Je kuna haja ya wanawake waajiriwa kupewa mapumziko wakiwa kwenye siku zao?

haja ipo kwa kweli maana yale ni maumivu haswa.....kuna watu tuliambiwa tukishajifungua yataisha aah wapi mwendo ule ule tu
 
Sidhani kama ni sawa kwa sababu.

1. Kuna wanawake wengi ambao hawapati shida hii, (si wanawake wote wenye kusumbuliwa na maumivu wakati wa hedhi.)

2. Kuna dawa nyingi zinazoweza kutumiwa endapo mwanamke anapokuwa katika siku zake za hedhi..ba kumfanya aendelee na takribani shughuli zake za kila siku.

3. Si wanawake wote wenye mizunguko sawa, nikimaanisha kuwa baadhi huweza kuingia hedhi mara moja, mara mbili na wengine hata mara tatu, hivyo wapo watakao-claim siku zaidi.

4. Hypothetically, speaking..endapo tukikubali, hii itajumuisha viongozi wa serikali, ..na endapo kwa mfano viongozi wakuu wa nchi watakuwa ni wakike na coincidentally, wako katika siku zao nchi itakuwa katika wakati mgumu.

5. Itakuwa ni upenyo wa watu kufanya shughuli binafsi(pengine zisizo na tija) kwani si rahisi kutambua endapo mwanamke yuko katika siku zake, mf. akikudanganya, utahakikishaje? kwa kumchungulia?


6. Kwanini ziwe siku mbili, wapo wenye kuwa hedhi kwa siku nyingi kuliko wengine, je hawa watapaswa waongezewe siku zaidi.

Shukrani sana mkuu kwa ufafanuzi, ni kweli hata mie ni mmojawapo wa wasio pata maumivu yeyote wakati wa hedhi. Sasa nakuuliza je nitakuwa na tatizo au niko sawa. ..

Pia pitia jukwaa la Doctor kuna ushauri unahitajika!!
 
Hili Jambo gumu kidogo kumeza....

Ukweli ni kwamba wapo ambao huwa wanaumwa hata ukimwambia aje kazini kwa kweli utakuwa unamwonea, I remember kuna kipindi girlfriend wangu aliacha kufanya final chuo kwa sababu ya haya maumivu.

Tatizo linakuja hapa, kila mwanamke ana experience zake ha hivi vitu, wengine hawaumwi kabisa, wengine ni siku 5 kalala ndani, unapotengeneza sheria/utaratibu lazima uwe na vigezo. Mtatumia vigezo gani? Tunaweza tukaweka siku X za kupumzika, kumbe kuna wengine wanahitaji X+3 days. Halafu huku kupumzika kutakuwa ni generic kwamba kila mwanamke akiwa period apumzike au itakuwa wale tu ambao wanaumwa which brings another question, je wavivu hawatatumia periods kujiongezea likizo?

Ni idea nzuri ila implementation yake naona ngumu kidogo, siku 2/month = approx 24/year, kwenye mfumo wetu wa kibepari nani atakae kubali mfanyakazi wake apumzike 24[period leave] + 28[Work leave] = 52 leave days in a year. Ngumu kumeza.

Point ya mwisho pia ni privacy, haya mambo ni ya siri, ni wanawake wangapi watakuwa comfortable na hili swala, I mean usipomwona Zinduna jumatatu na jumanne means yupo kwenye periods, it might be awkward kwa wengine.

Tuyaache tu kama yalivyo, ila tu kuwe na urahisi na uelewa kwamba wenzetu wakiwa katika hicho kipindi wakisema wanaenda kupumzika, tuwaelewe.
 
hahaha, yaani mie nilishajijua kabisaa, naanza kutoa disclaimer 'nna kisirani leo!' ili ukiona nalalama ujue kabisaa ndo yalee na usijibu.
mie napinga likizo. hivi ukiwa na kisirani na ukakaa kutwa nyumbani ikifika saa kumi si unaanza kuuliza uko wapi, unarudi saa ngapi, mbona umechelewa? dawa yake ni kuwa busy tu kama kichaa
Na hicho kisirani mnakuwaga nacho kwelikweli....Kama mimi siku za mwanzoni na my wife nilikuwa najua kabisa "Kugombana bila sababu days" are coming soon. Hata ikafikia muda hizo days zikifika hatujuani mpaka zikipita. Sasa hivi nimezoea ila kuna Visirani next levo inabidi tu kujihami.

NAUNGA MKONO HOJA ndugu mleta UZI
 
.



Point ya mwisho pia ni privacy, haya mambo ni ya siri, ni wanawake wangapi watakuwa comfortable na hili swala, I mean usipomwona Zinduna jumatatu na jumanne means yupo kwenye periods, it might be awkward kwa wengine.

Tuyaache tu kama yalivyo, ila tu kuwe na urahisi na uelewa kwamba wenzetu wakiwa katika hicho kipindi wakisema wanaenda kupumzika, tuwaelewe.

Hapo hata mimi pananipa shida....na kuna mijanaume mingine hainaga adabu...kesho ukienda job itaanza kukutania
 
Na ndiyo maana nawashangaa wanaume wanaowalalamikia wanawake wanaotoa huduma kwa wateja pale wanapopewa maneno mbofu mbofu, yaani hawaelewi tu sababu....!

Tupewe tu likizo tujipumzikie zetu mambo yakishaharibika.

Kumbeee, kweli kitanda usichokilalia hujui kunguni wake.
 
Yale maumivu achana nayo,ila mie nikilala huwa naona kama yanazidi bora niwe active.
Nakerwa tu na kubadili pads mara kwa mara kwenye public toilets na hasa nikiwa na kazi za nje ya ofisi!!
Hicho kisirani huwa si kila mwezi ila nikimu attend mtu wakati ninacho ataona rangi zote!!!
Unaingia ofcn umekunja uso hata salamu unaitolea kwenye meno kama hutaki,nikwaze kwa bahti mbaya nikutangaze makusudi!!!!!
Uanamke kweli kazi!!!!
 
Back
Top Bottom