Je, endapo kumbukumbu zako zote zikafyonzwa na kufutika, kisha ukawekewa kumbukumbu za gaidi, nawe utakuwa gaidi? Au moyo utagoma?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
21,126
2,000
Ni vyema tukaliweka hili sawa, je, mtu yupo kichwani au moyoni?

Mfano mtoto mdogo wa miaka 12, mwenye tabia nzuri kama malaika, tukaamua kunyonya memory yake na kuifuta kabisa kichwani kwake, kisha tukamjaza memory za gaidi la katili.

Je, huyo mtoto atakuwa yule gaidi kwa kila namna au moyo wa ule mtoto unaweza ukapambana na zile kumbukumbu moya za kimauaji?

Sasa je, mtu yupo wapi hasa, kichwani au moyoni? Na endapo mtoto huyu atafanya mauaji ya kujitoa muhanga, dhambi zitakuwa za nani? Za mwenye kumbukumbu au za mwenye mwili?

Maana inabidi tuassume mwili ni hardware na mawazo/akili/ utashi ni software tu.
 
Kitombise

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
7,405
2,000
kwani kazi ya kichwa ni ipi na kazi ya moyo ni ipi?
kwa mantiki hiyo ukishajua utendaji wa kazi zake, basi hata jibu lake utalipata
 
Tom McCarthy

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
29,607
2,000
Kuna wakati niliwahi fikiri "soul" ilitakiwa kutambuliwa kama mlango wa sita wa fahamu, kisha "pineal gland" iwe mlango wa saba wa fahamu!
Jibu basi, je spirit itapambana na hizo kumbukumbu? (si watu wote wana hiyo elimu kutambua tofauti ya roho na moyo tumelelewa kufikiri ni kitu kimoja, utasikia mtu anasema roho inauma akikusudia moyo and viceversa)
Kwanza tuelewe kijachokufanya wewe uwe wewe sio kumbukumbu. Kumbukumbu ni experience ya uliyoyaona na kutenda au kusikia.
Mtu ni roho na nafsi ndio inayomfanya awe mtu.

Tukumbuke pia huruma, upole, na menginiyo mengi hayaratibiwi na kumbukumbu.. hizo ni tabia za mtu binafsi.
Personalities za binadamu imegawanyika katika sehemu kuu ambazo ni Behaviour,(Tabia) Cognition (Utambuzi),Emotions (Hisia), tutaangalia zaidi Behaviour, tuone tabia mbalimbali za wanadamu

Wanasaikolojia wanasema kuwa Tabia za binaadamu zinasababishwa na Endocrine system
(Mfumo wa tezi) na Nervous System (Mfumo wa Fahamu/Neva). Lakini inasemekana kua mfumo wa Neva ndio husababisha zaidi tabia za mtu, wanasema kwamba Utathabiti au mwenye imfumo imara/thabiti wa neva basi anakua na uwezo mkubwa wa kuweza kujifunza hivyo anaweza kudhibiti tabia zake, labda kutoka tabia moja kwenda nyingine ambazo ni Aggressive, Passive na Assertive

Hivyo basi kama mtu mwenye behavior ya Passive ambazo ni upole akifutwa kumbukumbu zake akawekewa za Aggressive ambazo ni ukorofii/gaidi. Bado mtu huyo hawezi kua gaidi kutokana na kumbukumbu hizo. Ni sawasawa mtu umlazimishe kumvisha nguo za CCM hafu useme tayari mtu huyo sio CDM tena. Kiufupi ni kama utakua umesafisha dumu nje ila ndani bado ni chafu

Hivyo labda Kama wangefuta kumbukumbu afu wakampa madawa ya kuchochea hiyo tezi hapo juu kuzalisha hormones zitakazofanya mtu awe mkorofi. Ndio maana ambacho hua kinafanyika in real life. Hua wanafuta kumbukumbu zako afu wanakuBrainwash kwa mafunzo mbalimbali. Lakini hata hivyo ikitokea kitu kikatriger lost memories za victim basi kumbukumbu zote hurudi. Mara nyingi huwa wanabadirika
 
harakati za siri

Senior Member
Aug 23, 2020
193
500

Tabia zinakaa wapi, rohoni au nafsini?
 
Midazolam

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
283
500
Ni akili tu ndo hutumika hapo na mtu akikuteka akili hata nafsi inapenda kile kitu,

Jiulize leo vita itokee alafu uende pale udom ukawachukue wale wanafunzi ukawa silaa wakapambane vitani,Ni asilimia ndogo sana watakubali au wasikubali

Ila chukua wajeda uone watakavyoshangilia vzr Sana,maana akili yao tayari imeshakubali kile kitu

Sumu ya ugaidi hulishwa mtu kuanzia akiwa mdogo
 
harakati za siri

Senior Member
Aug 23, 2020
193
500
Obviously personality za mtu zinakaa kwenye Mind. Mind ni sehemu kuu ya Soul! Ndio maana kuna kamsemo mnasema eti "ni mindset yako tu"
Safi, kujibu swali la poster inawezekana kabisa kumtengeneza gaidi, refer uzi wako
Thread 'Kukataliwa na kudharaulika kunavyoweza kumfanya mtu mwema akawa mtu mbaya'
Kukataliwa na kudharaulika kunavyoweza kumfanya mtu mwema akawa mtu mbaya
Kama tabia yaweza kuwa influenced na external factors then hata hilo lawezekana kufanyika.
 
Tom McCarthy

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
29,607
2,000
Safi, kujibu swali la poster inawezekana kabisa kumtengeneza gaidi, refer uzi wako
Thread 'Kukataliwa na kudharaulika kunavyoweza kumfanya mtu mwema akawa mtu mbaya'
Kukataliwa na kudharaulika kunavyoweza kumfanya mtu mwema akawa mtu mbaya
Kama tabia yaweza kuwa influenced na external factors then hata hilo lawezekana kufanyika.
Kwamba basi tabia zinaweza kua influenced kwa kufuta kumbukumbu za mtu.. kumbuka mtoa mada anaongelea kumbukumbu sio tabia.
 
FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
21,126
2,000
Kwanza tuelewe kijachokufanya wewe uwe wewe sio kumbukumbu. Kumbukumbu ni experience ya uliyoyaona na kutenda au kusikia.
Mtu ni roho na nafsi ndio inayomfanya awe mtu.

Tukumbuke pia huruma, upole, na menginiyo mengi hayaratibiwi na kumbukumbu.. hizo ni tabia za mtu binafsi.
Personalities za binadamu imegawanyika katika sehemu kuu ambazo ni Behaviour,(Tabia) Cognition (Utambuzi),Emotions (Hisia), tutaangalia zaidi Behaviour, tuone tabia mbalimbali za wanadamu

Wanasaikolojia wanasema kuwa Tabia za binaadamu zinasababishwa na Endocrine system
(Mfumo wa tezi) na Nervous System (Mfumo wa Fahamu/Neva). Lakini inasemekana kua mfumo wa Neva ndio husababisha zaidi tabia za mtu, wanasema kwamba Utathabiti au mwenye imfumo imara/thabiti wa neva basi anakua na uwezo mkubwa wa kuweza kujifunza hivyo anaweza kudhibiti tabia zake, labda kutoka tabia moja kwenda nyingine ambazo ni Aggressive, Passive na Assertive

Hivyo basi kama mtu mwenye behavior ya Passive ambazo ni upole akifutwa kumbukumbu zake akawekewa za Aggressive ambazo ni ukorofii/gaidi. Bado mtu huyo hawezi kua gaidi kutokana na kumbukumbu hizo. Ni sawasawa mtu umlazimishe kumvisha nguo za CCM hafu useme tayari mtu huyo sio CDM tena. Kiufupi ni kama utakua umesafisha dumu nje ila ndani bado ni chafu

Hivyo labda Kama wangefuta kumbukumbu afu wakampa madawa ya kuchochea hiyo tezi hapo juu kuzalisha hormones zitakazofanya mtu awe mkorofi. Ndio maana ambacho hua kinafanyika in real life. Hua wanafuta kumbukumbu zako afu wanakuBrainwash kwa mafunzo mbalimbali. Lakini hata hivyo ikitokea kitu kikatriger lost memories za victim basi kumbukumbu zote hurudi. Mara nyingi huwa wanabadirika
Kwa mantiki hiyo, mtoto mdogo anapofanyiwa ‘brainwashing’ ili akikua awe gaidi na kwenda kujitoa muhanga, huwa inahusisha kurekebisha utengenezaji wa hormones kwenye tezi zake? Na je, hiyo dhambi ya kujitoa muhanga ni ya nani? Maana it seems huyu mtoto anakuwa kama vessel tu, au robot, unaweza kumuadhibu robot au utamuadhibu yule aliye - programme lile robot? Na consequently, ni haki kwa binadamu kuadhibiwa wakati aliyetu-programme yupo na wote tunamjua?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom