kiumbempole
JF-Expert Member
- Jan 15, 2016
- 551
- 905
Wadau,
Kama mlivyosikia Wizara ya Tamisemi imetangaza ongezeko la tahsusi za kidato cha tano na sita katika michepuo mbalimbali ikiwemo sayansi, lugha, michezo, sanaa, biashara na dini.
Kwa tafakari ya haraka naona haya ni maendeleo katika kuruhusu wigo mpana zaidi wa kujifunza mambo ambayo zamani tulizoea kuona yakiishia O-level pekee au yakianzia vyuoni huko kwa wanaojikita kwenye michepuo husika., mfano elimu ya dini (Kikristo na kiislamu) na masuala ya sanaa (fineart). Lakini pia naona Lugha za kujifunza zimeongezeka, awali pamoja na kiswahi, lugha za kifaransa na kiingereza zilifundishwa. Kwa sasa kiarabu na kichina zimeongeka.
Kitu kimoja nilichokiona pia ni ongezeko kubwa la ghafla la idadi ya michepuo/ tahasusi hizo ambayo tuombee taasisi zinazosimamia ubora wa elimu ziwe zimejipanga kwa ngazi zote kuanzia ufundishaji hadi utungaji wa mitihani. Pia tuanze kujipanga kozi watakazozisoma kwa vyuo vya kati na vya juu kwa wahitimu hao.
Bado kuna maswali kama, je, serikali imefikia vipi uamuzi wa kuongeza lugha mbili pekee na sio kwa mfano kihindi, kidachi au kizulu?
Je, mfumo wa zamani ulikuwa na mapungufu yapi ambayo mfumo mpya umekuja kuyarekebisha? Mfano elimu za dini kufundishwa/kutolewa zaidi seminarini, masuala ya arts kufundishwa kwenye vyuo mahsusi kama pale Bagamoyo kwa ngazi ya cheti, diploma hadi digrii n.k.