@sokomoko: kwa mtizamo wangu jibu la swali lako ni HAPANA, SI MDINI;
Hata hivyo naona nawe mwenyewe umeingia katika mtego wa madai na hofu batiri zinazopikwa na watu pasi msingi. Kosa la mtelezo ulichokifanya katika mada yako ni hili:
Kwa vile 2x2 = 2+2 = 4
sasa unasema 3x3 = 6
Sokomoko, Kiongozi Mkuu wa nchi au yeyote hawezi kuonyeshwa kuwa si mdini au ni mdini simply kwa kutoa hesabu ya Mawaziri na Wakuu wa Mikoa / Wilaya n.k Ukifanya hivyo asubuhi na mapema Wahindu, Wapagani, Wabidha n.k nao watabisha katika mlango wango uwape hesabu yao mapema vinginevyo watakurudisha na kusema ama serikali yetu ni wadini wa Uislam au Ukristo! Je ni vipi watu kwa kutumia mahesabu yako watasema kuhusu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Tafadhali sana kuwa makini katika kuleta hoja zenye kuleta mshikamano wa Kitaifa badala ya kuchochea hisia ambazo hakika mimi binafsi nasema hatuna udini isipokuwa kuna wachache wanataka tuelekee huko.
Kwa kifupi njia unayoitumia ni sawa na ile wengine pia wenye ufinyu wa mawazo wanaitumia kutoa lawama za udini.
Nakuuliza je ni halali kuassume kwamba idadi ya Watanzania wenye
sifa za kuajirika ni sawa kati ya Wakristo na Waislamu na kwamba tukiteremka katika sifa (profile) zao
kitaaluma, kiuzoefu, kimaadili na hata kiutashi pia utapata idadi sawa yaani 50% kila moja. kama jibu la swali langu ni hapana basi huna haja ya kuonyesha asilimia kujaribu kuprove kuwepo kwa udini au kutokuwepo kwa udini.
Mimi kawaida yangu namsubiri yeye anayedai kuwa Rais wetu ni Mdini, ndiye atuhakikishie hilo na nakwambia kuwa hakuna anayeweza kutuonyesha hilo.
Zaidi ya yote, Sokomoko unasema,
Nasikia JK aliwaambia kuwa nchi hii haina dini na itakuwa ubaguzi kuwapa ruzuku watu wa dini moja na kuwaacha wa dini nyinginezo akatolea mfano kuna waislam, wabudda, masingasinga, wahindu na wasiokuwa na dini je hao hawana haki ya kupewa ruzuku? na serikali ikitoa ruzuku kwa hawa wote itawezaje kujiendesha?
Hakika huu ni uzushi na kuleta Sokomoko fanya tu assigment yako ujue hadi unaposoma maandishi yangu sasa ni Vyuo vingapi na Vituo vya Afya hususani hospitali teule ngapi zinaendelea kupewa ruzuku mpaka leo!.
True, 2 x 2 = 2+ 2 but 3x3 is not equal to 3+3