Je, inawezekana kuiunganisha ATCL na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ikawa ni taasisi moja?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,004
142,034
Jana CEO wa ATCL amesema shirika lake liko katika mipango ya kufanya baadhi ya huduma lenyewe bila kutumia wakala, na kati ya huduma hizo ni ile ya chakula na vinywaji ndani ya ndege.

Matindi amesema huo ndiyo mfumo wa kisasa unaotumiwa na mashirika mengi ya ndege yenye mafanikio duniani.

Swali dogo ni je, ATCL na mamlaka ya viwanja vya ndege haziwezi kuunganishwa ikawa taasisi moja kama ilivyokuwa Dawasco na Dawasa?

Mkuu Barafu, msaada wako tafadhali.

Maendeleo hayana vyama!
 
Haiwezekani kuunganisha na TAA. Huduma za Chakula na Vinywaji hazitolewi na mamlaka ya viwanja vya ndege.

Huduma Kama hizi zinatolewa na private company Kama LSG sky chef, huduma za handling zinatolewa na Swiss port.

Hawa watoa huduma wote wanalipa mamlaka za viwanja vya ndege. However, ATC inaweza ikatoa huduma hizi yenyewe Kama Wana facilities.

Kwa mfano handling, ATC watalazimika kununua yale mabasi ya kubeba abiria kutoka katikati ya kiwanja mpaka arrival gate.

My view ATCL CEO anatakiwa aweke jitihada na kuhakikisha anaendesha shirika bila utegemezi wa serikali
 
Aisee! unafahamu vizuri majukumu ya mamlaka ya viwanja vya ndege?

Ni sawa na kusema kwanini tusiiunganishe UDART na TANROADS?
 
johnthebaptist,
Unataka kusema nini hasa??
Huduma zipi hizo za Mamlaka za Viwanja vya Ndege unataka ziunganishwe na ATCL..??

Nani kakwambia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ndio inayotoa huduma za chakula na vinywaji kwenye Ndege??hahahahaah.

Duu kumbe kichwani mweupe namna hii??

These aren't your levels..nenda kaandike habari za Humphrey Polepole na wajinga wengine hapo Lumumba.
 
MENGELENI KWETU,
Hahahaaaaa......... Mbona umepanic bwashee?!

Wenye akili wameelewa swali langu lakini wewe fly2kia huwezi kuelewa uwezo wako ni 16,000 ya Polepole Dsm - Moshi Christmas!
 
Back
Top Bottom