Uchaguzi 2020 Je, kauli hizi za 'Tamaa ya Madaraka na kutomtuma mtu kugombea' alizotoa Rais Magufuli ni dongo kwa Makonda na Gambo?

Ukimsikiliza msemaji wa Rais anakwambia wazaramo wanausemi ambao unabamba sana mjini usemao Mwana kulitafuta Mwana kulipata pia Mama Samia naye anakwambia wateule wa Rais wajifunze kuridhika Ukija kwa JPM mwenyewe anawaambia mie sijatuma mtu pia mjifunze kuridhika hapo bado Sijamsikia boss wa ma RC na DC Yani Majaliwa ukirud kuyatafuta maneno ya Polepole kuhusu Kigamboni ndo kabisa utajua Makonda alikuwa analindwa tuu mana mabosi wake wanajua kuwa hapendwi na watu hvyo wamwachie madaraka ili apate kinga Sasa naleo tunaambiwa Mtoto akililia Wembe tumpe au tumnyime
 
Inaweza kuwa hii hapa
20200716_115842.jpeg
 
Ukimsikiliza msemaji wa Rais anakwambia wazaramo wanausemi ambao unabamba sana mjini usemao Mwana kulitafuta Mwana kulipata pia Mama Samia naye anakwambia wateule wa Rais wajifunze kuridhika Ukija kwa JPM mwenyewe anawaambia mie sijatuma mtu.

Pia mjifunze kuridhika hapo bado Sijamsikia boss wa ma RC na DC Yan Majaliwa ukirud kuyatafuta maneno ya Polepole kuhusu Kigamboni ndo kabisa utajua Makonda alikuwa analindwa tuu mana mabosi wake wanajua kuwa hapendwi na watu hivyo wamwachie madaraka ili apate kinga Sasa naleo tunaambiwa Mtoto akililia Wembe tumpe au tumnyime?
 
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Sijaona sababu ya Rais kulalamikia hicho kizazi cha 1982!

Ni ukweli ulio wazi, kiburi na dharau za Makonda zimetokana na Rais mwenyewe kwa kuamua kumkweza zaidi kuliko Wateule wake wengine.
 
Ila Magufuli nimekubali...kweli Hajaribiwi. Ukiweka ugoko anaweka chuma.

Kamkataa dogo mapema tu.
 
Uzuri ni kwamba Makonda alisha jiandaa kisaikolojia ukisikiliza hotuba yake alipokutana na UVCCM mkoa wa Dar.

Nanukuu “kwa sasa raisi ata akisema nikalime nyanya, nipo tayari. Lengo langu kubwa ni kuhakikisha CCM inarudisha majimbo yote ya Dar uchaguzi huu baada ya hapo ntakuwa happy ata nje ya siasa”.

Inawezekana ameshavuna vya kutosha anataka kutumia mtaji aliokusanya kufanya biashara zingine kwenye ubunge akipata akikosa hakuna wa kumuuliza hela anatoa wapi.

I don’t know nadhani ni maamuzi yaliyotokana na calculated risks.

Hila ni kipindi cha Makonda kujua nani alikuwa rafiki yake wa ukweli.
 
Back
Top Bottom