Je, kazi ya Jaji kwenye kesi ya Mbowe ni kurekebisha sheria Mahakamani au kutoa tafsiri ya sheria?

Mnachekesha sana, Jaji kajibu hoja za mawakili wenu vizuri sana, mifano yote waloainisha kwa pingamizi haiendani na swala walowekea pingamizi, lakini pia sheria ya tafsiri ya sheria iko wazi, jina la sheria tu linatosha na kumbuka Tanzania Bara kuna CPA moja tu, hoja nyepesi sana ile.

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app

Jaji alitumia tafsiri ya kamusi [TUKI], bila kifungu chochote cha kisheria.
 
Toa hoja, Matusi hayatakusaidia kwenye maisha yako hapa Duniani

Hoja hujibiwa kwa hoja

Mtu asiyekuwa na hoja mara nyingi anapata hasira na kukimbilia kutukana matusi

Matusi hayajengi wala hayakuongezei pesa mfukoni
Huyu Jaji ni wa ajabu sana, anadhalilisha taaluma ya Sheria.
 
Naona jamaa wameigeuza tasnia yao kama uwanja wa burudani wanadhani wale wanaohudhiria ile kesi ni mashabiki wanaoenda kutazama maigizo yao, jaji wa sampuli hii hata kama angekuwa baba yangu akirudi nyumbani au hata kwa simu ningemwambia kweli mzee unazingua hii sheria yenu mpya ya siku hizi nyie mmeisonea wapi?
 
Jaji Tiganga anayesikiliza kesi ya Freeman Mbowe inayohusiana na ugaidi amekubali kuwa sheria iliyotumika ili ushahidi upokelewe mahakamani imekosewa kutoka upande wa mamlaka ya kiserikali au Mashtaka.

Maajabu, Kwanini Jaji Tiganga amelazimisha kupokea huo ushahidi wakati kuna kesi nyingi alizoamua Yeye mwenyewe zamani alizitupilia mbali kwa kigezo cha kutumia kifungu tofauti yaani(Wrong Citation).

Swali 1,
Je Jaji Tiganga Yeye amegeuka kuwa Bunge la kutunga sheria kwa kuamua kurekebisha sheria akiwa mahakamani badala ya kutafsiri?

Kitendo alichofanya Jaji Tiganga eti pingamizi halina Madhara ni kunajisi mahakama, Ni dhahiri haki haiwezi kupatikana kwenye kesi ya Mbowe.

vitendo kadhaa anavyovionyesha Jaji Tiganga mahakamani vinasikitisha sana Raia, Kwa mfano kuna muda analazimisha maneno ambayo mashahidi wa serikali hawajayatamka na yeye anasema aliyasikia, Anapoambiwa mheshimiwa soma Inaonekana hilo neno halipo.

Swali 2,
Je Kitendo cha Jaji kuwa omba msamaha mashahidi wa Mashtaka yaani upande wa serikali kwa kuhojiwa maswali magumu na upande wa utetezi inaleta picha gani?

Ni dhahiri hukumu ya hii kesi walishaandaa kwa kuamua kupindisha sheria.

Kesi hii imekuwa ya Zig zag na ya kutokueleweka kabisa, Kesi hii na Jaji huyu anaifedhehesha mahakama.

Hawa majaji ndio wanajenga Taifa linalogawanyika.

Je hawa Majaji ni Raia wa Tanzania?

Nashindwa kuelewa kabisa kwanini Majaji wengi aliowateua JPM hayati wanatuharibia Taifa, JPM aliwapa kitu gani hawa watu mpaka kufukia sehemu ya kuchochea utengamano wa Taifa kwa kutokufuata msingi ya sheria ya Bunge.
Kwa kweli hata mimi sasa nimeanza kutoelewa kama mahakama bado ina ule msimamo wake wa siku zote kwamba chochote kinacholetwa mahakamani sharti kiungwe mkono na sheria husika. Sasa kama Polisi wanaandaa mashitaki na vielelezo kwa kutumia sheria ambayo haipo na mahakama inapokea maana yake nini? Sasa kama ni hivyo sheria zina kazi kazi mahakamani? Na hao wanaitwa wanasheria kwa sababu sheria ndio msingi wa utendaji kazi wao na wa mahakama. Ukweli ni kwamba Mahakama msingi wake mkubwa wa utendaji kazi ni sheria. Sasa kama mtu anashitakiwa kwa sheria ambayo haipo na inakubalika, maana yake nini?
 
Jaji Tiganga anayesikiliza kesi ya Freeman Mbowe inayohusiana na ugaidi amekubali kuwa sheria iliyotumika ili ushahidi upokelewe mahakamani imekosewa kutoka upande wa mamlaka ya kiserikali au Mashtaka.

Maajabu, Kwanini Jaji Tiganga amelazimisha kupokea huo ushahidi wakati kuna kesi nyingi alizoamua Yeye mwenyewe zamani alizitupilia mbali kwa kigezo cha kutumia kifungu tofauti yaani(Wrong Citation).

Swali 1,
Je Jaji Tiganga Yeye amegeuka kuwa Bunge la kutunga sheria kwa kuamua kurekebisha sheria akiwa mahakamani badala ya kutafsiri?

Kitendo alichofanya Jaji Tiganga eti pingamizi halina Madhara ni kunajisi mahakama, Ni dhahiri haki haiwezi kupatikana kwenye kesi ya Mbowe.

vitendo kadhaa anavyovionyesha Jaji Tiganga mahakamani vinasikitisha sana Raia, Kwa mfano kuna muda analazimisha maneno ambayo mashahidi wa serikali hawajayatamka na yeye anasema aliyasikia, Anapoambiwa mheshimiwa soma Inaonekana hilo neno halipo.

Swali 2,
Je Kitendo cha Jaji kuwa omba msamaha mashahidi wa Mashtaka yaani upande wa serikali kwa kuhojiwa maswali magumu na upande wa utetezi inaleta picha gani?

Ni dhahiri hukumu ya hii kesi walishaandaa kwa kuamua kupindisha sheria.

Kesi hii imekuwa ya Zig zag na ya kutokueleweka kabisa, Kesi hii na Jaji huyu anaifedhehesha mahakama.

Hawa majaji ndio wanajenga Taifa linalogawanyika.

Je hawa Majaji ni Raia wa Tanzania?

Nashindwa kuelewa kabisa kwanini Majaji wengi aliowateua JPM hayati wanatuharibia Taifa, JPM aliwapa kitu gani hawa watu mpaka kufukia sehemu ya kuchochea utengamano wa Taifa kwa kutokufuata msingi ya sheria ya Bunge.
Ile kauli ya hukumu dhidi ya Mbowe toka kwa Mama kupitia BBC inaitesa mahakama. Alisha sema Mbowe ni gaidi na magaidi wenzake walishafungwa alibaki yeye tu na kwamba bahati nzuri amekamatwa na atapata haki yake kama wenzake
 
Mpaka sasa huo ugaidi haujaonekana, hiyo bastola kwako ndiyo silaha nzito ya kufanyia ugaidi! Wengine tulitegemea mwanzo tu tungeoneshwa silaha zilizoandaliwa kufanyia ugaidi ni si mbege na nyama choma, kesi ya ugaidi inatumia muda mrefu kuzungumzia uzurulaji na nyama choma!
Kesi hii haipo kwani Rais alikwisha thibitisha tuhuma na waliokwisha hukumiwa japo wasio wanaccm hawakuisikia kesi hiyo. Kabla jeshi la polisi kutumia ushahidi wa kukata miti Dar mpaka Iringa wangeweka ushahidi wa kulipua daraja la Ruvu na Ruaha Mbuyuni na madogo madogo mengine angalau ungeeleweka. Katika ugaidi wote unaofanyika duniani hatujawahi kushuhudia uchomaji wa vituo vya mafuta ukiua watu au kuangusha serikali. Ugaidi wote hufanyika kwa lengo maalum na unakuwa na viongozi waliojipanga pamoja na silaha nzito.
Ugaidi wa kukata miti toka Dar hadi Iringa! Kwanini siyo kutoka Dar hadi Arusha?
 
Inatia hasira sana! Yaani "wrong citation" kwenye kesi ingine kwa jaji huyohuyo haifai, wrong citation kwenye kesi ya Mbowe kwa jaji huyohuyo inafaa!!
 
Umeanza vizuri napoint nzuri mwisho unamalizia na uzwazwa, hivi jpm yupo hapa sasaivi, unamlaumu yeye ndio anaongoza serikali sasaivi? Kwanini usimlaumu kiongozi mkuu awabadolishe hao majaji.

Mnamfanya mwenye mamlaka nayeye kujificha kwenye hizolawama za kipuuzi.

Mkianza kumsifia mama wote mnakenuamimeno mnasema aaaaah hakuwachagua yeye hawa sindio!!.

Mnapoteza muda na nguvu nyingi kupambana na marehemu hovyo sana nyinyi watu.
Hapo ndipo inashangaza, kumsema vibaya marehamu ni kukwepa uwajibikaji. Binafsi nilikuwa simpendi kabisa JPM lakini kitendo cha kuendelea kusutwa naona ni very unfair; katika jamii zilizo staarabika huwezi kuta tabia za namna hii.
 
Jaji anaondoa pingamizi la kisheria kwa kutumia tafsiri za TUKI, hovyo kabisa..!!
Ogopa sana msomi anayesema hadharani katolewa jalalani... Ogopa sana neno "...wa darasa la saba wanatosha!" ogopa zaidi neno "...nimekuteua mimi na nakulipa mshahara halafu nishindwe kesi!!?" tunakoelekea jaji anaweza kutuletea mifano ya huihui na bulicheka kama si kuchukua maneno ya abunuwas na kuwa mfano katika kesi hii.
Haya ni baadhi ya maneno yametufikisha hapa leo mahakama kuonekana ni sehemu ya mchezo kama wa tom and jerry. Ahsante kwa Jamhuri kutuletea kesi ya Mbowe ambayo inafunua yaliyojificha
 
Back
Top Bottom