Je kuna haja ya wanawake waajiriwa kupewa mapumziko wakiwa kwenye siku zao?

ha ha mkuu sipati picha!! Lazima wapinge!!
Lakini lazima wakubali kutoa likizo kama sheria itapitishwa.
na hapo ndipo utakapoona wanawake watakavyoajiriwa kwa idadi maalum kwa hofu ya likizo za period
 
ni kweli na sisi wanaume tupewe siku za kupumzika tukiwa tumegegeda mwanamke maana huwa tunachoka sana kama leo nimekuja kazini basi tu ikiwezekana tulipwe hela tu tusifanye kazi

kuchoka ni tofauti na kuumwa jameni...!!!! mbona hata wanawake huwa wanachoka

Dah kwa hiyo watu wakipeana mambo kesho yake tuwape likizo? Kuna wengine watakuwa hawaji kazini kabisa!
 
Okota maganda
Peleka Uganda
Yamepanda bei
Sukuma, waaaaaaaaaaaaaa

Posa subiri subiri kidogo

Nipo hoi taabani, moyo kwako umetua,
Nitakuwa furahani, wewe kinikubalia,
Nimekuweka moyoni, uniweke nawe pia,
Nimeshindwa vumilia, kutosema nakupenda.

Chonde chonde muhashamu, nifanye moyo tulia,
Nikupe pendo adhimu, pekee hii dunia,
Pendo liso na awamu, kila siku lachanua,
Nimeshindwa vumilia, kutosema nakupenda.

Nikupe pendo la huba, pendo nalosisimua,
Pendo tele na si haba, moyoni ‘shakujazia,
Pendo mara saba saba, mahaba yalozidia,
Nimeshindwa vumilia, kutosema nakupenda.
 
Da Zinduna, mie sijui ni bahati au ugonjwa yaan huwa siumwi na sina dalili nisipokuwa makini tu naharibu pozi la siku!

Sasa sifahamu kama niko sawa au la...
 
Last edited by a moderator:
Nipo hoi taabani, moyo kwako umetua,
Nitakuwa furahani, wewe kinikubalia,
Nimekuweka moyoni, uniweke nawe pia,
Nimeshindwa vumilia, kutosema nakupenda.

Chonde chonde muhashamu, nifanye moyo tulia,
Nikupe pendo adhimu, pekee hii dunia,
Pendo liso na awamu, kila siku lachanua,
Nimeshindwa vumilia, kutosema nakupenda.

Nikupe pendo la huba, pendo nalosisimua,
Pendo tele na si haba, moyoni ‘shakujazia,
Pendo mara saba saba, mahaba yalozidia,
Nimeshindwa vumilia, kutosema nakupenda.

Wasikutishe wahepe
Akili wasikutibue
Wanaoleta sekeseke
Waambie bibi wakutue

Utapewa maneno na wapekepeke
Ukose raha usichangamke
Wasiwasi wako pembeni uweke
Mi ndo wako n'takufanya ucheke
 
Ulichokisema kinaweza kuwa sahihi lakini sio kwa wachumi

Kila mwezi huyu atakuwa ana siku mbili za kupumzika kwa mwaka ana siku 24,na kama atajifungua huo mwaka siku za kupumzika zitakuwa 114,hiyo ni karibu miezi mi 4 ambayo mwanamke huyo hatafanya kazi kabisa

Hii inamaana kuwa atalipwa mshahara wa miezi hiyo bure,yaani bila kufanya kazi,kwa sehemu anayofanya kazi hii ni hasara kwasababu hajatumikia ujira wake

Lakini ni hasara kwa taifa kwakuwa hatakuwa amelitumikia ipasavyo

Hebu fikiri ni wanawake wangapi wapo kwenye ajira sasa hivi na jaribu kufikiria tu ni hasara kiasi gani taifa litapata kutokana na hii kitu

Na hili litawapanguvu sana wale wanaopinga wanawake kufanya kazi!
 
Sidhani kama ni sawa kwa sababu.

1. Kuna wanawake wengi ambao hawapati shida hii, (si wanawake wote wenye kusumbuliwa na maumivu wakati wa hedhi.)

2. Kuna dawa nyingi zinazoweza kutumiwa endapo mwanamke anapokuwa katika siku zake za hedhi..ba kumfanya aendelee na takribani shughuli zake za kila siku.

3. Si wanawake wote wenye mizunguko sawa, nikimaanisha kuwa baadhi huweza kuingia hedhi mara moja, mara mbili na wengine hata mara tatu, hivyo wapo watakao-claim siku zaidi.

4. Hypothetically, speaking..endapo tukikubali, hii itajumuisha viongozi wa serikali, ..na endapo kwa mfano viongozi wakuu wa nchi watakuwa ni wakike na coincidentally, wako katika siku zao nchi itakuwa katika wakati mgumu.

5. Itakuwa ni upenyo wa watu kufanya shughuli binafsi(pengine zisizo na tija) kwani si rahisi kutambua endapo mwanamke yuko katika siku zake, mf. akikudanganya, utahakikishaje? kwa kumchungulia?


6. Kwanini ziwe siku mbili, wapo wenye kuwa hedhi kwa siku nyingi kuliko wengine, je hawa watapaswa waongezewe siku zaidi.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom