Mikael Aweda
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 2,973
- 3,901
Kuna watu wanasema kuwa lugha ya kufundishia kwenye mfumo wetu wa Elimu iwe Kiingereza kwa sababu Kiingereza ndo lugha ya dunia na uandishi wa vitabu mbali mbali na ugunduzi wa technologia nyingi ikiwepo kompyuta uko kwenye lugha ya kiingiereza.
Watetezi wa hoja hii wanasema nchi nyingi zlilizoendelea zinatumia kiingereza kwa hivyo sisi tulio nyuma kimaendeleo hatuwezi kuacha kufundisha watoto wetu kwa lugha hiyo ya dunia.
Watetezi wa hoja hii wanasema tusipojifunza kiingereza tutashindwa kuwasiliana na nchi tajiri duniani kama Uingereza, marekani nk ambazo zinatumia kiingereza. Kushindwa kuwasiliana huko kutaathiri mahusiano yetu na nchi Tajiri na mwishowe tutashidwa kufanya biashara na nchi hizo. Kubwa zaidi, hata vijana wetu hawataweza kuajiriwa katika nchi hizo.
Watetezi wengi wa hoja hii ni wanasiasa ambao watoto wao ama wanasoma nje ya nchi ama wako ndani ya nchi lakini kwenye shule za st xyz au accademy ambazo shule zinazotumia kiingereza kama lugha ya kufundishia.
Kwa upande wa pili, Wako wanaosema kiingereza isiwe lugha ya kufundishia kwenye shule na vyuo vyetu. Watetezi wa msimamo huu wengi wao (si wote) ni wataalamu wa vyuo vya juu, wao wanasema kiingereza ifundishwe kama lugha nyingine yo yote kama kifaransa, kichina, kireno, kiarabu nk ili watanzania wawasiliane na watu wengine duniani. Wao wanataka lugha ya kufundishia shuleni na vyuoni iwe kiswahili.
Sababu zao ni kama hizi zifuatazo:
Kwamba wanadai kuwa kisayansi Binadamu yo yote hufikiri kwa kutumia lugha ya kwanza wa wazazi wake, kisha hulazimika kutafsiri lugha hiyo kichwani kama atalazimika kuongea kiingereza na kwamba mchakato huu unarudisha nyuma au unachelewesha ubunifu wa watoto na hivyo tunaishia kuwa na wasomi waliokariri badala ya wasomi wanaoibua vitu vipya.
Matokeo yake wahitimu wa vyuo vikuu hawaji na ugunduzi wo wote mpya na mwisho wa siku wasomi wetu wa kukariri kiingereza wameshindwa kututoa kwenye lindi la umasikini pamoja na rasilimali nyingi tulizo nazo.
Pili, kwa kuwa kiingereza yenyewe ni tabu, wengi wanadhani kuwa wanafunzi wengi wa sekondary wakifika shuleni wanaanza kuhangaika na lugha ya kiingereza matokeo yake uelewa/ufaulu wao kwenye masomo lengwa unaathiriwa.
Watetezi wa hoja hii wanatoa mifano ya nchi kama China, Korea kusini, Malaysia nk ambazo zimeendelea kwa kutumia lugha zao za asili na hawatumii kiingereza hata kwenye mifumo yao ya Elimu. China kwa sasa ndo mkopeshaji wa Marekani.
Kati ya watetezi wa hoja hii wako Dr Martha Qoroo( Dean wa Chuo kikuu cha Dsm) na Jenerali Ulimwengu (mmiliki wa gazeti la Raia Mwema na Raia Tanzania)
Tume ya jaji Warioba kwenye rasimu yao ya pili walitangaza kiswahili kama lugha rasmi ya Taifa lakini hawakusema pia kwamba Kiingereza kisiwe lugha ya kufundishia -- waliipa kiswahili nguvu lakini kuhusu lugha ya kufundishia walikaa kimya.
kwa maneno rahisi akina Warioba walikwepa mjadala huu na kuamua kukaa katikati, japo katikati yao inaelemea upande wa Kiswahili zaidi hata kama ni kwa kiasi kidogo sana.
Wewe una maoni gani na kwa nini?