Baada ya Vuta Nikuvute Hatimaye KADCO Yakabidhi Uwanja wa Ndege Kilimanjaro kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA)

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Kiwanja cha Ndege cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA) kimekabidhiwa rasmi kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA) kutoka kwa iliyokuwa Kampuni ya Uendelezaji na Uendeshaji Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (Kadco) baada mkataba wa uendeshaji kukamilika Novemba 9, mwaka huu.

Akizungumza leo Novemba 11, wakati wa hafla ya makabidhiano ya kiwanja hicho Waziri wa Uchukuzi, Prof Mbarawa amesema pamoja na mabadiliko hayo yaliyofanyika Serikali itazingatia stahiki zote za wafanyakazi zinalipwa kulingana na sheria.

“Kiwanja cha KIA ni cha kimkakati pamoja hivyo pamoja mabadiliko yaliyofanyika tayari kuna kikosi kazi kinatakachohakikishwa viwango vya uendeshaji vinaendelea kukua na maslahi ya watumishi yanapatikana kulingana na sheria za utumishi zilizopo,” amesema.

Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa kutoa tamko kwa Kadco kuachia kiwanja hicho Novemba 9, 2023 bungeni, wakati akisoma taarifa yake mbele ya wabunge baada ya mvutano uliochukua mwaka mmoja, huku wabunge wakitaka TAA ichukue jukumu la uendeshaji.
 
Back
Top Bottom