Je, kisheria hii imekaaje?

Bi dentamol

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
987
1,912
It's lady action again.....drama queen.

Haya najua wengi mtatukana weee lakini ndio nishaumbwa hivi sasa nitafanyaje?

Ipo hivi baada ya kutengana na mume kwa miezi kama 4 hivi, nimerudi na kudai vitu vyangu anazingua kunipa inabidi nibebe vyeti vyake vya shule kuanzia Kuzaliwa, Form Four, Diploma mpaka Degree.

Lengo sio kukaa nacho, lengo mpaka anipe haki yangu ndio nimpe ikiwemo na pesa nilizochangia kujenga nyumba

Je, kuna hatua zozote kisheria? Anaweza kuchukua jamaa?
 
Sasa hapo si utaonekana mwizi? Kama kweli alikuwa mumeo, si kuna taratibu za kugawana mali mlizochuma pamoja?

Au wewe ulikuwa unajulikana kwake tu kama mke?
 
Sasa vyeti vitakusaidia Nini Kama ajira zenyewe ndo hizi. Sasa hapo atakushitaki Kwa kosa la wizi Tena sio vyeti tu na vingine utavikuta kwenye hati ya mashitaka. Kabla ya kufanya huo upuuzi ulitakiwa wewe ufuate taratibu za kisheria za kuomba mgao kupitia mahakama.
 
Kwanini hukuondoka na vitu vyako kabisa!!??

Au ulikuwa unatingisha kiberiti!?

Vyeti beba vyote yeye atapita ofisi Moja Hadi nyingine na atapewa vingine, si anaenda tu kupewa loss report.....

Kuachana ni pamoja na kufanya maamuzi ya busara na hekima, otherwise utaonekana unapenda drama tu.
 
Huna akili, vyeti umechukua vya nini sasa, akisema ulimwibia na pesa utasemaje?
Rudisha hivyo vyeti dai haki zako kama ulikuwa mke kweli.
Halafu inaonekana wewe ndo chanzo cha kuachana kwenu.
 
Kwanini hukuondoka na vitu vyako kabisa!!??

Au ulikuwa unatingisha kiberiti!?

Vyeti beba vyote yeye atapita ofisi Moja Hadi nyingine na atapewa vingine, si anaenda tu kupewa loss report.....

Kuachana ni pamoja na kufanya maamuzi ya busara na hekima, otherwise utaonekana unapenda drama tu.
Eti atapita ofisi moja hadi nyingine na kupewa cheti kingine,kirahisi rahisi tu cha form four,na six,hawezi akapewa cheti kingine tena.
 
Drama Queen 👑, I was imagine how she looks like, fortunately I met one 🙌

There is no need of disposing/hiding academic certificates of your husband, instead there are rights based tools to deal with such family matter.

You can do such childish thing to your Man today of which your beautiful future of your beloved Children may be ruined when your Man loose Job.

So please handle it with care
 
Ungesema unataka ushauri jinsi ya kupata mali zako ungepata ushauri murua kabisa kwa wajuzi.
Hilo la cheti limetia doa wadau wanachangia kwa hisia na sio ujuzi walionao. Labda kama ulitaka kutrend jf tu..
 
Sema kweli!? Wanaopotelewa vyeti Huwa inakuwaje Hadi wanavipata Tena??
cheti kama cheti huwa hakitolewi tena,wtakachokupa ni statement of results,sasa kama hujapata ajira hapo ndipo mziki utakuwepo,kwani kwenye utafutaji ajira huwa wana hitaji vyeti halisi.
 
Back
Top Bottom