Je, kuna umuhimu mume/mwanaume kumuachia mwanamke usukani wa gari? safari zote mwanamke afanye?

tupe ambazo sio outdated basi..kwa sabbu wewe inaonesha much know sana
Usichukie ukiambiwa ukweli
Kule UAE mwana mfalme MBS alipo pewa tu utawala aliruhusu wanawake ku drive na MBS alisema kuzuiaa mwanamke kuendesha gari ktk karne hii ni OUT DATED
 
Yaan hapo inakuuma kaka ako kampa mkewe gari yeye akitumia public transport ndugu wa mume mna sheeeder sana nyie
 
Kwenye barabara ya vumbi spidi 100 uongo huo tena road ya mtaani.. Labda rough road zile za vijijini ambazo ni barabara kuu.
 
Mkuu hapo kwenye "kuvurugwa tumbo" umenifanya nicheke sanaa aisee.

Ila rough road nyingine zipo vizuri utadhani ni mkeka
Zipo fresh lakini kwa gari la kawaida mkuu kama alivyotaja dada hapo binafsi naona lazima utumbo ukorogwe...

Hapa nafanya assumption gari la kawaida ni kama kina Spacio, IST, RunX, Wish, Isis na ndugu zao wote (yaani yale magari ambayo yameundwa kupita kwenye lami)...

Ila kuna gari kama Kilimo kwanza, Harrier, Pickup 4x4 yoyote, Landrover, Mkonge na ndugu zao wote hao wakubwa wakubwa, sasa hizi mimi naziona sio za kawaida kwa sababu zimeundwa kuvumilia shurba
 
..tukiwa na safari za kifamilia namuachia mama usukani kwasababu nikiendesha mimi malalamiko yanakua mengi kuwa naendesha kwa spidi kubwa.
 
Ok..

Ila pole nahisi hukunielewa nilichokuwa maanisha

Ipo hivi mimi sipendi kutembea na gari hovyo hovyo...hivyo natamani kama ikiwezekana ninunue nimpe mke awe ananiendesha kabisa.

Kwa sabbu hata maofisini kuna kufuatiliana sasa nikauliza ni zipi faida na hasara?

Usifanye hilo kosa Mkuu.

Nunua gari kwa maana ya unajinunulia mwenyewe kwa ajili ya matumizi yako na ya familia.

Ila usinunue kwa kusema eti unamkabidhi mkeo ndo awe analiendesha.

Weka tu utaratibu ambao uko open, kwamba gari unaendesha wewe, ikitokea wife anahitaji kutoka na gari lipo anatakiwa kukuuliza kama anaweza kulitumia au la.

Na mnapotoka wote yeyote aendeshe kutegemea na mazingira.

Usifanye kosa la kutamka eti nimekununulia gari hili hapa uwe unaendesha, labda tu kama uko vizuri na unaweza kununua yako na yake.
 
Kwenye lami sawa...ila kwa rough roads unaua gari dada...na hata mtu akipanda kwa spidi hiyo anaweza vurugwa tumbo
Kama anaendesha haya ma V8 hawezi kuusikia mtikisiko wa nje! Lakini Kama ni Passo akifika mwisho wa safari lazima akimbilie chooni kushusha Mzigo!!
 
Ktk karne hii kuja na mada kama izi nahisi ni kuwa out dated
Kuna watu wengine Magari ndiyo wameanza kuyamiliki Sasa hivi! Ndiyo maana wakimuona Mwanamke anaendesha hata Basi la Mwendokasi wao ni full kushangaa kisa Mwanamke anaendesha gari!!
 
Sehem ambazo zimepita sgr kumetengenezwa barabara nzuri sana ...haina mabonde mkuu imenyooka safi...sisi tulikoswa koswa na bomoa bomoa ya mwendokasi..tuna barabara nzuri sana siwez kwenda taratib hata kdg...
Pamoja na kupenda kwako kuendesha gari kwa speed,bado unatakiwa uzingatie Sheria za barabarani! Siyo mradi umekuta barabara imenyooka na wwe unakandamiza mguu kwa kibati,kuna sehemu zingine kuna makazi ya Watu,unatakiwa upite taratibu hata Kama hakuna kibao Cha speed limit!!
 
Pamoja na kupenda kwako kuendesha gari kwa speed,bado unatakiwa uzingatie Sheria za barabarani! Siyo mradi umekuta barabara imenyooka na wwe unakandamiza mguu kwa kibati,kuna sehemu zingine kuna makazi ya Watu,unatakiwa upite taratibu hata Kama hakuna kibao Cha speed limit!!
😁😁naona limewauma...jaman kipande chenyewe toka hom had road ni 8min..nikifika road unaendeshaje 100 barabara zimejaa gar ..ni.kipande kiduchu mno...point yang sipend kuendesya slow...sijawah pata ajali....s8jawah koswakoswa ajali..niko makini kuliko udhaniavyo wewe ...
 
Mwenzangu anaendaga na 20...mie 100 barabara ya vumbi..bas anamind balaa...sizidi 100...
Upo vizuri.

100 ni speed ya kati na ya kistaarabu pia, haiboi dereva, haiboi abiria na haiboi watumiaji wengine wa barabara, haisababishi ajali za 'overspeed' na humfanya dereva awe makini.

Mwendo mdogo wa kobe barabarani hausaidii kupunguza ajali bali husaidia kuleta ajali kwako na kwa wengine.

Maana unapotembea kikonokono, huleta hamu kwa walioko nyuma yako ya ku overtake kusikokuwa na ulazima kunakoweza kusababisha ajali.
 
Back
Top Bottom