Zinduna
JF-Expert Member
- Nov 6, 2011
- 2,378
- 3,379
Naamini mwanamke awaye yeyote ambaye bado anaziona siku zake anajua maumivu ya tumbo, hisia na msongo wa mawazo anaopitia wakati anapokuwa kwenye siku zake. wako wengine hulazimika kulala kitandani wakiwa hoi bin taaban wakati wanapozitumikia siku zao achilia mbali kisirani wanachokuwa nacho na mambo mengine yanayofanana na hayo.
Je kuna haja sasa ya sheria za kazi kuweka kipengele kitakachowapa nafasi wanawake waajiriwa ya kupumzika japo kwa siku mbili tu wakati wanapokuwa kwenye siku zao?
Naamini wengi mnajua ni kiasi gani hata ufanisi wa kazi kwa mwanamke aliye katika siku zake unavyopungua achilia mbali kisirani kinachoweza kujitokeza na kusababisha kutoelewana na aidha wafanyakazi wenzie au wateja pindi mwanamke aliye katika siku zake anapokuwa kazini.
Kwa mfano kule Japan hapo mnamo mwaka 1947 baada ya vita kuu ya pili ya dunia walipitisha sheria mpya ya kazi inayoitwa Menstrual Leave Policy. Sheria hiyo inawapa wanawake wanaoingia katika siku zao mapumziko ya siku mbili kutokana na maumivu wanayoyapata wakiwa katika siku zao ambapo kwa Kijapana wanaita Seirikyuuka (Physiological Leave). Mara baada ya sheria hiyo kutungwa na kupitishwa, ilisababisha wimbi kubwa la wanawake nchini Japan kuingia katika mfumo wa ajira nchini humo na hivyo kuongeza nguvu kazi na pato la taifa hilo kuongezeka mara dufu.
Najua wapo baadhi ya wanawake wenzangu wanaweza wasiunge mkono hoja yangu kwa hofu kwamba jambo hili linaweza kusababisha kuongezeka kwa unyanyasaji wa kijinsi kwa wanawake na pia kuwafanya waajiri kukwepa kuwaajiri wanawake kwa kuwaona kama ni mizigo na ni dhaifu.
Tukumbuke tu kwamba swala la kubeba mimba na likizo ya uzazi bado ni mtihani mkubwa sana kwa wanawake waajiriwa, ingawa swala la uzazi ni muhimu kwa ustawi wa taifa lolote duniani kwa sababu ni kitendo cha kuzalisha nguvu kazi mpya lakini bado mpaka sasa kuna baadhi ya waajiri wanakwazwa na swala la wanafanyakazi wa kike kubeba mimba.
Sasa je swala la likizo japo ya siku mbili kwa wanawake wanapokuwa kwenye siku zao watalipokeaje?
Mchango wenu tafadhali
snowhite, King'asti, BADILI TABIA, AshaDii, Lady doctor, ladyfurahia, Preta, Fixed Point, Kongosho, Nivea, Neylu, Lisa, miss neddy, miss chagga, Mamndenyi, Tina, Ennie, charminglady, Asnam, MankaM, Munkari, lara 1, Heaven on Earth, cacico, miss strong, a.rahabu, gfsonwin, afrodenzi, Husninyo, Karucee