Je! Kuvuta Sigara ni Dhambi?

Je! Kuvuta Sigara ni Dhambi?

Hakuna kitu inaitwa makuruhu kwenye quran na hadithi. Ukitaka kujua kitu ni halali au haram na ukakosa kwenye quran na hadithi basi unacho takiwa kufanya ni kupima hicho kitu kwa akili.

Kama faida ya hiyo kitu ni kubwa kuliko hasara basi hiyo kitu itakua ni halali.

Na hasara ya hiyo kitu ikiwa ni kubwa kuliko faida basi hiyo kitu itakua ni haram.

Kwa hiyo hasara ya sigara ni kubwa kuliko faida, kwa hiyo sigara ni haram.

Na sigara ina dhuru afya ya mtumiaji. na quraa inasema: {{Wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo.}} [Al-Baqarah, 2: 125]
Kwako
 
Siku zote mzalishaji anafaida ata kampuni ya computer inafaidi hivyo hilo sio tatizo kabisa, kama jambo linatafasiri nyingi wacha zisemwe ili kila mtu achague anapoona ni sahihi zaidi

Kulinganisha sigara na computer ni kupoteza muda. If computers were harmful to human health, governments all over the world, wangeweka tahadhari kwenye matumizi yake, just like they do for cigarettes!
 
Mkuu naomba nitofautiane na wewe. Kati Uislam sigara haipo kwenye uharamu. Sigara ipo kwenye MAKRUHU

Makruhu ni jambo ambalo ni bora au vizuri ukaliacha lakini utakapolifanya hupati dhambi

Asante sana mkuu kwa kuniquote. Nimejibu swali lako kwenye post hapa juu. Ila ningependa kuchukua fursa hii kwa kupongeza wewe for being a good human being! Ukotayari kusaidia watu humu bila masharti na ukipata hela zisozako, unazirudisha! Mungu akubariki sana, mkuu!
 
sigara ina dhuru afya ya mtumiaji. na andiko linasema {{Wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo.}} [Al-Baqarah, 2: 125]



Imesimuliwa na Ibn Mas'uud na Abu Barzah. Imepokewa na at-Tirmidhiy. Imesahihishwa na al-Albaaniy].

Na amesema:

((Yeyote anayekula sumu, akijiua mwenyewe kuwa hiyo (sumu), basi atakula sumu ndani ya moto wa jahannam, na itamuingia ndani ya tumbo lake daima na kuendelea milele.)) [Imesimuliwa na Jaabir. Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim]
 
Kwahyo hata sigara inahitaji kiasi si ndio
Kama itakuwa na japo manufaa kidogo.
Tueleze manufaa ya sigara ili tujifunze kwako.
Kuwa na kiasi ni kwa vile vitu vyenye umuhimu tu.
Kama kula chakula.
 
Mvutaji sigara anaingiza mwilini moshi ambao haumpatii shibe yoyote. Hili linafanana na tendo la watu wa Motoni wanaokula mimea inayochoma na isiyo na manufaa:

{{Hawatakuwa na chakula isipokuwa cha miba.}}

{{Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa.}} [Al-Ghaashiyah, 88: 6-7]
 
Before wakat nashabikia biblia nilikua najua kwamba pombe na sigara Ni dhambi ila nikaamua kukaa chini na kuisoma vizur nkaja kugundua kwamba hakuna kikuingiacho kinywan kinachosababisha dhambi Bali dhambi(unajisi) hutoka moyoni

Soma warumi 14 yote....na mwisho inasema ukifanya kitu pasipokua na imani hapo utakua umetenda dhambi

Hata yesu mwenyew amenukuliwa Mara nyingi akisistiza kwamba kikuingiacho mtu sio najisi Bali kikutokacho moyoni coz moyon hutoka mambo mabaya..

Hiyo Ni kwa uelewa wangu Mimi baada ya kuchambua kidogo
 
Uvutaji wa Sigara ni Dhambi kwakuwa.
1. Ni madawa ya kulevya
2. Haina faida yoyote kwa afya ya mwili wako.
3. Ina haribu Afya ya mwili wako uliotengenezwa kwa thamani kubwa sana.
4. Ina haribu Afya ya walio jirani yako.
5. Ina (adiction) inayokupelekea kudhohofisha akili yako ifikirie kuvuta sigara badala yawaza mambo ya maana.
6. Unakupotezea muda na kipato chako bila faida yoyote.
7. Ni Sumu kali unayokudhohofisha siku hadi siku, maisha ya wavuta sigara ni mafupi.
8. Inasababisha kushambuliwa na magonjwa hatarishi kama TB na Kansa
9. Inashawishi wengine kuiga tabia ya uvutaji ambayo haina faida yoyote.
10, Inakuchafua kwa harufu mbaya, uchafu na kuwa kero kwa mkeo na watu wa karibu yako.
NAKADHALIKA.
na wanaopika chakula kwa kutumia kuni na mikaa inayotoa moshi, je , moshi huo hauna shida kwao! ?
 
Kama itakuwa na japo manufaa kidogo.
Tueleze manufaa ya sigara ili tujifunze kwako.
Kuwa na kiasi ni kwa vile vitu vyenye umuhimu tu.
Kama kula chakula.
Kwa watumiaji inawaburudisha, inawafanya wajisikie free, inawapa kampani etc......inawapa furaha ya nafsi
 
sigara si dhambi ni karaha tu kama ambayo unakarahika mtu akibanja na kitema makohoz hadharani
 
Kulinganisha sigara na computer ni kupoteza muda. If computers were harmful to human health, governments all over the world, wangeweka tahadhari kwenye matumizi yake, just like they do for cigarettes!
Kwahiyo unakataa kuwa computer haina madhara au kipi unapinga? suala la tahadhari sio sababu inategemea serikali inanufaika vip na ilo suala, mbona serikali nyingine zimeruhusu ushoga lakini nyingine zimekataa , hapa Tunazungumzia kipimo gani kimetumika kufanya madhara ya sigara yawe dhambi lakini madhara ya computer ambayo ni cancer n.k isiwe dhambi ? jikite hapo
 
na wanaopika chakula kwa kutumia kuni na mikaa inayotoa moshi, je , moshi huo hauna shida kwao! ?

Cha kushangaza ni moshi ya kuni haina shida kwa binadamu. Zaidi zaidi inafanya macho yawe nyekundu, na pengine kuitwa mchawi! Lakini moshi ya sigara imejaa sumu ya kila aina - nicotine na toxic chemicals tele.
 
Back
Top Bottom