Uchaguzi 2020 Je, kauli hizi za 'Tamaa ya Madaraka na kutomtuma mtu kugombea' alizotoa Rais Magufuli ni dongo kwa Makonda na Gambo?

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,059
4,041
Rais Magufuli baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu Dodoma amenena kwamba viongozi mbalimbali hawaridhiki kabisa na madaraka hasa waliozaliwa mwaka 82 (1982).

Pia soma> Uchaguzi 2020 - Tamaa za Wateule wa Rais kutia nia Ubunge zitawaponza wengi. Ushahidi huu hapa wa Rais Magufuli na Humphrey Polepole...

Kauli hii imenifanya niangalie mwaka aliozaliwa Paul Makonda na Mrisho Gambo na kukuta wote wamezaliwa mwaka 1982. Naamini hii haiwezi kuwa bahati mbaya ila Rais alimaanisha alichokisema.

Nanuia kusema kwamba Makonda na Gambo mpaka sasa wana hali mbaya na huenda ukawa mwisho wao kisiasa.


Baadhi ya nukuu za Rais Magufuli...

Kwenye hizi kazi kuridhika ni kitu kikubwa. Yule kijana pale anaitwa Selemani ana PHD lakini mshahara ni laki 5. Aliridhika na mshahara wake. Ilipojitokeza fursa ndiyo tukamteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa. Viongozi vijana imekuwa ngumu kuridhika hasa waliozaliwa miaka ya 1982.

Nilikuwa napewa taarifa na Makamu wa Rais, waliojitokeza kugombea kupitia CCM mpaka sasa ni zaidi ya 8,000 na Dar es Salaam ndiyo inaongoza ambapo hadi leo alfajiri wapo 829


Nawapongeza waliotia nia lakini niwahakikishie hakuna aliyetumwa na mimi, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mzee Mangula wala Katibu Mkuu, kama wapo wanaosema mimi nimewatuma ni waongo na hii meseji iwafikie Wana-CCM wote nyinyi wapimeni wagombea kulingana na mnavyoona wanafaa

Sijatuma mtu [kugombea ubunge]. Siwezi nikatuma mtu kupitia mgongo wa pembeni. Kama ningekuwa na uwezo wa kukutuma, kwanini nihangaike kukutuma, si ningesubiri tu kwenye viti vyangu 10 nikakuteua kama ningeshinda.

Makonda.JPG

Screen Shot 2020-07-16 at 14.07.02.png

Screen Shot 2020-07-16 at 14.05.54.png
 
Lakini pia ukiwa mbunge,huna hofu ya kuondolewa kama ukiwa mteule hasa wa Magu, hivyo huenda ndio maana wengi wanaona bora wajaribu nafasi za kuchaguliwa achilia mbalii masilahi bora zaidi.

Ila bado nasisitiza,msimuamini Magu katika hili.
 
Bashite .....😔😔
Mi naona kabisa koroboi utambi unazama. Magu hanaga mambo ya kiswahili Kwanza Hana Siri akisema hakutaki ,hakutaki kweli, akisema sijakutuma ujue hujatumwa Hana kupapasa papasa mambo.

Kwenye hili makondo hawezi kosa tundikwa dripi za kutosha.
 
Wacha tungoje tuone. Nchi hii ina maajabu mengi. Let's not jump to conclusion. In the long run I am sure he knows what he is doing, hajakurupuka
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom