Je hi inathibitisha dunia (Earth) siyo tufe (sphere)?

Je hi inathibitisha dunia (Earth) siyo tufe (sphere)?

Dah! Uzi huu ni Ushahidi mkubwa kwamba kuna Walimu walipata Tabu sana kufundisha...![emoji35][emoji35]
 
Mtoa mada pole sana kwa umbumbumbu uliozidi kipimo !! Unasikitisha SANA!!!! Yaani hata elimu ya msingi ya jiografia au basi form one na two hukupita ukaona dunia iliyochorwa kwenye tufe na jinsi Urusi kaskazini ilivyo karibu na America ya kaskazini (Alaska)? Nenda kwenye duka la stationery waambie wakuonyeshe (au kama una hela wakuuzie) tufe la dunia la kufundishia jiografia. Kama dunia ingekuwa flat ndege inayoruka kutoka nchi iliyoko mwishoni si ingeanguka huko ambako hakuna nchi ?
Kama mimi ni mbumbumbu basi wewe ni nomenclature.
Zee la hekima kabisa linasema elimu ya msingi na.... (Kwa kubana pua)
Unauhakika gani na hayo mafundisho? Hivi nikianza kufundisha humu JF kwamba ZEE LA HEKIMA na ngarawa utaafiki? Kama hutoafiki ni kwanini?

Hivi unajua kuna zuio ' Boundary ' katika Flat Bense Earth na Earth.
 
Hapa nina swali. Kama dunia ni sahani au kama ulivyosema,huu usiku na mchana tunaupataje ?
Soma kwa makini,
Jua siyo moja yapo takribani matatu hadi matano. Jua haya huzima yafikapo magharibi na kuanza kurudi mashariki huku lile la mashariki uwaka na kuanza kuja magharibi ni maisha ya viumbe hivi vyenye furaha katika kila siku.

Mwezi ni mraba wa LED (mfano wa bracelets za mraba ziwakazo wakati wa kiza) ambavyo mwezi huwezi kuonesha mwanga wake halisi wakati wa jua. Uonekana pale jua linapozima.

Nyota ni moja kubwa Sana miale yake ndizo hizi nyota tuonazo.
 
Dah! Uzi huu ni Ushahidi mkubwa kwamba kuna Walimu walipata Tabu sana kufundisha...![emoji35][emoji35]
Huu ni ushahidi walimu walipata wepesi wa kukaririsha na kulisha watu uongo mfano mmoja wapo ni wewe.
 
Soma kwa makini,
Jua siyo moja yapo takribani matatu hadi matano. Jua haya huzima yafikapo magharibi na kuanza kurudi mashariki huku lile la mashariki uwaka na kuanza kuja magharibi ni maisha ya viumbe hivi vyenye furaha katika kila siku.

Mwezi ni mraba wa LED (mfano wa bracelets za mraba ziwakazo wakati wa kiza) ambavyo mwezi huwezi kuonesha mwanga wake halisi wakati wa jua. Uonekana pale jua linapozima.

Nyota ni moja kubwa Sana miale yake ndizo hizi nyota tuonazo.

Hapa kazi ipo aisee.
 
mtoa mada haeleweki!! uchizi unaanzaga mdo mdo

Unajua ukishamjua mtu,hupati tabu. Unajua bora ujadiliane na wajuzi mia moja unaweza kuwashinda kwa hoja na ukapata faida kuliko kujadiliana na mjinga moja lazima atakushinda tu,hutafaidika na chochote na utapoteza muda. Huyu mtoa mada post yake namba 63 imenifanya nisiendelee kumuuliza tena maswali sababu najua kitakacho fata ni muendelezo wa uhayawani wake.

Endeleeni nae wadau......
 
Kila mmoja hujiona yeye ni bora na yupo sahihi. Amini wakati utayaleta haya yote
 
Post yako namba 63,imenifanya nisiendelee kukuhoji wala kujadiliana na wewe.
Wadau wataendelea na wewe...!
Nipo ....
Unavyoniona sipo sahihi ndivyo naona haupo sahihi pia.
 
Unavyoniona sipo sahihi ndivyo naona haupo sahihi pia.

Poa. Tatizo unakosea mpaka kwenye lugha.

Unajua mara nyingi tukikosa majibu katika njia fulani,huwa tunarejea kwenye lugha.

Ulichokiandika post #63 hata lugha yenyewe inakataa ila ukalazimisha.

Lugha gani inakubali wingi wa JUA ? Na sentensi ikakaa ikaleta maana ?

Pili inaonekana hamna uhakika wa idadi ya JUA. Kusema " ....matatu mpaka matano..." hii inatia shaka.

Lakini swali la msingi ni kuwa,mmejuaje kuna idadi zaidi ya moja ? Sababu njia za kisayansi tunazijua.
 
Wote tuko sahihi kuanzia Mleta uzi mpaka sisi wachangiaji. Tena kupingana na kukosoana huku ndio kuna uonesha usahihi wa mawazo yetu mazuri.

ila mimi nina maswali naomba nisaidiwe majibu na yeyote humu.

Je Bila kufindishwa/kujulishwa kuwa dunia ni mviringo, sisi wenyewe tusingejua?

Kama mwanzo tungefundishwa dunia ni tambarate mfano wa sahani au disc, tungetumia hoja gani kupinga hilo?

Na hapo ulipo wewe mwenyewe na mazingira yakuzungukayo unajiona upo ktk uduara au utambarare wa dunia?

Na mwisho, wanaompinga mleta uzi wanajua usiku na mchana au majira ya mwaka yanavyopatikana katika dunia ni flat/tambarare? Kama hawajui je wana haki ya kumpinga?

Mleta uzi anapinga yale tunayoyajua so nae apingwe kwa kuyakanusha anayoyajua yeye.
 
Nikutakie kila la heri maana safari uliyonayo kitafiti ni ndefu sana. Ila nikupe changamoto ndogo tu, Kuna picha NASA waliiachia July 6, 2015 umeshaiona? ina umbile la sinia au sahani iliyochimbika au mduara? Tuendelee kuelimishana.
 
Poa. Tatizo unakosea mpaka kwenye lugha.
Unajua mara nyingi tukikosa majibu katika njia fulani,huwa tunarejea kwenye lugha.
Ulichokiandika post #63 hata lugha yenyewe inakataa ila ukalazimisha.
Lugha gani inakubali wingi wa JUA ? Na sentensi ikakaa ikaleta maana ?
Pili inaonekana hamna uhakika wa idadi ya JUA. Kusema " ....matatu mpaka matano..." hii inatia shaka.
Lakini swali la msingi ni kuwa,mmejuaje kuna idadi zaidi ya moja ? Sababu njia za kisayansi tunazijua.
Sababu ya kutumia JUA ni wengi waelewe maana tayari wamefanya mapokeo ya JUA hivyo huona hamna wingi.
-
Njia za kisayansi mnazoamini naona zina utata endapo ukivua ushabiki na kukaririshwa, katika uhalisia na fikra Jua hilo mnalo amini ni moja na limesimama 'position moja' lina utata katika dira/nafasi yake.
Ukifualia utaona sio kila siku linachomoza mashariki kuelekea magharibi kuna wakati huchomoza Kuskazini-Mashariki na huishia Kusini-Magharibi hivyo inaondoa uhalisia huo maana halina consistency. Lakini kwa kutumia direction hiyo hiyo utaona inawezekana sio JUA tena ni maJUA hupishana na kusababisha kupoteza uelekeo.
 
Wote tuko sahihi kuanzia Mleta uzi mpaka sisi wachangiaji. Tena kupingana na kukosoana huku ndio kuna uonesha usahihi wa mawazo yetu mazuri.

ila mimi nina maswali naomba nisaidiwe majibu na yeyote humu.

Je Bila kufindishwa/kujulishwa kuwa dunia ni mviringo, sisi wenyewe tusingejua?

Kama mwanzo tungefundishwa dunia ni tambarate mfano wa sahani au disc, tungetumia hoja gani kupinga hilo?

Na hapo ulipo wewe mwenyewe na mazingira yakuzungukayo unajiona upo ktk uduara au utambarare wa dunia?

Na mwisho, wanaompinga mleta uzi wanajua usiku na mchana au majira ya mwaka yanavyopatikana katika dunia ni flat/tambarare? Kama hawajui je wana haki ya kumpinga?

Mleta uzi anapinga yale tunayoyajua so nae apingwe kwa kuyakanusha anayoyajua yeye.
Kuna line inatenganisha usiku na mchana inaitwa terminator line. Natamani kujua kwenye ulimwengu ulio kama sahani kama huu mstari utakuwa straight line au curved. Halafu na mwezi je? nao una umbile gani? unazunguka dunia kinyume nyume au kimbelembele au unapita juu chini juu chini?
 
Kwa vipindi tofauti nimekuwa nikipingana na NASA na allies wake 'JF Wamejaa' ya kuwa dunia haina umbo la tufe 'Spherical Shape' kama tunavyoaminishwa, kufundishwa na kukaririshwa.

Huku nikieleza ya kuwa dunia ni ubapa uliokuwa na bonde kidogo nikitolea mfano sahani maalum zilizotengenezwa kwa plastiki nyepesi na hutumiwa sana katika hafla, sherehe au misiba kwa ajiri ya chakula. (Recyclable Plastic Plates)

Zifuatazo ni tafiti na mifano juu ya utafiti huu wa dunia ya tufe (Sphere) vs dunia ubapa (Flat Bense);-
- Kama dunia ni sphere kweli basi US amekaribiana na Russia Federation kwa ukaribu wa Anchorage, Alaska - US kwa Anadyr, Verkhoyansk - Russia Federation wakitenganishwa na Chukchi Sea kwa upande wa mashariki na Bering Sea kwa upande wa magharibi. (Kama tunavyo aminishwa) Kijiografia naweza kutumia mfano wa Kigali, Rwanda na Bukoba, Tanzania umbali uliokuwepo kutoka Anchorage, Alaska hadi Anadyr, Verkhoyansk unatumia masaa 5+ ilhali Kigali hadi Bukoba ni dakika 45 arobaini tano hadi saa 1 moja. Kama kweli dunia ni duara/sphere Anchorage hadi Anadyr ilitakiwa itumike saa 1 moja. *Usafiri wa ndege

- Zanzibar na Comoros, dunia hii ya NASA na allies wake inaonyesha Comoros imepakana na Palma katika rasi ya Cape Delgado ikumbukwe Palma imekaribiana na Mtwara unaweza kusema ni Dar es Salaam City Center hadi Bagamoyo pia tambua Dar imepakana na Zanzibar ikitenganishwa kwa maji. Kinachoshangaza Zanzibar (Urban West) wao hufika Comoros kwa muda mfupi kuliko Palma waliotenganishwa na Comoros kwa Cape Delgado (According to NASA). Ukistajaabu ya Sphere utayaona ya Sufuria hapa....

- Ndege (Aero) kupaa kwa kufuata Northern-Eastern direction. Kama dunia ni sphere itakuwaje Ndege isafiri kwa direction hiyo ikufuata upepeo na mawingu makali yanayotoka upande wa mashariki?!

- Nile kutoka Ziwa Victoria kuelekea Midteranean Sea, Uele River kutoka Central Africa Rep. Kuleta Victoria na Kagera River kutoa Victoria kupeleka Lake Tanganyika, Kalemie kutoa Tanganyika kupeleka Atlantic Ocean. Aiseee hapa hadi uchanganyikiwe ndio uelewe

- Kutoka Sekondi - Takoradi, Ghana (Gulf of Guinea) ambayo ni North Western Africa hadi Port Gentil, Gabon ambayo ni Central Western Africa ni sawa kutoka Dar es Salaam Eastern Africa hadi hapo Port Gentil lakini anayetoka Sekondi - Takoradi anitafuta Port Gentil kwa kupanda yani North East ilhali mwanaume wa Dar anapanda kwa North East direction. Haki ya Ngowi NASA wanaumbuka zamu hii

- Ukiwa Copenhagen (Københavin) Canton ya Odense Zealand kwa Jon Stefano ni karibu sana kufika Malmö au Helsingborg yani Copenhagen ni Ilala na Malmö ni Kigamboni kinachoshangaza mtu anayetoka Cuxhaven kuelekea Copenhagen anaelekea North East huyo huyo anayetoka Cuxhaven kuelekea Helsingborg anakuwa anaelekea North West, lakini NASA wametumianisha hawa Copenhagen, Helsingborg na Malmö wote wapo East. *Cuxhaven amesimama kama Kisarawe

- Persian Gulf sasa hapa NASA tuwashike kidole jichoni, Hawa na NASA wanadai dunia ni sphere na Middle East indaiwa kuwa kama mlivoaminishwa, Je Meli hii ya US yenye jina la mtu inapita wapi kufika Strait of Hormuz?!

Mambo ni mengi lakini nimechoka kuandika, Kwanza tuchambue haya.

BA in Geouniorld! [emoji23]
Fanya tafiti zako usije na tafiti za watu kutudanganya
 
Wote tuko sahihi kuanzia Mleta uzi mpaka sisi wachangiaji. Tena kupingana na kukosoana huku ndio kuna uonesha usahihi wa mawazo yetu mazuri.
ila mimi nina maswali naomba nisaidiwe majibu na yeyote humu.
Je Bila kufindishwa/kujulishwa kuwa dunia ni mviringo, sisi wenyewe tusingejua?
Kama mwanzo tungefundishwa dunia ni tambarate mfano wa sahani au disc, tungetumia hoja gani kupinga hilo?
Na hapo ulipo wewe mwenyewe na mazingira yakuzungukayo unajiona upo ktk uduara au utambarare wa dunia?
Na mwisho, wanaompinga mleta uzi wanajua usiku na mchana au majira ya mwaka yanavyopatikana katika dunia ni flat/tambarare? Kama hawajui je wana haki ya kumpinga?
Mleta uzi anapinga yale tunayoyajua so nae apingwe kwa kuyakanusha anayoyajua yeye.
Hakika umetumia busara.
 
Back
Top Bottom