Je, kosa la kanisa liko wapi juu ya waraka ule?

gm man

JF-Expert Member
Nov 26, 2017
1,179
1,453
Wakuu,

Kama kichwa cha habari kinvyo jieleza hapo..je kosa la kanisa liko wapi juu ya waraka ule??????

Tujaribu kukumbuka kuwa kanisa siku zote limekuwa likihubiri amani na upendo..kanisa limekuwa likiiombea serikali kila kuicha..kanisa limekuwa likiombea amani ya nchi kila kukicha..kanisa limekuwa likiwasihi viongozi kuongoza katika hali ya usawa na kweli..

Kwakuwa mm ni muumini wa dhehebu la KKKT naomba niwakumbushe hili wale wote wanaopingana na waraka ule

Ibada katika kanisa la KKKT huwa muongoza ibada anapo elekea kufunga ibada huwa anasema "ulimwenguni pote,uwabariki watawalao,tukae na amani,hasa tunamwombea raisi wetu wa jamuuri ya muungano wa tanzania(taja jina),mawaziri na wote wenye mamlaka katika nchi hii watawale katika haki na kweli.twakusihi" (maneno haya yapo katika kitabu cha tumwabudu mungu page 350.. )...

Kwa maneno hayo tu inajitosheleza kuona jinsi ambavyo kanisa limekuwa likihubiri amani na upendo..waraka ule ulikuwa ni wakukemea matendo yote ambayo yanakinzana na mahubiri ya kanisa ambayo ni upendo na amani…

swali lakujiuliza kama kanisa huwa linaombea taifa liwe katika amani na kuwaombea viongozi wanchi watawale katika haki na kweli... je kanisa haliruhusiwi kukosoa pale linapoona viongozi hawa hawatawali katika haki na kweli???????
 
Hata enzi za JK makanisa yalionya na kushauri pale walipoona mambo hayaendi sawa ila awamu hii imekuwa nongwa!
 
Kanisa lijikite kwenye kuhubiri Imani liache siasa za mafisadi
hapo juu nimekuonesha kipande kidogo cha maneno ya kuhubiri amani...je katika waraka ule siasa iko wapi?????????
 
Kusifu Na Kuabudu
Maombi Na Maombezi
Kanisa Lipo Sawa Sawa Hakuna Tatizo Lolote
1517 Matengenezo Ya Kanisa
 
Na wale waliopita kanisani kuomba kura umewasahau...
tunacho jiuliza ni kuwa kama wao wanahitaji kuombewa kwanini sisi walitukataza kumuombea mpendwa wetu ambaye alijeruhiwa kwa risasi nyingi mwilini mwake huku wao wakikaa kimya kwa kushindwa kufanya uchunguzi na hata kulipia gharama za matibabu?????? kama wao wanaenda makanisani na kuomba kuombewa kwanini wanapingana na waraka wa kanisa?????///
 
Back
Top Bottom