Je kuna haja ya wanawake waajiriwa kupewa mapumziko wakiwa kwenye siku zao?

Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,378
3,379
period.jpg

Naamini mwanamke awaye yeyote ambaye bado anaziona siku zake anajua maumivu ya tumbo, hisia na msongo wa mawazo anaopitia wakati anapokuwa kwenye siku zake. wako wengine hulazimika kulala kitandani wakiwa hoi bin taaban wakati wanapozitumikia siku zao achilia mbali kisirani wanachokuwa nacho na mambo mengine yanayofanana na hayo.

Je kuna haja sasa ya sheria za kazi kuweka kipengele kitakachowapa nafasi wanawake waajiriwa ya kupumzika japo kwa siku mbili tu wakati wanapokuwa kwenye siku zao?

Naamini wengi mnajua ni kiasi gani hata ufanisi wa kazi kwa mwanamke aliye katika siku zake unavyopungua achilia mbali kisirani kinachoweza kujitokeza na kusababisha kutoelewana na aidha wafanyakazi wenzie au wateja pindi mwanamke aliye katika siku zake anapokuwa kazini.

Kwa mfano kule Japan hapo mnamo mwaka 1947 baada ya vita kuu ya pili ya dunia walipitisha sheria mpya ya kazi inayoitwa Menstrual Leave Policy. Sheria hiyo inawapa wanawake wanaoingia katika siku zao mapumziko ya siku mbili kutokana na maumivu wanayoyapata wakiwa katika siku zao ambapo kwa Kijapana wanaita Seirikyuuka (Physiological Leave). Mara baada ya sheria hiyo kutungwa na kupitishwa, ilisababisha wimbi kubwa la wanawake nchini Japan kuingia katika mfumo wa ajira nchini humo na hivyo kuongeza nguvu kazi na pato la taifa hilo kuongezeka mara dufu.

Najua wapo baadhi ya wanawake wenzangu wanaweza wasiunge mkono hoja yangu kwa hofu kwamba jambo hili linaweza kusababisha kuongezeka kwa unyanyasaji wa kijinsi kwa wanawake na pia kuwafanya waajiri kukwepa kuwaajiri wanawake kwa kuwaona kama ni mizigo na ni dhaifu.

Tukumbuke tu kwamba swala la kubeba mimba na likizo ya uzazi bado ni mtihani mkubwa sana kwa wanawake waajiriwa, ingawa swala la uzazi ni muhimu kwa ustawi wa taifa lolote duniani kwa sababu ni kitendo cha kuzalisha nguvu kazi mpya lakini bado mpaka sasa kuna baadhi ya waajiri wanakwazwa na swala la wanafanyakazi wa kike kubeba mimba.

Sasa je swala la likizo japo ya siku mbili kwa wanawake wanapokuwa kwenye siku zao watalipokeaje?

Mchango wenu tafadhali

snowhite, King'asti, BADILI TABIA, AshaDii, Lady doctor, ladyfurahia, Preta, Fixed Point, Kongosho, Nivea, Neylu, Lisa, miss neddy, miss chagga, Mamndenyi, Tina, Ennie, charminglady, Asnam, MankaM, Munkari, lara 1, Heaven on Earth, cacico, miss strong, a.rahabu, gfsonwin, afrodenzi, Husninyo, Karucee
 
Ufanisi utapungua sana...imagine ofisi ina wanawake 20 halaf 10 wawe kwny cku zao wasije kazini cku 2
 
hapa tulipo tu uchumi wetu na effeciency ya kazi tia maji hairidhishi sasa tuongeze na suala la 2 days leave every month huoni kama tunapunguza GDP(services carried over a period of time)
 
Naamini mwanamke awaye yeyote ambaye bado anaziona siku zake anajua maumivu ya tumbo, hisia na msongo wa mawazo anaopitia wakati anapokuwa kwenye siku zake. wako wengine hulazimika kulala kitandani wakiwa hoi bin taaban wakati wanapozitumikia siku zao achilia mbali kisirani wanachokuwa nacho na mambo mengine yanayofanana na hayo.
Mchango wenu tafadhali

Na hicho kisirani mnakuwaga nacho kwelikweli....Kama mimi siku za mwanzoni na my wife nilikuwa najua kabisa "Kugombana bila sababu days" are coming soon. Hata ikafikia muda hizo days zikifika hatujuani mpaka zikipita. Sasa hivi nimezoea ila kuna Visirani next levo inabidi tu kujihami.

NAUNGA MKONO HOJA ndugu mleta UZI
 
Ufanisi utapungua sana...imagine ofisi ina wanawake 20 halaf 10 wawe kwny cku zao wasije kazini cku 2
What a coincidence....., yaani wanawake 20 wa ofisi moja wote kwa pamoja waingie kwenye siku zao...!
Please tell me you are just kidding....
 
ni kweli na sisi wanaume tupewe siku za kupumzika tukiwa tumegegeda mwanamke maana huwa tunachoka sana kama leo nimekuja kazini basi tu ikiwezekana tulipwe hela tu tusifanye kazi
 
Na hicho kisirani mnakuwaga nacho kwelikweli....Kama mimi siku za mwanzoni na my wife nilikuwa najua kabisa "Kugombana bila sababu days" are coming soon. Hata ikafikia muda hizo days zikifika hatujuani mpaka zikipita. Sasa hivi nimezoea ila kuna Visirani next levo inabidi tu kujihami.

NAUNGA MKONO HOJA ndugu mleta UZI

Na ndiyo maana nawashangaa wanaume wanaowalalamikia wanawake wanaotoa huduma kwa wateja pale wanapopewa maneno mbofu mbofu, yaani hawaelewi tu sababu....!

Tupewe tu likizo tujipumzikie zetu mambo yakishaharibika.
 
ni kweli na sisi wanaume tupewe siku za kupumzika tukiwa tumegegeda mwanamke maana huwa tunachoka sana kama leo nimekuja kazini basi tu ikiwezekana tulipwe hela tu tusifanye kazi

kuchoka ni tofauti na kuumwa jameni...!!!! mbona hata wanawake huwa wanachoka
 
ni kweli na sisi wanaume tupewe siku za kupumzika tukiwa tumegegeda mwanamke maana huwa tunachoka sana kama leo nimekuja kazini basi tu ikiwezekana tulipwe hela tu tusifanye kazi
Ulilazimishwa kugegeda.
Kumbuka kwa mwanamke kuwa kwenye siku zake ni kanuni ya maumbile na kugegeda ni swala la kuamua kwamba ugegede au uache...
Kama huna ubavu wa kugegeda basi usilazimishe lala zako mzungu wa nne.
 
mie siungi mkono hoja....coz kwa walio wengi maumivu huja kama unakuwa umejilazalaza....mwanamke kujikaza Zinduna
 
Last edited by a moderator:
What a coincidence....., yaani wanawake 20 wa ofisi moja wote kwa pamoja waingie kwenye siku zao...!
Please tell me you are just kidding....

Unadhani haiwezi kutokea?...na tutapata uhakika gani kama kweli mtu yupo period kweli?labda kaamua kufanya mambo yake mengine tu asije kazini...mnataka haki sawa nyie lkn.
 
kuchoka ni tofauti na kuumwa jameni...!!!! mbona hata wanawake huwa wanachoka

Hujambo DEMBA,

Huyu jamaa analeta masikhara tu hapa, anafananisha uchovu kugegeda na maumivu ayapatayo mwanamke anapokuwa kwenye siku zake......!
Nakwambia itokee tu siku moja Mungu amjaalie awe mwanamke halafu halafu aingie kwenye siku zake kisha amrejeshee uanaume wake halafu aje hapa kusimulia
 
Last edited by a moderator:
Unadhani haiwezi kutokea?...na tutapata uhakika gani kama kweli mtu yupo period kweli?labda kaamua kufanya mambo yake mengine tu asije kazini...mnataka haki sawa nyie lkn.
Kwani mwanamke anaingia kwenye siku zake mara ngapi kwa mwezi?
Kama mwanamke kadanganya si itakuwa imekula kwake? Kumbuka sheria ikitungwa masharti na vigezo huwa vinazingatiwa
 
mie siungi mkono hoja....coz kwa walio wengi maumivu huja kama unakuwa umejilazalaza....mwanamke kujikaza Zinduna
DEMBA kuna wale ambao wakipata siku zao wanaombe ED makazini kwao kutokana na mauamivu wanaoyapata. Sikatai kwmaba wapo ambao wala hawaumwi na si rahisi kuwajua, lakini wengi huumwa
 
Last edited by a moderator:
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom