Je, Kanda ya Ziwa kutumika kama daraja la kuwavusha wanasiasa 2025 waliodiriki kumkejeli Hayati Magufuli?

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,720
10,216
JE, KANDA YA ZIWA KUTUMIKA KAMA DARAJA LA KUWAVUSHA WANASIASA 2025 WALIODIRIKI KUMKEJELI DR JOHN POMBE MAGUFULI?

1699961410512.jpg


Baada ya kifo cha marehemu Dr John Pombe Magufuli tuliona wanasiasa waliokuwa karibu yake na wengine ambao Leo hii wapo madarakani Kwa sababu yake walianza kumnanga na kumkejeli Kwa lugha za dharau na kumwita kama Kiongozi ambaye hakufanya chochote.

Kitendo hicho sio kwamba kimeacha mpasuko mkubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi na hata Serikalini na kwamba wapo watu naamini wakipewa nafasi ya kuongea nini maoni yao kuhusiana na chawa waliokuwa wanamkashfu hayati nadhani unaweza kuona namna walivyokasirishwa na uchawa ule lakini Kwa sababu wengi aidha kwa uoga ama kuogopa na kutetea vibarua vyao waliamua kukaa kimya na kuunga azimio la kumkashifu hayati.

Kadri siku zinavyokwenda wapo wanasiasa wamesoma na kuona upepo wa Kanda ya Ziwa hauko vizuri na wameona waje na mbinu mbadala za kutaka kuwaaminisha kuwa wao wapo pamoja na Kanda ya Ziwa wakati kiukweli sio kweli. Ninaposema hivyo nadhani wabobevu wananielewa ninamaanisha nini.

Wapo watu wameumizwa na propaganda za Sukuma Gang waliowaaminisha wenye Mamlaka kuwa watu wa Kanda ya Ziwa ni hatari na hawatakiwi kuwepo katika nafasi wakati wakifahamu kuwa sio kweli na Kwa kiasi fulani wamefanikiwa na hivyo kupelekea wengine kutolewa katika nafasi zao na wengine wamestaafishwa Kwa manufaa ya umma bila sababu.

Rai yangu kwa watu wa Kanda ya Ziwa ni wakati wa kusoma pumba na mchele

Ni bora kufa ukiwa umesimama kuliko kupiga magoti kuwasujudia watu.

Tanzania yetu Sote

Madulu S. Shingamagaji

Itilima- Simiyu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom