bobdizo turuku
Member
- Sep 5, 2018
- 5
- 1
Wadau,
Nimeisoma kwa umakini mkubwa sana thread ya mdau mmoja aliyekata shauri na kuamua kwenda kupima HIV!
Kiukweli kabisa toka katika uvungu wa moyo wangu nampongeza sana na Mwenyezi Mungu amuokoe huyu ndugu! Lakini kati ya wachangiaji waliosimama kidedea kuchangia thread hii, mchangiaji mmoja nimemnukuu akisema, "hukujua kuwa kupata UKIMWI ni kazi ngumu sana.."
Na kwa bahati mbaya alipoombwa kutoa elimu na uzoefu wake na baadhi ya wadau, hakuonekana tena! Usemi huu umeibua tafakari na tafakuri nyingi katika halmashauri yangu ya kichwa, nikirejea na siku za mgongoni nikiwa darasani mwalimu pia aliwahi kusema maneno sawia na ya mchangiaji wa leo na toka ya hapo, swali hili limetoka katika tawala za kichwa changu kwamba, "Je, inawezekana mtu akalala (siyo kulala huku kwa kawaida, tafsida imezingatiwa) na mtu mwenye UKIMWI tena bila condom na asipate UKIMWI?".
Nisaidieni wadau.
Nawasilisha.
======