Je! Kuvuta Sigara ni Dhambi?

Kwa sisi waislamu, uvutaji sigara ni haramu, kwa hiyo ni dhambi, ingawa watu watajitokeza kupinga. Ni tabia mbaya sana ambayo inachafua mazingira na ni ishara ya maporomoko ya maadili. Karibu kote duniani, uvutaji sigara hadharani imepigwa marufuku. Nairobi wavutaji sigara wametengewa maeneo maalum vya kuvuta sigara, kuvuta barabarani ni kosa! Hapa kwetu mbona bado haijapigwa marufuku?
Sigara inalewesha?
 
Kwahiyo unakataa kuwa computer haina madhara au kipi unapinga? suala la tahadhari sio sababu inategemea serikali inanufaika vip na ilo suala, mbona serikali nyingine zimeruhusu ushoga lakini nyingine zimekataa , hapa Tunazungumzia kipimo gani kimetumika kufanya madhara ya sigara yawe dhambi lakini madhara ya computer ambayo ni cancer n.k isiwe dhambi ? jikite hapo

I'm just wasting my time with you. Huna la maana ya kuzungumza, so I'm not replying again!
 
Uvutaji wa Sigara ni Dhambi kwakuwa.
1. Ni madawa ya kulevya
2. Haina faida yoyote kwa afya ya mwili wako.
3. Ina haribu Afya ya mwili wako uliotengenezwa kwa thamani kubwa sana.
4. Ina haribu Afya ya walio jirani yako.
5. Ina (adiction) inayokupelekea kudhohofisha akili yako ifikirie kuvuta sigara badala yawaza mambo ya maana.
6. Unakupotezea muda na kipato chako bila faida yoyote.
7. Ni Sumu kali unayokudhohofisha siku hadi siku, maisha ya wavuta sigara ni mafupi.
8. Inasababisha kushambuliwa na magonjwa hatarishi kama TB na Kansa
9. Inashawishi wengine kuiga tabia ya uvutaji ambayo haina faida yoyote.
10, Inakuchafua kwa harufu mbaya, uchafu na kuwa kero kwa mkeo na watu wa karibu yako.
NAKADHALIKA.
Safi nimependa mkuu
 
Sigara inalewesha?
Ndio Sigara inalewesha ndio maana inavutwa.
Ipo Dhambi ya Ulevi ambayo imesemwa.
Ulevi ni pamoja na
1. Kunywa kilevi kinachouzwa sokoni kupita kiasi. ni ulevi.
2. Kunywa kilevi, (hata iwe kwa kiasi kidogo) kisichopimwa na wataalam wa Afya kama pombe ya Gongo. ni ulevi.
3. Kunywa pombe wakati wa kazi (ndio maana serikali imeamrisha kufungua mabaa kuanzia saa kumi jioni ) ni ulevi.
4. Kutumia kipato cha huduma nyinyine na kukinywea pombe ( mfano nyumbani wanakosa chakula wewe unanunua bia baa na kunywa ) ni ulevi.
5. Kutumia vilevi hatarishi kama madawa ya kulevya, Bangi, Sigara, Petroli, Mirungi nk. ( hivyo hata ukitumia kidogo sana wewe ni mlevi tu) ni ulevi.
Nk
Hivyo kuvuta sigara ni ulevi kwa maana kwamba ni kihatarishi cha afya yako.
 
Naomba mada iendelee tafadhar......mana mpka sasa hakuna aliemjibu mleta mada
 
Chochote kilicho hatari kwa afya na,maisha yako si vizuri kukiendekeza...

Unaweza sema dhambi...


Cc: mahondaw
 
2.kuendesha gari kunahatarusha Hali yako na jirani yako kwa maana hiyo nayo Ni dhambi .
Binadamu tunapenda kujitungia maandiko yetu
Nani kasema kuendesha gari ni dhambi ?
Mbona unajitungia maneno na kuhukumu wengine ?
Kuendesha gari kunahatarishaje hali ya jirani yako.
Kama unaendesha bila leseni basi ni sawa na ni dhambi kweli, kama una leseni haina shida.
 
Wakuu Salaam.

Naamini mko salama, na kwa wale mliopata nafasi ya kuhudhuria ibada ni matumaini yangu mmekuwa na ibada njema.

Moja kwa moja kwenye swali langu, Je! Kuvuta sigara ni dhambi?

Naomba ku - declare interest kuwa binafsi si mvutaji wa sigara na sina mpango wa kuwa mtumiaji, lengo la uzi huu ni kutaka kuongeza ufahamu na uelewa.

Kwa muda nimekua nikisikia watu mbalimbali wanapokuwa wakitoa hotuba za mahubiri na hata leo nimelisikia tena waki-categories uvutaji wa sigara kama mojawapo ya dhambi, ingawa ni kweli uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya lakini Biblia haitaji wazi kuwa uvutaji wa sigara ni dhambi kama ilivyotaja wazi kwa mfano uzinzi, uasherati, wizi, ufisadi, ufiraji nk nk nk kuwa ni dhambi na viko vifungu ktk Biblia vinaeleza hilo kwa uwazi kabisa.

Naomba kwa wataalamu wa maandiko walioko humu wanisaidie kufahamu ni sehemu gani ktk Biblia imeandikwa uvutaji wa sigara ni dhambi au hawa wanao - categories uvutaji wa sigara kama mojawapo ya dhambi wanatumia maandiko yapi na kwa nini.

Thanks in advance kwa elimu nitakayoipata hapa.
Kiukweli sigara ni dhambi kwa sababu Neno la Mungu linasema kwamba;

Hamjui kuwa nyinyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu ambalo ndilo ninyi. (1Kor.3:16,17)

Sasa kama mimi na wewe ni mahekalu ya Roho mtakatifu; tutasalimikaje tujiharibu kwa sigara?

Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala nyinyi si Mali yenu wenyewe. (1Kor.6:19)

Kwa mafungu haya mawili, moja kwa moja uvutaji wa sigara ni uasi kama uasi mwingine.
 
Sigara inalewesha?

Mkuu, sigara haileweshi, lakini wavutaji sugu wakikosa fegi, wanaonyesha 'withdrawal symptoms', yaani wanajisikia vibaya, kichwa kinaumiza na mikono zinatetemeka, yote kwa sababu ya kukosa dozi yao ya nicotine!
 
sio dhambi ila ni hatari kwa afya ya mwili., dhambi hutokana na uvunjifu wa amri kumi.
 
Ni dhambi kwasababu uvutaji wa sigara unaharibu mwili aliokupatia mwenyezi Mungu huku ukiwa unatambua kabisa uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako.
 
Kwa sisi waislamu, uvutaji sigara ni haramu, kwa hiyo ni dhambi, ingawa watu watajitokeza kupinga. Ni tabia mbaya sana ambayo inachafua mazingira na ni ishara ya maporomoko ya maadili. Karibu kote duniani, uvutaji sigara hadharani imepigwa marufuku. Nairobi wavutaji sigara wametengewa maeneo maalum vya kuvuta sigara, kuvuta barabarani ni kosa! Hapa kwetu mbona bado haijapigwa marufuku?
Niliwahi kumsikia shehe mkuu (Mufti) aliyepita akikiri kuwa alikuwa anavuta sigara alipokuwa kijana!
 
Reference ni Biblia,
Marko 12 : 28-31

" 28 Na mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza?

29 Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;
30 nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.

31 Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi. "

( Usipotenda yanayompendeza Mungu na Jirani yako ni dhambi )
Hamna utetezi hapa
 
Dhambi haiwezi kuwa dhambi kama hamna Katazo/sheria! Ukivunja sheria mojawapo kati za hizi apo chini ndio unamtendea Mungu dhambi, mengine ni makatazo ya kibinadamu wakijaribu kuutawala mwili kwa ukali lakini hayaondoi tamaa za mwili.

KUTOKA 20

1 Mungu akanena maneno haya yote akasema,
2 Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.
4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
7 Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
10 lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
11 Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
13 Usiue.
14 Usizini.
15 Usiibe.
16 Usimshuhudie jirani yako uongo.
17 Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng?ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.


Kama dhambi ya sigara inatokana na madhara yake kimwili, basi tuseje kuhusu mafuta ya kula yenye rehemu au nyama nyekundu tuseme na kula ivyo vitu ni dhambi kisa vinaharibu mwili?
tumsifu YESU KRISTU mkuu.
 
Niliwahi kumsikia shehe mkuu (Mufti) aliyepita akikiri kuwa alikuwa anavuta sigara alipokuwa kijana!

Tuseme tu, kuwa kwenye ujana wake mufti alikuwa amepotea. Baadaye akapata hidaya (mwongozo) na akaokoka!
 
Kama hutumii usiwasemee wanao tumia, Bora nimuache mke wangu kuliko kuacha Sigara.

Nikiwa na stress inanituliza na kuniliwaza, nikiwa na furaha hasa nikishiba ndio burudani haswaa.

Hapa yenyewe navuta, najua lote ili naenda Dukani bila shida kabisa.

Nimekubali kufa na kifo cha mapaff haina shida Maana Mungu ni mwema. Wewe binadamu damu unaishi hujui utakufa kwa tatizo lipi? Kama dhambi bora niingie motoni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom