Je, endapo kumbukumbu zako zote zikafyonzwa na kufutika, kisha ukawekewa kumbukumbu za gaidi, nawe utakuwa gaidi? Au moyo utagoma?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,066
40,725
Ni vyema tukaliweka hili sawa, je, mtu yupo kichwani au moyoni?

Mfano mtoto mdogo wa miaka 12, mwenye tabia nzuri kama malaika, tukaamua kunyonya memory yake na kuifuta kabisa kichwani kwake, kisha tukamjaza memory za gaidi la katili.

Je, huyo mtoto atakuwa yule gaidi kwa kila namna au moyo wa ule mtoto unaweza ukapambana na zile kumbukumbu moya za kimauaji?

Sasa je, mtu yupo wapi hasa, kichwani au moyoni? Na endapo mtoto huyu atafanya mauaji ya kujitoa muhanga, dhambi zitakuwa za nani? Za mwenye kumbukumbu au za mwenye mwili?

Maana inabidi tuassume mwili ni hardware na mawazo/akili/ utashi ni software tu.
 
kwani kazi ya kichwa ni ipi na kazi ya moyo ni ipi?
kwa mantiki hiyo ukishajua utendaji wa kazi zake, basi hata jibu lake utalipata
 
Kwanza tuelewe kijachokufanya wewe uwe wewe sio kumbukumbu. Kumbukumbu ni experience ya uliyoyaona na kutenda au kusikia.
Mtu ni roho na nafsi ndio inayomfanya awe mtu.

Tukumbuke pia huruma, upole, na menginiyo mengi hayaratibiwi na kumbukumbu.. hizo ni tabia za mtu binafsi.
Personalities za binadamu imegawanyika katika sehemu kuu ambazo ni Behaviour,(Tabia) Cognition (Utambuzi),Emotions (Hisia), tutaangalia zaidi Behaviour, tuone tabia mbalimbali za wanadamu

Wanasaikolojia wanasema kuwa Tabia za binaadamu zinasababishwa na Endocrine system
(Mfumo wa tezi) na Nervous System (Mfumo wa Fahamu/Neva). Lakini inasemekana kua mfumo wa Neva ndio husababisha zaidi tabia za mtu, wanasema kwamba Utathabiti au mwenye imfumo imara/thabiti wa neva basi anakua na uwezo mkubwa wa kuweza kujifunza hivyo anaweza kudhibiti tabia zake, labda kutoka tabia moja kwenda nyingine ambazo ni Aggressive, Passive na Assertive

Hivyo basi kama mtu mwenye behavior ya Passive ambazo ni upole akifutwa kumbukumbu zake akawekewa za Aggressive ambazo ni ukorofii/gaidi. Bado mtu huyo hawezi kua gaidi kutokana na kumbukumbu hizo. Ni sawasawa mtu umlazimishe kumvisha nguo za CCM hafu useme tayari mtu huyo sio CDM tena. Kiufupi ni kama utakua umesafisha dumu nje ila ndani bado ni chafu

Hivyo labda Kama wangefuta kumbukumbu afu wakampa madawa ya kuchochea hiyo tezi hapo juu kuzalisha hormones zitakazofanya mtu awe mkorofi. Ndio maana ambacho hua kinafanyika in real life. Hua wanafuta kumbukumbu zako afu wanakuBrainwash kwa mafunzo mbalimbali. Lakini hata hivyo ikitokea kitu kikatriger lost memories za victim basi kumbukumbu zote hurudi. Mara nyingi huwa wanabadirika
 
Ni akili tu ndo hutumika hapo na mtu akikuteka akili hata nafsi inapenda kile kitu,

Jiulize leo vita itokee alafu uende pale udom ukawachukue wale wanafunzi ukawa silaa wakapambane vitani,Ni asilimia ndogo sana watakubali au wasikubali

Ila chukua wajeda uone watakavyoshangilia vzr Sana,maana akili yao tayari imeshakubali kile kitu

Sumu ya ugaidi hulishwa mtu kuanzia akiwa mdogo
 
Kwamba basi tabia zinaweza kua influenced kwa kufuta kumbukumbu za mtu.. kumbuka mtoa mada anaongelea kumbukumbu sio tabia.
 
Kwa mantiki hiyo, mtoto mdogo anapofanyiwa ‘brainwashing’ ili akikua awe gaidi na kwenda kujitoa muhanga, huwa inahusisha kurekebisha utengenezaji wa hormones kwenye tezi zake? Na je, hiyo dhambi ya kujitoa muhanga ni ya nani? Maana it seems huyu mtoto anakuwa kama vessel tu, au robot, unaweza kumuadhibu robot au utamuadhibu yule aliye - programme lile robot? Na consequently, ni haki kwa binadamu kuadhibiwa wakati aliyetu-programme yupo na wote tunamjua?
 
Binaadamu hayupo programed unless otherwise hujui maaa sahihi ya programming au unashindwa kuihusianisha na Creation.
 
Binaadamu hayupo programed unless otherwise hujui maaa sahihi ya programming au unashindwa kuihusianisha na Creation.
Nipe mtazamo wako juu ya programming, maana kuna conditioned na learned programmes, zipi unazungumzia?
 
Je unaweza kuniambia ni namna ipi mwanadamu yupo programmed?
Through conditioning tangia kuzaliwa, mfano kuna nyoka huwa wakiwa threatened wanajifanya wamekufa na mwili wao unaanza kutoa harufu na kunuka kama mzoga papo hapo, yaani hata kinyoka kilichozaliwa leo kinakuwa na huo utaalam, sasa hiyo ni genetic conditioni (programming), ila kuna zile programme za kujifunza mfano mtoto mdogo anapojifunza kuongea lugha ya wazazi wake. Je, yule anaetupa conditioned programmes hana cha kuwajibishwa nacho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…