Je hi inathibitisha dunia (Earth) siyo tufe (sphere)?

Je hi inathibitisha dunia (Earth) siyo tufe (sphere)?

Wote tuko sahihi kuanzia Mleta uzi mpaka sisi wachangiaji. Tena kupingana na kukosoana huku ndio kuna uonesha usahihi wa mawazo yetu mazuri.

ila mimi nina maswali naomba nisaidiwe majibu na yeyote humu.

Je Bila kufindishwa/kujulishwa kuwa dunia ni mviringo, sisi wenyewe tusingejua?

Kama mwanzo tungefundishwa dunia ni tambarate mfano wa sahani au disc, tungetumia hoja gani kupinga hilo?

Na hapo ulipo wewe mwenyewe na mazingira yakuzungukayo unajiona upo ktk uduara au utambarare wa dunia?

Na mwisho, wanaompinga mleta uzi wanajua usiku na mchana au majira ya mwaka yanavyopatikana katika dunia ni flat/tambarare? Kama hawajui je wana haki ya kumpinga?

Mleta uzi anapinga yale tunayoyajua so nae apingwe kwa kuyakanusha anayoyajua yeye.
Mkuu nilikuwa napitia kitabu Cha Steven Hawking Cha A brief history of time.Ni kweli tumefundishwa dunia ni duara lakini hapo zamani kabla ya Mwaka 1609 walikuwa wanafundishwa dunia ni flat.Mpaka walipotokea wanasayansi Ptolemy na Galilleo.

Watu wa zamani waliamini dunia ndio ilikuwa center of the universe.The sun,moon,fixed stars and the five known planets at that time(Mercury,mars,Venus,Jupiter and suturn) were believed to move arround the earth.Lakini up to date mambo yamebadilika

Hatuzaliwi tukiwa tunajua vitu ila tunafundishwa ili tujue.Cha msingi ni kujua je unachofundishwa ndio ukweli.Kuna evidences kibao zinazothibitisha dunia duara.
 
Sababu moja kubwa inatokea hapa ni kuzima kwa kufifia siyo ya kwamba linazima ghafla kama Bulb, hivyo kufanya concentration yako kupungua.
Hapana kadri unavyozidi kwenda juu zaidi na kwa spidi sahihi unaliona likizama tena na tena mpaka utakapofanikiwa kutoka nje ya layer ya dunia ukajitenga na layer hiyo ndipo utakapoliona kwa uhalisia wake. Jaribu siku moja, kaa chini lala likizama simama ghafla likizama panda mpaka ghorofa kadhaa, likizama panda zaidi nenda juu kadri unavyoweza utathibitisha hili. uzingatie kasi maana ukichelewa hutalikuta. Lingekuwa ninafifia basi kusingekuwa na ulazima wa kuzama, kwanini lizame? Ukiwa ardhini, ukawa na chombo ambacho kina spidi inayotosha kukimbizana na mzunguko wa dunia, na pia mazingira ya chombo hicho yaruhusu kukimbizana na kuzama kwake basi katika safari yako hiyo jua litakuwa likizama wakati wote. Ukiwa na kasi zaidi basi utaukuta mchana na ukichelewa usiku utakukuta wewe. ukiwa constant basi jua litakuwa likizama wakati wote. Fanya uchunguzi kuhusu terminator line utagundua kwanini jua halizimi bali dunia ndo ina hama hama upande pale inapozunguka.

Tazama kwenye video hii kuna ndege moja mwishoni mwa video ipo through terminator line
 
Sababu ya kutumia JUA ni wengi waelewe maana tayari wamefanya mapokeo ya JUA hivyo huona hamna wingi.
-
Njia za kisayansi mnazoamini naona zina utata endapo ukivua ushabiki na kukaririshwa, katika uhalisia na fikra Jua hilo mnalo amini ni moja na limesimama 'position moja' lina utata katika dira/nafasi yake.
Ukifualia utaona sio kila siku linachomoza mashariki kuelekea magharibi kuna wakati huchomoza Kuskazini-Mashariki na huishia Kusini-Magharibi hivyo inaondoa uhalisia huo maana halina consistency. Lakini kwa kutumia direction hiyo hiyo utaona inawezekana sio JUA tena ni maJUA hupishana na kusababisha kupoteza uelekeo.
Hapo ndio ujue dunia inazunguka jua
 
Hapana sio kila kinazunguka na Flat Bense Earth haizungukia bali baadhi ya vitu ndivyo uzunguka.
-
Hali ya Hewa
Kiuhalisia JUA linalokuwa zamu linapozima (huzima kwa kififia/kupungua) kuna nyakati huzima na kutonesha dalili na mara nyingine hubakiza dalili ya kuwaka. 'Unaweza kuona nyakati mbingu hubakia na hali ya uwekundu au mwanga jua'
Hivyo endapo halitozima moja kwa moja joto lazima hutokea. Je kwanini kuna maeneo joto uwepo siku zote/mara nyingi mfano Dar? Hapa ikumbukwe linapozima huanza safari ya kurudi makao makuu na wakati huo makao makuu kuna Jua hutumwa kuja, hivyo jua hili linalokuwa linarudi makao makuu hujikuta kila wakati lipo katika eneo hilo (ukanda huo) mfano Dar na Middle East.
-
Mvua
Ikumbukwe Flat Bense Earth ina boundary iliyochongwa kama rainbow inazuia pembe na pembe huku imeninginia angani, mvuke na moshi huenda na kujikusanya hapo juu na inafika wakati hulainika na kuwa maji na kurudi ardhini.
-
Upepo
Hapa bado nafanya tafiti. Lakini uchunguzi wa awali unaonyesha kuna kitu kimepewa jukumu la kutoa/puliza upepo, na inaonyesha kinavyopata nguvu ndivyo upepo huwa wa Kasi na mkubwa na endapo huchoka basi upepo upungua.
Hapa mkuu unanipoteza zaidi. Hebu fafanua vizuri sehemu ya Jua
1. Kuna ma Jua mangapi?
2. Likizima linarudi wapi? Linazima kwa mechanism gani?
3. Umesema likizima linarudi makao makuu, na lingine linatumwa, Je yanapishana wapi?
Aisee umenipa maswali mengi sana mkuu
 
Hapana kadri unavyozidi kwenda juu zaidi na kwa spidi sahihi unaliona likizama tena na tena mpaka utakapofanikiwa kutoka nje ya layer ya dunia ukajitenga na layer hiyo ndipo utakapoliona kwa uhalisia wake. Jaribu siku moja, kaa chini lala likizama simama ghafla likizama panda mpaka ghorofa kadhaa, likizama panda zaidi nenda juu kadri unavyoweza utathibitisha hili. uzingatie kasi maana ukichelewa hutalikuta. Lingekuwa ninafifia basi kusingekuwa na ulazima wa kuzama, kwanini lizame? Ukiwa ardhini, ukawa na chombo ambacho kina spidi inayotosha kukimbizana na mzunguko wa dunia, na pia mazingira ya chombo hicho yaruhusu kukimbizana na kuzama kwake basi katika safari yako hiyo jua litakuwa likizama wakati wote. Ukiwa na kasi zaidi basi utaukuta mchana na ukichelewa usiku utakukuta wewe. ukiwa constant basi jua litakuwa likizama wakati wote. Fanya uchunguzi kuhusu terminator line utagundua kwanini jua halizimi bali dunia ndo ina hama hama upande pale inapozunguka.
Tazama kwenye video hii kuna ndege moja mwishoni mwa video ipo through terminator line

"Jaribu siku moja, kaa chini lala likizama simama ghafla likizama panda mpaka ghorofa kadhaa, likizama panda zaidi nenda juu kadri unavyoweza utathibitisha hili. uzingatie kasi maana ukichelewa hutalikuta."
Hapa kuna kitu nakifahamu na ushahidi pia lakini nashindwa nikuelezee vipi ningelikuwa na uwezo ningeomba kipindi kwa TV au tukutane nikuoneshe hayo mambo physicality.
 
Ok Boss. Nakutakia kila la heri kama ni kweli siku moja watu tukuelewe au atokee atakayekusaidia tuelewe au wewe uelewe. Yote heri
 
Hapa mkuu unanipoteza zaidi. Hebu fafanua vizuri sehemu ya Jua
1. Kuna ma Jua mangapi?
2. Likizima linarudi wapi? Linazima kwa mechanism gani?
3. Umesema likizima linarudi makao makuu, na lingine linatumwa, Je yanapishana wapi?
Aisee umenipa maswali mengi sana mkuu
ma Jua niliyogundua hadi sasa ni matatu lakini niliemshirikisha anasema yanaweza kuwa matano hadi zaidi.

Likizama linakuwa western side linaanza kurudi Eastern side (right hand side panapopatikana muumba) dimension na distance yanakuwa sawa kwamba likizima la western linawaka la eastern hivyo usiku uingia western na mchana huonekana eastern.

Linazima kwa kufifia/kupungua (Kuchanua) mwanga sio kwa mshtuko kama taa.
 
Unauhakika upi juu ya longitude na latitude ilhali ni hao NASA wamekupangia na kukutaarifu?
Mleta hoja wewe una uhakika gani na muda (kwa maana ya masaa toka sehemu moja kwenda nyingine kama ulivyooridhesha kwenye uzi wako - maana hata hayo masaa unayosema toka point moja kwenda nyingine tumepangiwa tu ) hata kwa maana ya direction (east, west , north, south pia tumepangiwa tu kama unavyosema) wewe unapata wapi uhalali wa kupingana na NASA wakati hata facts na evidence unazotumia nyingi ni za kupanga tu na pengine huna namna ya kuthibitisha ....
 
Sawasawa.. je watu wa mwanzo walioamini ni flati walikaa wakakubaliana kuwa sasa tuamini ni mviringo au watu walikuja na hoja za dunia ni mviringo waliweza kueneza hoja zao kuzidi wanaoamini ni flat?

Unazani kwanini hatufundishwi hoja za walioamini ni flat mashuleni ili kuthibitisha kuwa walikuwa wrong.?
Mkuu nilikuwa napitia kitabu Cha Steven Hawking Cha A brief history of time.Ni kweli tumefundishwa dunia ni duara lakini hapo zamani kabla ya Mwaka 1609 walikuwa wanafundishwa dunia ni flat.Mpaka walipotokea wanasayansi Ptolemy na Galilleo.

Watu wa zamani waliamini dunia ndio ilikuwa center of the universe.The sun,moon,fixed stars and the five known planets at that time(Mercury,mars,Venus,Jupiter and suturn) were believed to move arround the earth.Lakini up to date mambo yamebadilika

Hatuzaliwi tukiwa tunajua vitu ila tunafundishwa ili tujue.Cha msingi ni kujua je unachofundishwa ndio ukweli.Kuna evidences kibao zinazothibitisha dunia duara.
 
Na hapa tukitumia uanasayansi ndio tutapotezana kabisa coz tulissoma kukalili tuliowengi hivyo kuzipata hoja za kisayansi matokeo yake ndio hivyo itatubidi tuamini tuu maan ukipinga na wewe utaambiw onesh sayansi yako. Kwa hilo tupo pamoja.

Ila kama unasoma soma na kuangalia video kuhusu shape ya dunia, jitahidi soma soma na angalia video za wanasayansi wa hiyo hiyo shpe ya dunia ila wanaoamini ni tambarare. Kisha linganisha hoja zao bila kusema hoja zao hazina mashiko.

Halafu tuwaze pia nje ya hizo hoja za wanasayansi, wewe kama wewe unaona upo katika ardhi ya hali gani, mviringo au tambarare?
Pia kati ya jua na dunia kipi ambacho una ushahidi wakukiona wewe mwenyewe kikitembea?

Sijampinga popote wala sijamwambia kakurupuka. Sanasana nimemtakia kila la heri kwenye utafiti wake. Mm si mwanasayansi boss zaidi ya kusoma soma na kuangalia videos za wanasayansi sina namna nyingine ya kumpinga. Halafu wapo binadamu wengi sana waliamini na wanaamini dunia si mduara, tangu miaka ya 80's wapo sema hoja zao zina ukakasi mwingi sana ukilinganisha na wanasayansi wanaosema ni duara na uthibitisho wanaoutoa. uzuri kwa sasa binadamu Tuna teknolojia nzuri sana kuthibitisha umbile la dunia.
 
Mleta hoja wewe una uhakika gani na muda (kwa maana ya masaa toka sehemu moja kwenda nyingine kama ulivyooridhesha kwenye uzi wako - maana hata hayo masaa unayosema toka point moja kwenda nyingine tumepangiwa tu ) hata kwa maana ya direction (east, west , north, south pia tumepangiwa tu kama unavyosema) wewe unapata wapi uhalali wa kupingana na NASA wakati hata facts na evidence unazotumia nyingi ni za kupanga tu na pengine huna namna ya kuthibitisha ....
Muda niliotumia nimakisio yatokanayo na Natural Intelligence 'NI' ambayo ipo driven by Spirit, Will na Desire.
Ukiwa na Natural Spirit (Spiritual) unaweza kupata hisia ya mambo.

Nakumbuka kipindi nasoma niliwahi kuamka saa mbili asubuhi (kwa saa tunazotumia) lakini nilijihi sijachelewa bali dunia ndio umewahi.
Kipindi naelekea Bus Station niliona pilika na watu wengi wakiwahi kazini na maeneo mbalimbali hata shuleni pia walimu na wanafunzi walionekana kuchelewa lakini hapa niligundua hamna consistency ya muda, usiku na mchana yani vinapishana (Muda ndio unaweka logic ya hali husika)

Kinachoshangaza nikifumba macho na kufikiri najihisi niliwahi kuwepo kwenye miaka ya 1910 wakati nimezaliwa 2000.
 
Kwa vipindi tofauti nimekuwa nikipingana na NASA na allies wake 'JF Wamejaa' ya kuwa dunia haina umbo la tufe 'Spherical Shape' kama tunavyoaminishwa, kufundishwa na kukaririshwa.

Huku nikieleza ya kuwa dunia ni ubapa uliokuwa na bonde kidogo nikitolea mfano sahani maalum zilizotengenezwa kwa plastiki nyepesi na hutumiwa sana katika hafla, sherehe au misiba kwa ajiri ya chakula. (Recyclable Plastic Plates)

Zifuatazo ni tafiti na mifano juu ya utafiti huu wa dunia ya tufe (Sphere) vs dunia ubapa (Flat Bense);-
- Kama dunia ni sphere kweli basi US amekaribiana na Russia Federation kwa ukaribu wa Anchorage, Alaska - US kwa Anadyr, Verkhoyansk - Russia Federation wakitenganishwa na Chukchi Sea kwa upande wa mashariki na Bering Sea kwa upande wa magharibi. (Kama tunavyo aminishwa) Kijiografia naweza kutumia mfano wa Kigali, Rwanda na Bukoba, Tanzania umbali uliokuwepo kutoka Anchorage, Alaska hadi Anadyr, Verkhoyansk unatumia masaa 5+ ilhali Kigali hadi Bukoba ni dakika 45 arobaini tano hadi saa 1 moja. Kama kweli dunia ni duara/sphere Anchorage hadi Anadyr ilitakiwa itumike saa 1 moja. *Usafiri wa ndege

- Zanzibar na Comoros, dunia hii ya NASA na allies wake inaonyesha Comoros imepakana na Palma katika rasi ya Cape Delgado ikumbukwe Palma imekaribiana na Mtwara unaweza kusema ni Dar es Salaam City Center hadi Bagamoyo pia tambua Dar imepakana na Zanzibar ikitenganishwa kwa maji. Kinachoshangaza Zanzibar (Urban West) wao hufika Comoros kwa muda mfupi kuliko Palma waliotenganishwa na Comoros kwa Cape Delgado (According to NASA). Ukistajaabu ya Sphere utayaona ya Sufuria hapa....

- Ndege (Aero) kupaa kwa kufuata Northern-Eastern direction. Kama dunia ni sphere itakuwaje Ndege isafiri kwa direction hiyo ikufuata upepeo na mawingu makali yanayotoka upande wa mashariki?!

- Nile kutoka Ziwa Victoria kuelekea Midteranean Sea, Uele River kutoka Central Africa Rep. Kuleta Victoria na Kagera River kutoa Victoria kupeleka Lake Tanganyika, Kalemie kutoa Tanganyika kupeleka Atlantic Ocean. Aiseee hapa hadi uchanganyikiwe ndio uelewe

- Kutoka Sekondi - Takoradi, Ghana (Gulf of Guinea) ambayo ni North Western Africa hadi Port Gentil, Gabon ambayo ni Central Western Africa ni sawa kutoka Dar es Salaam Eastern Africa hadi hapo Port Gentil lakini anayetoka Sekondi - Takoradi anitafuta Port Gentil kwa kupanda yani North East ilhali mwanaume wa Dar anapanda kwa North East direction. Haki ya Ngowi NASA wanaumbuka zamu hii

- Ukiwa Copenhagen (Københavin) Canton ya Odense Zealand kwa Jon Stefano ni karibu sana kufika Malmö au Helsingborg yani Copenhagen ni Ilala na Malmö ni Kigamboni kinachoshangaza mtu anayetoka Cuxhaven kuelekea Copenhagen anaelekea North East huyo huyo anayetoka Cuxhaven kuelekea Helsingborg anakuwa anaelekea North West, lakini NASA wametumianisha hawa Copenhagen, Helsingborg na Malmö wote wapo East. *Cuxhaven amesimama kama Kisarawe

- Persian Gulf sasa hapa NASA tuwashike kidole jichoni, Hawa na NASA wanadai dunia ni sphere na Middle East indaiwa kuwa kama mlivoaminishwa, Je Meli hii ya US yenye jina la mtu inapita wapi kufika Strait of Hormuz?!

Mambo ni mengi lakini nimechoka kuandika, Kwanza tuchambue haya.

BA in Geouniorld! [emoji23]
Naunga mkono hoja. The earth is a flat, round surface and is sorrounded by an ice wall on all sides. The sun and the moon are all in the earth's atmosphere
 
Naunga mkono hoja. The earth is a flat, round surface and is sorrounded by an ice wall on all sides. The sun and the moon are all in the earth's atmosphere
Ndio kaka, hii itadhihirika endapo watu wengi waliokaririshwa wakiachiwa huru.
 
Ndio kaka, hii itadhihirika endapo watu wengi waliokaririshwa wakiachiwa huru.
Kabisa kaka. Nasa ni chombo kinachotumika kimkakati na satanic elites kudeceive humanity na kuharakisha usimikwaji wa new world order through "space" propaganda

"real" aliens do not exist. Aliens is another name for demons. Siku nasa
 
Kuna mambo mengi MUHIMU ulimwengu umefungwa kwa kisingizio cha elimu. Ndio elimu ni muhimu lakini isitumike kudanganya na kuendesha watu kwa matakwa binafsi.
 
Sawasawa.. je watu wa mwanzo walioamini ni flati walikaa wakakubaliana kuwa sasa tuamini ni mviringo au watu walikuja na hoja za dunia ni mviringo waliweza kueneza hoja zao kuzidi wanaoamini ni flat?

Unazani kwanini hatufundishwi hoja za walioamini ni flat mashuleni ili kuthibitisha kuwa walikuwa wrong.?
Mambo haya yana historia ndefu kidogo.Kuna kipindi mwanasayansi wa Uingereza Bentrad Russell alikuwa akitoa somo kuhusiana na astronomy jinsi dunia inavyozunguka jua,Lakini pia jua linavyoizunguka milk way galaxy.Mwanamke mmoja alisimama akambishia akamwambia "dunia ni flat ipo imelala kwenye mgongo wa Kobe mmoja mkubwa" Bentrad Russell alitabasamu halafu akamuuliza "je huyo Kobe yupo kwenye Nini" mwanamke yule alishindwa kujibu ikabidi amsifie Russell kwamba ana akili nyingi.

Aristotle inawezekana ndiye alikuwa mwanafalsafa maarufu wa Kwanza kusema dunia ilikuwa ni duara hii yote ni kwa sababu aliona kivuri Cha dunia kinakuwa duara mwezini kipindi Cha lunar eclipse.Lakini suala hili aliliacha Kama assumption kutokana na mambo ya imani walivyokuwa wanaamini na miungu yao ya Kigiriki.

Corpenicus miaka ya 1500's mwenyewe alikuja na assumption za dunia kulizunguka jua lakini aliogopa kanisa la Roma.Maana imani iliamini dunia ipo katikati na inazungukwa.

Ptolemy na Gallileo ndio walisimama imara kutetea hizo assumption za dunia kuwa duara na inalizunguka jua.Wakatoa mpaka na evidences za kuthibitisha.Wote tunajua mabaya yaliyomkuta Gallileo kutokana na kwenda kinyume na kanisa lilivyoamini.

Hapo utaona mitazamo mingi ya dunia kuwa flat ilikuwa kwa sababu za kiimani tu lakini sio kwa fact za kisayansi.Ndio maana hawakuwa na uthibitisho wowote Kama waliotoa wanasayansi zaidi ya imani.

Ukisema tufundishwe darasani kwa nini waliamini ni flat mimi binafsi naona hakuna sababu ya kufundishwa hayo.Huwezi ukafundisha imani kwenye somo la sayansi.Haya mambo darasani yanafundishwa kwenye masomo ya sayansi hivyo darasani ni lazima tufundishwe sayansi.Imani itafundishwa sehemu zake Kama huko kanisani na misikitini.
 
Kabisa kaka. Nasa ni chombo kinachotumika kimkakati na satanic elites kudeceive humanity na kuharakisha usimikwaji wa new world order through "space" propaganda

"real" aliens do not exist. Aliens is another name for demons. Siku nasa
I think religion deceives more than Nasa
 
Back
Top Bottom