Je, Japan inajua alipo Rachel Dangwa?

Je, Japan inajua alipo Rachel Dangwa?

Rachel (Recho) Dangwa amejitokeza hadharani na kuthibitisha kuwa yuko hai baada ya kupotea kwa takriban miezi miwili nchini Japan.

Taarifa mpya zilizotolewa na watu wake wa karibu, akiwemo Twaha Mwaipaya kwenye Facebook na kurasa za kijamii, zinasema kuwa alikuwa mgonjwa sana, lakini sasa amepona na amewashukuru Watanzania wote waliokuwa wanamwombea na kumjulia hali.

Kabla ya kujitokeza kwake, kulikuwa na sintofahamu kubwa mtandaoni kuanzia mapema mwezi Agosti 2026 baada ya wanaharakati kama Maria Sarungi kutoa tahadhari kuwa Rachel amepotea nchini Japan na hapatikani kwenye simu zake. Hali hiyo ilizua uvumi mbalimbali, ikiwemo madai ya uwongo kwamba alikuwa ametekwa au amefariki dunia, mambo ambayo sasa yamekanushwa rasmi baada ya yeye mwenyewe kujitokeza akiwa salama.
 
Back
Top Bottom