Je, hii 'Media Blackout' ya leo juu ya tukio zima la uchukuaji fomu wa Tundu Lissu ndiko kumuenzi vyema Mwanahabari Hayati Rais Mkapa?

Kwani chadema nyie si huwa mnarushwa DW, BBC, VOA, KTN.
Vyombo vya kimataifa mna shida gani na hutu tu media twa humu humu?
 
Kwa kweli katika hali ya kawaida ikatokea umetarget MTU kumuua ukajua umemaliza kazi afu baadae sana unamwona anaibika na kukunyooshea kidole kuwa ulitaka kumuua bila shaka utapatwa na hofu sana. Bila kumungunya maneno huyu mgombea wa CHADEMA anatia watu hofu na ikiwa atakuja kuwa rais siku moja atajijengea historia kuliko hata viongozi wa kiafrika waliopigania uhuru.
 
Nichukieni mtakavyonichukia GENTAMYCINE ila pamoja na kwamba nakipenda Chama changu Tawala ambacho ndicho Kimeshika Dola ya Kiserikali cha CCM, ila kama 'Mwanataaluma' kitendo kilichofanyika leo hasa cha 'Media Blackout' dhidi ya Tukio zima la Uchukuaji Fomu wa Tundu Lissu wa CHADEMA na ambayo nayasikia yameendelea huko katika Newsrooms ni 'Upumbavu' mtupu.

Sijaona sababu yoyote ile ya Vyombo Vikubwa vya Habari nchini Kupigiwa Simu na hata Waandishi wake 'Kutishwa' hasa kama wakipeleka Hewani ( kama haya Madai ni ya kweli kwani sijayathibitisha bado ) Habari za hili Tukio zima, lakini kinachonisikitisha tu ni kwamba Serikali yangu ya CCM imefanya mengi na makubwa kwa miaka hii Mitano sasa iweje leo hii imuogope Tundu Lissu hivi?

Najua kuwa Tundu Lissu ( Mtani wangu huyu kutoka Mkoani Singida nae ana Changamoto zake ) ila binafsi nilidhani njia pekee ya 'Kummaliza' Kisiasa ni Sisi wana CCM na Serikali yetu Kumuonyesha kwa Vitendo 'Maendeleo' tuliyoyafanya na siyo 'Kumuogopa' hivi hadi kumfanyia 'Mizengwe' ili Tukio zima la leo lisiwe Masikioni mwa Watu ( Watanzania ) tukidhani kuwa labda ndiyo tutamuweza.

Wala haiitaji 'Akili' kubwa kujua ya kwamba kadri Mamlaka husika iliyo chini ya Chama changu Tawala cha CCM kinavyopambana kutaka 'Kumzima' Kisiasa na Kiumaarufu hivi Tundu Lissu kwa 'Kuwatishia' Wanahabari na Vyombo vyao basi ijue ya kwamba ndiyo inasaidia mno Kumuongezea 'Umaarufu' wako na hapa kuna 'Athari' nyingi tu kwa upande wa Kura CCM yangu itazipata.

Halafu Wiki iliyoisha tulikuwa tunamsifu na kumpamba kweli kweli Nguli wa Habari nchini na Mwandamizi kabisa Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa kwamba alipenda 'Demokrasia' na hakuwa na 'Mabavu' dhidi ya Wapinzani. Je, huu 'Upumbavu' uliofanywa leo wa 'Kuvitishia' Vyomba vya Habari Vikubwa nchini 'Visiripoti' Tukio la Lissu ndiyo Kumuenzi Mkapa?

CCM yangu naipenda, Rais na Mwenyekiti wangu Dkt. Magufuli namkubali sana hata Mwenyezi Mungu anajua ila huu 'Upuuzi' mkubwa sijaupenda.
Me nadhani kwa namna nyingine wanamsaidia TL indirectly mana umaarufu wake unazidi kupaa kuliko miundombinu mana tushachoka kusikia mambo ya tumetekeleza 😂😂😂na kosa jingine kubwa nikuzuia watu kufanya siasa kwa kusubiri uchaguzi huo ulikuwa uamuzi mbovu kuwahi kutokea mana ni sawa kuwashindisha watu na njaa halafu sasa chakula ndio kimepatikana too late kwa tawala mambo yashakuwa sio mambo watu wana hamu sana na siasa kwakua siasa ndio maisha yetu hivyo media na yeyote yule ameshachelewa now kipyenga kishalia na hawajajipanga kwa haya kwauhakika.
 
Yaani hawako serious. Yaani kununua vifaa wameshindwa?
Vifaa vinavyohitajika ni
-camera yenye sdi out
-wireless microphone ya camera
-sdi cable
-liveUsolo
-modem ya 4G
-line ya 4g yenye bando.

Wakipata hiyo setup wanaweza kuenda live wakiwa popote kwenye mtandao kupitia youtube, facebook. Inabidi wanunue haraka kabla ya kampeni kuanza. Hakuna chombo chochote cha habari kitakacho onesha hata picha ya wapinzani.

NB: wale wazoefu wa kuagiza vitu mtafanya bajeti ya vifaa.
Naunga mkono hoja, maCCM yatawahujumu sana CDM kupitia vyombo vya habari. Ni muhimu CDM ichukue tahadhari mapema, sasahivi karibu kila mwananchi ameshasikia habari za social media na wengi wao kupata taarifa kupitia huko. Saa ya Ukombozi ni Sasa
 
Wapinzani kuweni na youtube channel zenu. Nunueni vifaa vya kurusha matangazo kama blackmagic, teradek,cerevo,liveUsolo,vidiu,mevo,gopro, roland livestream,dji drone livestream. Share link kupitia mitandao waambieni watu wasubscribe wafike 5m. Kulalamika hakutasaidia kitu.

Muda wa kampeni hakuna chombo chochote cha habari kitakacho onesha hata picha yenu.

Nunueni vifaa.
Wanunue kwa pesa ipi umewapa wewe pesa zote za ruzuku walizilamba zote Sasa wanalia Lia media ziwatangaza Bure utafikiri media Ni Charity organization !!! Kuwa wakirusha hewani wanarusha bure wafanyakazi watangazaji,makundi mitambo nk kuwa Ni wa Bure na umeme Ni bure,na leseni Yao Ni bure !!!!

So kulalamika hawaruhushwi hewani hawana pesa za kununua vifurushi vya air time na kuandikwa magazetini kununua kurasa
 
Tokea nikujue hapa Jamvini JamiiForums japo ni 'Mkongwe' ila hujawahi kuwa na 'Akili' na hata Michango yenye 'Tija' ila umejawa na 'Ujuha' sana.
 
Yaani hawako serious. Yaani kununua vifaa wameshindwa?
Vifaa vinavyohitajika ni
-camera yenye sdi out
-wireless microphone ya camera
-sdi cable
-liveUsolo
-modem ya 4G
-line ya 4g yenye bando.

Wakipata hiyo setup wanaweza kuenda live wakiwa popote kwenye mtandao kupitia youtube, facebook. Inabidi wanunue haraka kabla ya kampeni kuanza. Hakuna chombo chochote cha habari kitakacho onesha hata picha ya wapinzani.

NB: wale wazoefu wa kuagiza vitu mtafanya bajeti ya vifaa.
Na kibali cha tcra!?????
 
Nichukieni mtakavyonichukia GENTAMYCINE ila pamoja na kwamba nakipenda Chama changu Tawala ambacho ndicho Kimeshika Dola ya Kiserikali cha CCM, ila kama 'Mwanataaluma' kitendo kilichofanyika leo hasa cha 'Media Blackout' dhidi ya Tukio zima la Uchukuaji Fomu wa Tundu Lissu wa CHADEMA na ambayo nayasikia yameendelea huko katika Newsrooms ni 'Upumbavu' mtupu.

Sijaona sababu yoyote ile ya Vyombo Vikubwa vya Habari nchini Kupigiwa Simu na hata Waandishi wake 'Kutishwa' hasa kama wakipeleka Hewani ( kama haya Madai ni ya kweli kwani sijayathibitisha bado ) Habari za hili Tukio zima, lakini kinachonisikitisha tu ni kwamba Serikali yangu ya CCM imefanya mengi na makubwa kwa miaka hii Mitano sasa iweje leo hii imuogope Tundu Lissu hivi?

Najua kuwa Tundu Lissu ( Mtani wangu huyu kutoka Mkoani Singida nae ana Changamoto zake ) ila binafsi nilidhani njia pekee ya 'Kummaliza' Kisiasa ni Sisi wana CCM na Serikali yetu Kumuonyesha kwa Vitendo 'Maendeleo' tuliyoyafanya na siyo 'Kumuogopa' hivi hadi kumfanyia 'Mizengwe' ili Tukio zima la leo lisiwe Masikioni mwa Watu ( Watanzania ) tukidhani kuwa labda ndiyo tutamuweza.

Wala haiitaji 'Akili' kubwa kujua ya kwamba kadri Mamlaka husika iliyo chini ya Chama changu Tawala cha CCM kinavyopambana kutaka 'Kumzima' Kisiasa na Kiumaarufu hivi Tundu Lissu kwa 'Kuwatishia' Wanahabari na Vyombo vyao basi ijue ya kwamba ndiyo inasaidia mno Kumuongezea 'Umaarufu' wako na hapa kuna 'Athari' nyingi tu kwa upande wa Kura CCM yangu itazipata.

Halafu Wiki iliyoisha tulikuwa tunamsifu na kumpamba kweli kweli Nguli wa Habari nchini na Mwandamizi kabisa Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa kwamba alipenda 'Demokrasia' na hakuwa na 'Mabavu' dhidi ya Wapinzani. Je, huu 'Upumbavu' uliofanywa leo wa 'Kuvitishia' Vyomba vya Habari Vikubwa nchini 'Visiripoti' Tukio la Lissu ndiyo Kumuenzi Mkapa?

CCM yangu naipenda, Rais na Mwenyekiti wangu Dkt. Magufuli namkubali sana hata Mwenyezi Mungu anajua ila huu 'Upuuzi' mkubwa sijaupenda.
Uliza vizuri
Chadema wamelipia shilingi ngapi?
Au utopolo tu
Duniani hakuna vya bure
 
ccm halisi ilikufa baada ya Awamu ya 3 (RIP BWM) yaliyofuata ni magumashi hamna kitu kelele tu
 
Na kibali cha tcra!?????
Watafute mtu aliye nje ya nchi afungue account ya youtube kisha atume "stream key" kwa warusha matangazo waliopo nchini ili watumie "stream key" ya youtube ya nje ya nchi. Kisha baada ya hapo ni kuwashauri watu wasubscribe na kushare. Tcra mwisho wao ni hapo Namanga hawana uwezo wa kuzuia youtube account ya nje ya nchi kufanya kazi bongo.

Sheria haijazungumzia juu ya stream key sharing na credential livestreaming rtmp server and video encoding latency keys. Kwa hiyo bado nafasi ipo ya kushare stream key.
Labda wazime internet muda wote wa uchaguzi.
 
Licha ya media kuzuiwa chadema ilishindwa Nini kuanzisha online media, page zao na kutoa habari, maana jinsi wanavobanwa na ccm kuachwa wanapigwa gape, atleast wangerusha tukio kwenye account za CDM kusubiria huruma tu watasanda, CCM imechokwa ni vile inajipa promo

Chadema walilipia airtime wakakataliwa?
 
Genta my brother, I’m sorry to tell you that this year is the LAST YEAR FOR CCM to lead Tanzania.

Mark my words. Huu ndo mwaka wa mwisho kuongoza Tanzania. From October nchi inaenda kuwa chini ya Chadema.

Nimesikiliza kwa Makini sana hotuba ya Mzee Butiku jana kwenye mkutano wa NCCR. Kuna ujumbe aliutuma kwa TISS, Polisi, JWTZ na NEC . Kwa nilivyomsikia nimejiridhisha kuwa wazee wenye maamuzi yao waneridhia nchi kwenda upinzani mwaka huu.

Tukutane October ndugu yangu Genta!!

Kweli vichaa mko wengi sana.

Tar 15 tukutane taifa ili kuona maandalizi ya kampeni kupitia wasanii 109 watakaosambaa nchi nzima kuanzia tar 27 agositi.
 
Back
Top Bottom