Je! Kuvuta Sigara ni Dhambi?

Je! Kuvuta Sigara ni Dhambi?

Uvutaji wa Sigara ni Dhambi kwakuwa.
1. Ni madawa ya kulevya
2. Haina faida yoyote kwa afya ya mwili wako.
3. Ina haribu Afya ya mwili wako uliotengenezwa kwa thamani kubwa sana.
4. Ina haribu Afya ya walio jirani yako.
5. Ina (adiction) inayokupelekea kudhohofisha akili yako ifikirie kuvuta sigara badala yawaza mambo ya maana.
6. Unakupotezea muda na kipato chako bila faida yoyote.
7. Ni Sumu kali unayokudhohofisha siku hadi siku, maisha ya wavuta sigara ni mafupi.
8. Inasababisha kushambuliwa na magonjwa hatarishi kama TB na Kansa
9. Inashawishi wengine kuiga tabia ya uvutaji ambayo haina faida yoyote.
10, Inakuchafua kwa harufu mbaya, uchafu na kuwa kero kwa mkeo na watu wa karibu yako.
NAKADHALIKA.
Sigara hiyo
 
Computer ina madhara, simu ina madhara unalijua hilo, je nikikujulisha utaacha kutumia mkuu? au tunayapima madhara kwa kipimo gani mkuu?
Kama nikijiridhisha ina madhara sitaitumia.
Maana itakuwa dhambi kwangu, lete ushahidi mkuu.
 
Asante sana mkuu, kwa kunipa heshima! Dalili kwenye Quran tukufu si wazi kabisa, lakini kuna aya zinazotaja "shajaratul maloona" yaani mti yenye laana, na hii imetafsiriwa na baadhi ya maulema kuwa ni tumbaku. Ni kitu ambayo imejaa laana tupu - hakuna mimea ambayo inamadhara kwa binadamu kama tumbaku. Kwenye kilimo pia tumbaku inadhoofisha rutba ya ardhi na kuicha isiweze kutumika tena kwa miaka kadha! Pombe, ingawa pia ni kitu haramu na kibaya, lakini bado inamanufaa fulani kwenye mwili, mfano kuua bacteria nk., lakini tumbaku haina manufaa hata kidogo kwa binadamu. Tumbaku inazuia baraka na kuvuta balaa mmoja kwa mmoja bila fani!
",baadhi ya maulamaa" hili neno linatosha kuonyesha kuwa hilo ni jambo ambalo hawajakubaliana maulamaa wote , hivyo linabaki kuelea hewani tu , anaesema dhambi shauri yake na anaesema makruhu shauri yake
 
Dhambi haiwezi kuwa dhambi kama hamna Katazo/sheria! Ukivunja sheria mojawapo kati za hizi apo chini ndio unamtendea Mungu dhambi, mengine ni makatazo ya kibinadamu wakijaribu kuutawala mwili kwa ukali lakini hayaondoi tamaa za mwili.

KUTOKA 20

1 Mungu akanena maneno haya yote akasema,
2 Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.
4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
7 Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
10 lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
11 Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
13 Usiue.
14 Usizini.
15 Usiibe.
16 Usimshuhudie jirani yako uongo.
17 Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng?ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.

Kama dhambi ya sigara inatokana na madhara yake kimwili, basi tuseje kuhusu mafuta ya kula yenye rehemu au nyama nyekundu tuseme na kula ivyo vitu ni dhambi kisa vinaharibu mwili?
Uvutaji wa sigara ni dhambi.
Dhambi ni nini?
Dhambi ni uasi wa sheria.
Sheria ni nini?
Sheria ni makato yote yaliyoamriwa na muumbaji. i.e, amri kumi za Mungu.
Sheria inaweza kuwa spiritual au natural.
Mfano sheria zote zinazosema, usiwe na Miungu mingine, Sanamu usiziabudu, Usilitaje bure jina la Muumabaji na ikumbuke sabato ni natural, na nyinginezo ni natural. Yaani hata ukila sana ukavimbiwa ni dhambi kwa sababu unauharibu huu mwili.
Mtume Paulo anasema, je hamjui kuwa miili yenu ni hekalu la roho mtakatifu, mtu akiuharibu hekalu hilo ambalo ni mwili wako Mungu naye atamharibu mtu huyo. Matendo yote yenye kuharibu mwili ni dhambi sio sigara tu na vinginevyo vyote.
 
Kama nikijiridhisha ina madhara sitaitumia.
Maana itakuwa dhambi kwangu, lete ushahidi mkuu.
Computer ina toa radiation ambazo kiafya ya binadamu haifai , wamejaribu kupunguza kiwango chake lakini hawakuweza kuondoa yote , madhara ya zile radiation ni kama ifuatavyo
1.Cancer
2.Miscarriage
3.Birth defects
Wataalamu wanashauri ili kupunguza madhara kuna njia mbili
1.Kupunguza muda wa kuitumia
2.kuweka mbali wakati unaitumia

Hitimisho :hakuna asiejua ubaya wa cancer mkuu nakushauri acha computer ni dhambi
 
Shaka -Zulu heshima yako mkuu, kwa uelewa wangu sigara katika uislamu si dhambi bali makuruhu (yaani ni kama kero kwako na kwa Wengine), makuruhu ikizidi hua ni dhambi,
Kama una dalili basi leta (dalili mfano hadithi, aya, kisa n.k )
Nipo radhi kukosolewa
Every Intoxic is halam in Islam.
UNAPOTAKA KUTUMIA KITU ANGALIA FAIDA NA HASARA ZAKE. KAMA FAIDA NI NYINGI UNAWEZA TUMIA ILA KAMA HASARA NI NYINGI BASI NI HARAM KUTUMIA.
 
Computer ina toa radiation ambazo kiafya ya binadamu haifai , wamejaribu kupunguza kiwango chake lakini hawakuweza kuondoa yote , madhara ya zile radiation ni kama ifuatavyo
1.Cancer
2.Miscarriage
3.Birth defects
Wataalamu wanashauri ili kupunguza madhara kuna njia mbili
1.Kupunguza muda wa kuitumia
2.kuweka mbali wakati unaitumia

Hitimisho :hakuna asiejua ubaya wa cancer mkuu nakushauri acha computer ni dhambi
Nitakapo jiridhisha kuwa ni kweli nitafuata ushauri kwa wataalamu wa Afya.
Kama wataniambia niache kutumia basi na nitaacha.
Kumbuka kuna vitu huwa ni hatari kama utavitumia kwa kupita kiwango
Hata maji safi, ukiyanywa kupita kiwango chake yana madhara pia kwa Afya ya binadamu.

Imeandikwa
" muwe na kiasi kwa kila jambo "
 
",baadhi ya maulamaa" hili neno linatosha kuonyesha kuwa hilo ni jambo ambalo hawajakubaliana maulamaa wote , hivyo linabaki kuelea hewani tu , anaesema dhambi shauri yake na anaesema makruhu shauri yake

Lakini anayesema dhambi yuko pazuri duniani kuliko anayesema makruhu. Mwisho wa siku anayefahidi ni kampuni za sigara!
 
Nitakapo jiridhisha kuwa ni kweli nitafuata ushauri kwa wataalamu wa Afya.
Kama wataniambia niache kutumia basi na nitaacha.
Kumbuka kuna vitu huwa ni hatari kama utavitumia kwa kupita kiwango
Hata maji safi, ukiyanywa kupita kiwango chake yana madhara pia kwa Afya ya binadamu.

Imeandikwa
" muwe na kiasi kwa kila jambo "
Kwanini hiyo formular usiitumie kwenye sigara ni kwa kiwango gani cha matumizi sigara inakuwa haramu? maana tunaona watu wanazeeka wako fit na bado wanakula sigara saaafi
 
Lakini anayesema dhambi yuko pazuri duniani kuliko anayesema makruhu. Mwisho wa siku anayefahidi ni kampuni za sigara!
Siku zote mzalishaji anafaida ata kampuni ya computer inafaidi hivyo hilo sio tatizo kabisa, kama jambo linatafasiri nyingi wacha zisemwe ili kila mtu achague anapoona ni sahihi zaidi
 
Kwanini hiyo formular usiitumie kwenye sigara ni kwa kiwango gani cha matumizi sigara inakuwa haramu? maana tunaona watu wanazeeka wako fit na bado wanakula sigara saaafi
Sioni manufaa ya kuvuta sigara, kwani ni lazima kufanya kila kinachofanywa na wengine ?

Wewe unavuta Sigara ?
 
Shaka -Zulu heshima yako mkuu, kwa uelewa wangu sigara katika uislamu si dhambi bali makuruhu (yaani ni kama kero kwako na kwa Wengine), makuruhu ikizidi hua ni dhambi,
Kama una dalili basi leta (dalili mfano hadithi, aya, kisa n.k )
Nipo radhi kukosolewa
Hakuna kitu inaitwa makuruhu kwenye quran na hadithi. Ukitaka kujua kitu ni halali au haram na ukakosa kwenye quran na hadithi basi unacho takiwa kufanya ni kupima hicho kitu kwa akili.

Kama faida ya hiyo kitu ni kubwa kuliko hasara basi hiyo kitu itakua ni halali.

Na hasara ya hiyo kitu ikiwa ni kubwa kuliko faida basi hiyo kitu itakua ni haram.

Kwa hiyo hasara ya sigara ni kubwa kuliko faida, kwa hiyo sigara ni haram.

Na sigara ina dhuru afya ya mtumiaji. na quran inasema:
{{Wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo.}} [Al-Baqarah, 2: 125]
 
Kwa sisi waislamu, uvutaji sigara ni haramu, kwa hiyo ni dhambi, ingawa watu watajitokeza kupinga. Ni tabia mbaya sana ambayo inachafua mazingira na ni ishara ya maporomoko ya maadili. Karibu kote duniani, uvutaji sigara hadharani imepigwa marufuku. Nairobi wavutaji sigara wametengewa maeneo maalum vya kuvuta sigara, kuvuta barabarani ni kosa! Hapa kwetu mbona bado haijapigwa marufuku?
Kumbe waislam imeandikwa sigara Ni Haram ,ukinisaidia hili andiko nitashukuru Sana ,ukiwa huna andiko tubu maana alkadhibil haraam walaukana mizaha ,uongo Ni Haram hata Kama Ni mzaha.
 
Dhambi ni

1. Kufanya jambo lisilompendeza Mwenyezi Mungu.

2.Kufanya jambo ambalo lina hatarisha hali yako au ya jirani yako.
Yaani jambo lisilokupendeza wewe au Jirani yako.
2.kuendesha gari kunahatarusha Hali yako na jirani yako kwa maana hiyo nayo Ni dhambi .
Binadamu tunapenda kujitungia maandiko yetu
 
Kumbe waislam imeandikwa sigara Ni Haram ,ukinisaidia hili andiko nitashukuru Sana ,ukiwa huna andiko tubu maana alkadhibil haraam walaukana mizaha ,uongo Ni Haram hata Kama Ni mzaha.

Nimesha taja hapa juu Shajaratul Maloona kwenye Quran, kwa hiyo usijifanye mjuaji sana!
 
Uvutaji wa sigara ni dhambi.
Dhambi ni nini?
Dhambi ni uasi wa sheria.
Sheria ni nini?
Sheria ni makato yote yaliyoamriwa na muumbaji. i.e, amri kumi za Mungu.
Sheria inaweza kuwa spiritual au natural.
Mfano sheria zote zinazosema, usiwe na Miungu mingine, Sanamu usiziabudu, Usilitaje bure jina la Muumabaji na ikumbuke sabato ni natural, na nyinginezo ni natural. Yaani hata ukila sana ukavimbiwa ni dhambi kwa sababu unauharibu huu mwili.
Mtume Paulo anasema, je hamjui kuwa miili yenu ni hekalu la roho mtakatifu, mtu akiuharibu hekalu hilo ambalo ni mwili wako Mungu naye atamharibu mtu huyo. Matendo yote yenye kuharibu mwili ni dhambi sio sigara tu na vinginevyo vyote.
Je nikivuta na mwili wangu usiharibike inakuaje
 
Nitakapo jiridhisha kuwa ni kweli nitafuata ushauri kwa wataalamu wa Afya.
Kama wataniambia niache kutumia basi na nitaacha.
Kumbuka kuna vitu huwa ni hatari kama utavitumia kwa kupita kiwango
Hata maji safi, ukiyanywa kupita kiwango chake yana madhara pia kwa Afya ya binadamu.

Imeandikwa
" muwe na kiasi kwa kila jambo "
Kwahyo hata sigara inahitaji kiasi si ndio
 
Back
Top Bottom