Je! Kuvuta Sigara ni Dhambi?

Ingawa Biblia haina orodha ya mazoea yote tunayopaswa kuepuka, ina kanuni zinazoweza kutusaidia kuelewa jinsi Yehova anavyohisi kuhusiana na mazoea hayo. Hataki tuvute sigara, kutumia kileo kupita kiasi, au kutumia dawa za kulevya. Ikiwa sisi ni rafiki za Mungu, tutaepuka kufanya mambo hayo. Kwa nini? Kwa sababu tunaheshimu sana zawadi ya uhai. Tabia kama hizo zinaweza kufupisha uhai wetu, kudhuru afya yetu, na kuwadhuru watu walio karibu nasi. Watu wengi hujaribu kuacha mazoea hayo ili walinde afya zao. Hata hivyo, tukiwa rafiki za Yehova, tunaacha mazoea hayo kwa sababu tunampenda. Mwanamke mmoja kijana alisema hivi: “Kwa msaada wa Yehova, nilisafisha maisha yangu na kuacha uraibu wangu. . . . Ninafikiri isingekuwa rahisi kwangu kufanya mabadiliko hayo kwa nguvu zangu mwenyewe.” Acheni tuzungumzie kanuni tano za Biblia ambazo zitamsaidia mtu kuacha mazoea yenye kudhuru.

“Wapendwa, kwa kuwa tuna ahadi hizi, acheni tujisafishe kila unajisi wa mwili na roho, tukiukamilisha utakatifu katika kumwogopa Mungu.” (2 Wakorintho 7:1) Yehova anataka tuwe huru kutokana na mazoea yasiyo safi ambayo yanaweza kuchafua akili au mwili wetu.

Sababu kuu ya ‘kujisafisha kila unajisi’ inaelezwa kwenye 2 Wakorintho 6:17, 18. Yehova anatuambia: “Mwache kugusa kitu kichafu.” Kisha anatuahidi hivi: “Nitawakaribisha ndani. Nami nitakuwa baba kwenu, nanyi mtakuwa wana na mabinti kwangu.” Naam, kama vile baba anavyowapenda watoto wake ndivyo Yehova atakavyotupenda ikiwa tutaepuka kitu chochote kinachoweza kutufanya tusiwe safi mbele zake.

“Lazima umpende Yehova Mungu wako kwamoyo wako wote na kwa nafsi yako yote na kwa akili yako yote.” (Mathayo 22:37) Hii ndiyo amri muhimu zaidi kuliko zote. (Mathayo 22:38) Yehova anastahili upendo wetu kamili. Tunawezaje kudai kwamba tunampenda kikamili ikiwa tunaamua kufanya jambo linaloweza kufupisha uhai wetu au kuharibu ubongo wetu? Badala yake, tunafanya chochote tunachoweza ili kuonyesha kwamba tunaheshimu uhai ambao ametupatia.

“[Yehova] huwapa watu wote uhai na pumzi na vitu vyote.” (Matendo 17:24, 25) Rafiki yako akikupa zawadi ya pekee, je, unaweza kuitupa au kuiharibu? Uhai ni zawadi ya pekee sana kutoka kwa Yehova. Tunaithamini sana zawadi hiyo. Kwa hiyo, tunataka kuutumia uhai wetu kwa njia ambayo itamletea utukufu.— Zaburi 36:9.

“Lazima umpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.” (Mathayo 22:39) Mazoea yasiyo safi hayatudhuru sisi tu. Yanaweza kuwadhuru watu wengine pia, na mara nyingi yanawadhuru watu tunaowapenda sana. Kwa mfano, mtu anayeishi na mvutaji wa sigaraanaweza kupata ugonjwa mbaya kwa sababu tu ya moshi wa sigara. Lakini tunapoacha mazoea hayo, tunawaonyesha watu walio karibu nasi kwamba tunawapenda.—1 Yohana 4:20, 21.

“Endelea kuwakumbusha wajitiishe na kuzitii serikali na mamlaka.” (Tito 3:1) Katika maeneo mengi ni kosa kisheria kutumia au kuwa na dawa za kulevya. Kwa kuwa Yehova anatuamuru tuheshimu serikali, tunatii sheria hizo.—Waroma 13:1.
 
Kiukweli sigara ni dhambi kwa sababu Neno la Mungu linasema kwamba;

Hamjui kuwa nyinyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu ambalo ndilo ninyi. (1Kor.3:16,17)

Sasa kama mimi na wewe ni mahekalu ya Roho mtakatifu; tutasalimikaje tujiharibu kwa sigara?

Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala nyinyi si Mali yenu wenyewe. (1Kor.6:19)

Kwa mafungu haya mawili, moja kwa moja uvutaji wa sigara ni uasi kama uasi mwingine.
Mkuu kidogo apo kwa (1kr3:16) najiuliza maswali mengi! Hivi kweli Paulo alimaanisha vyakula na vinywaji? Maana kila chakula mwilini kina side effect na vingine ni sumu kwa asili yake mfano mihogo.
Japo si mbobezi wa maandiko lakini apa probably Paulo aliwaonya wakolintho kutojitia najisi na kuaharibu miili yao kwa vitu vitatu Zinaa na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwenye Sanamu na nyama iliyosongolewa na damu! Maana ayo mambo matatu ndiyo msingi au Key points ambazo Paulo alipewa na balaza la wazee(Kanisa) chini ya Petro akiambiwa awasisitizie mataifa wajiepushe na ayo mambo matatu maana yanawatia unajisi (MATENDO 15:20)

Hitimisho
Kuharibu hekaru la bwana yaani mwili wako siyo kula au kunywa au kutoa viungo bali ni kuunajisi mwili wako maana roho ya Mungu haikai sehemu najisi na ayo mambo matatu ndiyo yanayokutia unajisi.
 
Ingawa Biblia haina orodha ya mazoea yote tunayopaswa kuepuka, ina kanuni zinazoweza kutusaidia kuelewa jinsi Yehova anavyohisi kuhusiana na mazoea hayo. Hataki tuvute sigara, kutumia kileo kupita kiasi, au kutumia dawa za kulevya. Ikiwa sisi ni rafiki za Mungu, tutaepuka kufanya mambo hayo. Kwa nini? Kwa sababu tunaheshimu sana zawadi ya uhai. Tabia kama hizo zinaweza kufupisha uhai wetu, kudhuru afya yetu, na kuwadhuru watu walio karibu nasi. Watu wengi hujaribu kuacha mazoea hayo ili walinde afya zao. Hata hivyo, tukiwa rafiki za Yehova, tunaacha mazoea hayo kwa sababu tunampenda. Mwanamke mmoja kijana alisema hivi: “Kwa msaada wa Yehova, nilisafisha maisha yangu na kuacha uraibu wangu. . . . Ninafikiri isingekuwa rahisi kwangu kufanya mabadiliko hayo kwa nguvu zangu mwenyewe.” Acheni tuzungumzie kanuni tano za Biblia ambazo zitamsaidia mtu kuacha mazoea yenye kudhuru.

“Wapendwa, kwa kuwa tuna ahadi hizi, acheni tujisafishe kila unajisi wa mwili na roho, tukiukamilisha utakatifu katika kumwogopa Mungu.” (2 Wakorintho 7:1) Yehova anataka tuwe huru kutokana na mazoea yasiyo safi ambayo yanaweza kuchafua akili au mwili wetu.

Sababu kuu ya ‘kujisafisha kila unajisi’ inaelezwa kwenye 2 Wakorintho 6:17, 18. Yehova anatuambia: “Mwache kugusa kitu kichafu.” Kisha anatuahidi hivi: “Nitawakaribisha ndani. Nami nitakuwa baba kwenu, nanyi mtakuwa wana na mabinti kwangu.” Naam, kama vile baba anavyowapenda watoto wake ndivyo Yehova atakavyotupenda ikiwa tutaepuka kitu chochote kinachoweza kutufanya tusiwe safi mbele zake.

“Lazima umpende Yehova Mungu wako kwamoyo wako wote na kwa nafsi yako yote na kwa akili yako yote.” (Mathayo 22:37) Hii ndiyo amri muhimu zaidi kuliko zote. (Mathayo 22:38) Yehova anastahili upendo wetu kamili. Tunawezaje kudai kwamba tunampenda kikamili ikiwa tunaamua kufanya jambo linaloweza kufupisha uhai wetu au kuharibu ubongo wetu? Badala yake, tunafanya chochote tunachoweza ili kuonyesha kwamba tunaheshimu uhai ambao ametupatia.

“[Yehova] huwapa watu wote uhai na pumzi na vitu vyote.” (Matendo 17:24, 25) Rafiki yako akikupa zawadi ya pekee, je, unaweza kuitupa au kuiharibu? Uhai ni zawadi ya pekee sana kutoka kwa Yehova. Tunaithamini sana zawadi hiyo. Kwa hiyo, tunataka kuutumia uhai wetu kwa njia ambayo itamletea utukufu.— Zaburi 36:9.

“Lazima umpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.” (Mathayo 22:39) Mazoea yasiyo safi hayatudhuru sisi tu. Yanaweza kuwadhuru watu wengine pia, na mara nyingi yanawadhuru watu tunaowapenda sana. Kwa mfano, mtu anayeishi na mvutaji wa sigaraanaweza kupata ugonjwa mbaya kwa sababu tu ya moshi wa sigara. Lakini tunapoacha mazoea hayo, tunawaonyesha watu walio karibu nasi kwamba tunawapenda.—1 Yohana 4:20, 21.

“Endelea kuwakumbusha wajitiishe na kuzitii serikali na mamlaka.” (Tito 3:1) Katika maeneo mengi ni kosa kisheria kutumia au kuwa na dawa za kulevya. Kwa kuwa Yehova anatuamuru tuheshimu serikali, tunatii sheria hizo.—Waroma 13:1.
Mkuu Mhusika mkuu, kama nitakua nimeelewa vizuri mafafanuzi yako ni kuwa sababu ya uvutaji wa sigara kuwa dhambi ni matokeo au athari zinazojitokeza kwa sababu ya uvutaji sigara ambayo ni uharibifu wa organ muhimu ktk mwili na hatimaye kupelekea kifo na hii ndiyo inaifanya sigara kuwa Haram, ingawa pia kuna vyakula au vinywaji ambavyo pia vinaweza kuwa na matokea mabaya kiafya kama mtu atakuwa addicted kwavyo, hapa sizungumzii kula hadi kuvimbiwa (maana huu ni ulafi ambao Biblia imeuzungumzia) bali "ADDICTION YA VYAKULA AU VINYWAJI".

Sasa je hii nayo ni dhambi? Naamini kama mtu atakua na "kiasi" katika matumizi ya vyakula/vinywaji hivyo naamini hatakua ktk risk ya kupata madhara kiafya, sasa je, inawezekana mtu akawa anavuta kwa kiasi ktk level ambayo haiwezi kumletea madhara kiafya, kama inawezekana je, bado atakua anatenda dhambi?

Pia kuna hizi Electronic Cigarette, ambazo inasemekana madhara yake kwa afya ya binadamu ni ya chini sana sana kulinganisha na Tobacco Cigarette, je mtu akivuta hizi naye anatenda dhambi?
 
Asante sana mkuu kwa kuniquote. Nimejibu swali lako kwenye post hapa juu. Ila ningependa kuchukua fursa hii kwa kupongeza wewe for being a good human being! Ukotayari kusaidia watu humu bila masharti na ukipata hela zisozako, unazirudisha! Mungu akubariki sana, mkuu!
Aamin, hahahaaa mkuu umenichekesha sana lakini. Thanks for the compliment
 
kama kuvuta sigara ni dhambi tupen na ushahid bas ili tuweze kwamin ila hiv hiv tu inakuwa ngum wakuuuu!!!!
 
Computer ina toa radiation ambazo kiafya ya binadamu haifai , wamejaribu kupunguza kiwango chake lakini hawakuweza kuondoa yote , madhara ya zile radiation ni kama ifuatavyo
1.Cancer
2.Miscarriage
3.Birth defects
Wataalamu wanashauri ili kupunguza madhara kuna njia mbili
1.Kupunguza muda wa kuitumia
2.kuweka mbali wakati unaitumia

Hitimisho :hakuna asiejua ubaya wa cancer mkuu nakushauri acha computer ni dhambi
Dah
 
Uvutaji wa Sigara ni Dhambi kwakuwa.
1. Ni madawa ya kulevya
2. Haina faida yoyote kwa afya ya mwili wako.
3. Ina haribu Afya ya mwili wako uliotengenezwa kwa thamani kubwa sana.
4. Ina haribu Afya ya walio jirani yako.
5. Ina (adiction) inayokupelekea kudhohofisha akili yako ifikirie kuvuta sigara badala yawaza mambo ya maana.
6. Unakupotezea muda na kipato chako bila faida yoyote.
7. Ni Sumu kali unayokudhohofisha siku hadi siku, maisha ya wavuta sigara ni mafupi.
8. Inasababisha kushambuliwa na magonjwa hatarishi kama TB na Kansa
9. Inashawishi wengine kuiga tabia ya uvutaji ambayo haina faida yoyote.
10, Inakuchafua kwa harufu mbaya, uchafu na kuwa kero kwa mkeo na watu wa karibu yako.
NAKADHALIKA.
Mkuu hata soda ina madhara,nayo je Ni dhambi?
 
Dhambi ni

1. Kufanya jambo lisilompendeza Mwenyezi Mungu.

2.Kufanya jambo ambalo lina hatarisha hali yako au ya jirani yako.
Yaani jambo lisilokupendeza wewe au Jirani yako.
Usinywe soda ,usitumie mifuko ya plastic, usitumie chakula chochote chenye added chemicals ..

Maana kwa definition yako no 2 vyote vitakuwa dhambi
 
sigara si dhambi ni karaha tu kama ambayo unakarahika mtu akibanja na kitema makohoz hadharani
Ni karaha tu kama kelele za spika ya msikiti au kanisa inavyokera mtu aliyepumzika kitandani kwake! Wakati usingizi umekolea mara unasikia Pu pu pu pu!mhadhini anapotest mitambo yake!!
 
Binafsi sivuti feg ila napenda harufu yake, nadhan ungeifuta namba 10, kisha watu wa dini tusome biblia kitabu cha Mwanzo 1 kuna mistari inahalalisha matumizi ya majani kama dawa na matunda kama chakula na chakula cha kila mnyama.

Je kula Nguruwe ngamia sungura kambare na kuvuta feg ipi ni dhambi?? Tutumie maandiko ili tuelewane maana Bible is perfect book.
Kunamstari unasema ole wao wageuzao pua zao matanuru ya moshi
 
Hakuna kitu inaitwa makuruhu kwenye quran na hadithi. Ukitaka kujua kitu ni halali au haram na ukakosa kwenye quran na hadithi basi unacho takiwa kufanya ni kupima hicho kitu kwa akili.

Kama faida ya hiyo kitu ni kubwa kuliko hasara basi hiyo kitu itakua ni halali.

Na hasara ya hiyo kitu ikiwa ni kubwa kuliko faida basi hiyo kitu itakua ni haram.

Kwa hiyo hasara ya sigara ni kubwa kuliko faida, kwa hiyo sigara ni haram.

Na sigara ina dhuru afya ya mtumiaji. na quran inasema:
{{Wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo.}} [Al-Baqarah, 2: 125]
Al bakhara kiarabu, kiswahili sura ya ng'ombe jike. Nimekumbuka Miahadhara ya akina Simba Ulanga, Biblia ni Jibu, Mazinge, Magenzi na Yohana ( Yahya) kipindi cha miaka ya tisini
 
Al bakhara kiarabu, kiswahili sura ya ng'ombe jike. Nimekumbuka Miahadhara ya akina Simba Ulanga, Biblia ni Jibu, Mazinge, Magenzi na Yohana ( Yahya) kipindi cha miaka ya tisini

Inaitwa Suuratu Albaqarah. Na sio Al nabakhara. Simba ulanga kakudanganya ye mwenyewe hajui njaa tu inamsumbua.
 
Al bakhara kiarabu, kiswahili sura ya ng'ombe jike. Nimekumbuka Miahadhara ya akina Simba Ulanga, Biblia ni Jibu, Mazinge, Magenzi na Yohana ( Yahya) kipindi cha miaka ya tisini
Simbaulanga namsikia Sana ila sijawahi kuona mhadhara wake,Kuna video zake mitandaoni?
 
Kwa sisi waislamu, uvutaji sigara ni haramu, kwa hiyo ni dhambi, ingawa watu watajitokeza kupinga. Ni tabia mbaya sana ambayo inachafua mazingira na ni ishara ya maporomoko ya maadili. Karibu kote duniani, uvutaji sigara hadharani imepigwa marufuku. Nairobi wavutaji sigara wametengewa maeneo maalum vya kuvuta sigara, kuvuta barabarani ni kosa! Hapa kwetu mbona bado haijapigwa marufuku?
Kwetu sio dhambi usidanganye jamii,Sigara ni Makuruhu
 
HUKUMU YA KUVUTA NA KUUZA SIGARA KATIKA UISLAMU

FATWA YA SHEIKH ABDUL-AZIZ BIN BAAZ RAHIMAHULLAH.

Ameulizwa Sheikh Bin Baaz RahimahuLlah .

" Nini hukumu ya kuvuta Sigara, je, ni Haramu au Makuruhu na nini Hukumu ya kuuza na kuifanyia Biashara.?"

JAWABU:

" Sigara imeharamishwa kwa sababu yenyewe ni jambo Khabithi (Baya) na imebeba Madhara mengi, na Allah Subhaanahu wa Ta'ala amehalalisha kwa waja wake Attwayyibaat,
(vitu vizuri zuri)
katika Vyakula na Vinywaji na vinginevyo na amewaharamishia Alkhabaaith,
(vitu vibaya )

Amesema Allah Subhaanahu wa Ta'ala:

"Wanakuuliza ni kitu gani walichohalalishiwa ? Waambie, Mmehalalishiwa Attwayyibaatu"
( vizuri zuri ) . ( Almaaidah / 4 )

Na amesema: Katika kumsifia Nabii wake Muhammad ((Swalla Allahu alayhi wa Sallam))

katika Sura ya
Al aaraaf: Aya 57 :

"Anawaamrisha Mema na kuwakataza maovu na anawahalalishia , ( yaliyo mazuri ) na anawaharamishia Alkhabaaith"
( yaliyo mabaya ) .

Sigara katika aina zake zote si katika Attwayyibaati
(mambo mazuri ) bali ni katika Alkhabaaith
(mambo mabaya ) hivyo hivyo vilevya vyote ni katika Alkhabaaith,
(vitu vibaya )

Na Sigara haijuzu kuivuta wala kuinunua wala kuifanyia Biashara ilivyokuwa na Madhara makubwa na Miisho mibaya .

Ni Wajibu kwa yule aliekuwa anavuta kukimbilia kufanya Toba na kurejea kwa Allah Subhaanahu wa Ta'ala
na Kujuta kwa yale yaliyopita na kuazimia kutorudia hilo na mwenye kutubia kikweli kweli
Allah atamsamehe .

Kama alivyosema Azza wa Jallaa:

"Tubieni kwa Allah nyote nyinyi Waumini huenda mkafaulu" ( Annuur / 31 )
(

Na amesema Allah Subhaanahuu wa Ta’ala:

"Kwa hakika mimi ni mwenye kumsamehe mwenye Kutubia na Akaamini na kutenda matendo mema kisha akaongoka" ( Twaha / 82 ).

Na amesema Nabii ((Swallallahu alayhi wa Sallam))

"Toba inafuta yale yote yaliyopita"

Naam na amesema Mtume ((Swallallahu alayhi wa Sallam)) :

"Mwenye kutubia kutokana na dhambi
(aliyoifanya) ni kama yule ambae hana dhambi"

Twamuomba Allah atengeneze hali za Waislamu na awakinge na kila lenye kukhalifu Sheria yake , hakika yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kujibu "

Chimbuko :
حكم شرب الدخان وبيعه والاتجار به

حكم شرب الدخان وبيعه والاتجار به

السؤال :

" ما حكم شرب الدخان؟ وهل هو حرام أم مكروه؟ وما حكم بيعه والاتجار فيه؟

الجواب :

" الدخان محرم لكونه خبيثا ومشتملا على أضرار كثيرة والله سبحانه وتعالى إنما .أباح لعباده الطيبات من المطاعم والمشارب وغيرها وحرم عليهم الخبائث.
قال سبحانه وتعالى: يَسْأَلُونَكَ مَاذَا أُحِلَّ لَهُمْ قُلْ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ[1]، وقال سبحانه في وصف نبيه محمد صلى الله عليه وسلم في سورة الأعراف: يَأْمُرُهُمْ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَاهُمْ عَنِ الْمُنْكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ[2]، والدخان بأنواعه كلها ليس من الطيبات بل هو من الخبائث وهكذا جميع المسكرات كلها من الخبائث، والدخان لا يجوز شربه ولا بيعه ولا التجارة فيه لما في ذلك من المضار العظيمة والعواقب الوخيمة.
والواجب على من كان يشربه أو يتجر فيه البدار بالتوبة والإنابة إلى الله سبحانه وتعالى، والندم على ما مضى والعزم على ألا يعود في ذلك، ومن تاب صادقا تاب الله عليه كما قال عز وجل: وَتُوبُوا إِلَى اللَّهِ جَمِيعًا أَيُّهَا الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ[3]، وقال سبحانه: وَإِنِّي لَغَفَّارٌ لِمَنْ تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا ثُمَّ اهْتَدَى[4]، وقال النبي صلى الله عليه وسلم: التوبة تجب ما كان قبلها، وقال عليه الصلاة والسلام: التائب من الذنب كمن لا ذنب له.
ونسأل الله أن يصلح حال المسلمين وأن يعيذهم من كل ما يخالف شرعه إنه سميع مجيب.

[1] سورة المائدة الآية 4.
[2] سورة الأعراف الآية 157.
[3] سورة النور الآية 31.
[4] سورة طه الآية 82.

المصدر :

حكم شرب الدخان وبيعه والاتجار به

Usilichafue hekalu la Mungu wako na mwili wako ni hekalu la bwana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom