seedfarm
JF-Expert Member
- Feb 9, 2020
- 260
- 2,654
Jaji Tiganga anayesikiliza kesi ya Freeman Mbowe inayohusiana na ugaidi amekubali kuwa sheria iliyotumika ili ushahidi upokelewe mahakamani imekosewa kutoka upande wa mamlaka ya kiserikali au Mashtaka.
Maajabu, Kwanini Jaji Tiganga amelazimisha kupokea huo ushahidi wakati kuna kesi nyingi alizoamua Yeye mwenyewe zamani alizitupilia mbali kwa kigezo cha kutumia kifungu tofauti yaani(Wrong Citation).
Swali 1,
Je Jaji Tiganga Yeye amegeuka kuwa Bunge la kutunga sheria kwa kuamua kurekebisha sheria akiwa mahakamani badala ya kutafsiri?
Kitendo alichofanya Jaji Tiganga eti pingamizi halina Madhara ni kunajisi mahakama, Ni dhahiri haki haiwezi kupatikana kwenye kesi ya Mbowe.
vitendo kadhaa anavyovionyesha Jaji Tiganga mahakamani vinasikitisha sana Raia, Kwa mfano kuna muda analazimisha maneno ambayo mashahidi wa serikali hawajayatamka na yeye anasema aliyasikia, Anapoambiwa mheshimiwa soma Inaonekana hilo neno halipo.
Swali 2,
Je Kitendo cha Jaji kuwa omba msamaha mashahidi wa Mashtaka yaani upande wa serikali kwa kuhojiwa maswali magumu na upande wa utetezi inaleta picha gani?
Ni dhahiri hukumu ya hii kesi walishaandaa kwa kuamua kupindisha sheria.
Kesi hii imekuwa ya Zig zag na ya kutokueleweka kabisa, Kesi hii na Jaji huyu anaifedhehesha mahakama.
Hawa majaji ndio wanajenga Taifa linalogawanyika.
Je hawa Majaji ni Raia wa Tanzania?
Nashindwa kuelewa kabisa kwanini Majaji wengi aliowateua JPM hayati wanatuharibia Taifa, JPM aliwapa kitu gani hawa watu mpaka kufukia sehemu ya kuchochea utengamano wa Taifa kwa kutokufuata msingi ya sheria ya Bunge.