza vituo once nikitumia public transport pale tu inapotokea nimepanda siti mkabala na mtu alobeba mtoto mdogo...

Ni wazo zuri kwa kipindi fulani kuamua kutokuwa na watoto ila demerits zake ni kubwa mno once ukijaaliwa kuuona uzee wako. Hata kama utakuwa umejiwekeza kiasi gani ila kuna mammbo ambayo ukwasi wako hauwezi kukufanyia na hapa ndipo utajua umuhimu wa kuwa na uzazi!
 
Heri yako wewe unayejitambua.

Kuzaa watoto na kushindwa kuwahudumia na kuishia kuwatwisha wengine mzigo wako si sawa hata kidogo.

Au kuzaa watoto na kuishia kutokuwapenda kwa kuwatendea vibaya nayo si sawa.

Unakuta jitu limezaa mtoto lakini hata halimjali...halimpendi....mtoto kila siku anasumbuliwa na sonona kwa sababu hapati mapenzi ya mzazi au wazazi.

Ya nini kuleta kiumbe hapa duniani halafu unakitelekeza? Mijitu ya namna hiyo ina mioyo ya ajabu kweli.

Ni heri kutokuzaa kabisa kuliko kuzaa na kushindwa kutizimiza wajibu wako kama mzazi.

Inauma sana kuona vitoto visivyo na hatia yoyote ile vikihangaika hapa duniani.

Hakuna mtoto anayeomba kuzaliwa na mzazi wake.

Nawachukia kwa nguvu zangu zote wazazi watelekezaji.

Umegusia point nzuri mkuu Nyani Ngabu,bora mtu asizae kama anajijua hawezi ulezi kuliko kuwapa mateso tu viumbe wasio na hatia.

Watoto ni baraka na ni tunu tunayotakiwa tuitunze.Na mtoto jinsi unavyomlea ndio anavyokuwa.Mtoto hana furaha,hajiamini,hapati matunzo mazuri outcome yake haitokuwa nzuri, unakuta mzazi mwenyewe hajali maslahi ya mwanawe unafikiri huyo mtoto atakuwaje?

Kama mtu hawezi ulezi bora akae pembeni tu maana ulezi ni kazi nzito!!
 
Last edited by a moderator:
Stranger wangu una busara always! Napenda sana watoto, kuna wakati hata nimekuwa napitiliza vituo once nikitumia public transport pale tu inapotokea nimepanda siti mkabala na mtu alobeba mtoto mdogo.

Ni wazo zuri kwa kipindi fulani kuamua kutokuwa na watoto ila demerits zake ni kubwa mno once ukijaaliwa kuuona uzee wako. Hata kama utakuwa umejiwekeza kiasi gani ila kuna mammbo ambayo ukwasi wako hauwezi kukufanyia na hapa ndipo utajua umuhimu wa kuwa na uzazi!

Ha ha ha umenifurahisha ww unapitisha mpaka vituo loool itabidi uzae sasa na ww uitwe baba fulani nami niitwe Aunty G!!Halafu nilisahau kukushukuru...ahsante sana!!
 
yah ni kweli unavosema,ila kaa ukijua unaweza ukapata mtoto akawa dissappointment kubwa kwako baadae
 
Ha ha ha umenifurahisha ww unapitisha mpaka vituo loool itabidi uzae sasa na ww uitwe baba fulani nami niitwe Aunty G!!

Niombee Stranger wangu...haya mambo though ni binafsi ila tusipomshirikisha Mungu tokea awali mwisho wake hauwi mwema...
 
Stranger wangu una busara always! Napenda sana watoto, kuna wakati hata nimekuwa napitiliza vituo once nikitumia public transport pale tu inapotokea nimepanda siti mkabala na mtu alobeba mtoto mdogo..

Ni wazo zuri kwa kipindi fulani kuamua kutokuwa na watoto ila demerits zake ni kubwa mno once ukijaaliwa kuuona uzee wako. Hata kama utakuwa umejiwekeza kiasi gani ila kuna mammbo ambayo ukwasi wako hauwezi kukufanyia na hapa ndipo utajua umuhimu wa kuwa na uzazi!
kama vitu gani mkuu?mi najua kama utaishi vizuri na ndugu na watoto wa ndugu hutokosa kitu sababu pia wao ni watu wa karibu
 
yah ni kweli unavosema,ila kaa ukijua unaweza ukapata mtoto akawa dissappointment kubwa kwako baadae

Mkuu hayo yanakuwa matokeo.Maisha ni kama mtihani kuna kufanikiwa na kutokufanikiwa(wakati mwengine unapambana lakini bado unafeli).Tunapambana kila kukicha kwaajili ya maisha bora ya kesho lakini yet we cant predict the future.

Ni sawa na kuvuta pumzi tuna matumain ya kuamka kesho na tupumue maisha yaendelee lakini hatujui utaamkaje waweza amka mgonjwa utaabani.Tunachopaswa kufanya ni kumshukuru mungu kwa leo na kuomba/kuwish for a better tommorrow.

Na tunachotakiwa kufanya kama wazazi/guardians tunalea na nguvu zetu zote pamoja na busara na hekima kwa tarajio la matunda bora."AGAIN YOU CANNOT PREDICT THE FUTURE"
 
kama vitu gani mkuu?mi najua kama utaishi vizuri na ndugu na watoto wa ndugu hutokosa kitu sababu pia wao ni watu wa karibu

Uchaguzi wa kuamua kuishi bila kuzaa watoto,huku ukiwa huna tatizo kiafya ni ubinafsi wa hali ya juu simply cause Life rejuvenates and acquires energy when it multiplies: It is enriched, not impoverished...ni kanuni ya uumbaji hutakiwi kuiblock!
 
Back
Top Bottom