Je, CHADEMA hawaelewi maana ya Lockdown?

Je, CHADEMA hawaelewi maana ya Lockdown?

Sio kigogo ukweli ndo uwo TBC watu wanakufa kama njugu
Source kigogo. Hapo TBC hao watu wana makwao, unataka kusema huo ugonjwa wameambukizana hapo ofisini tu?Hivi huko shuleni ulisomea kijinga?

Senti bai yuzingi tecno T301
 
Si mlisema karibu mnakuwa Donor Country sasa wasi wasi wa nini ?, au zilikuwa blah blah za kisiasa.

Vipi update za hapo TBC.
 
Sio kigogo ukweli ndo uwo TBC watu wanakufa kama njugu
Mkuu samahani hiki unachokilazimisha hapa ni kitu cha ajabu Sana, wengine wanaweza hata kukuita mchawi.
Mana kulazimisha kuwa mtu kafa wakati ni mzima wa afya ni jambo la kushangaza kidogo.

Hebu angalia post number #33 hapo utaona huyo anayezushiwa kuwa kafa mwenyewe anazunguaza nini.

Ni ajabu sana kwa ma GT kuwa hivi mkuu.
 
Source kigogo. Hapo TBC hao watu wana makwao, unataka kusema huo ugonjwa wameambukizana hapo ofisini tu?Hivi huko shuleni ulisomea kijinga?

Senti bai yuzingi tecno T301
Mkuu angalia post #33 kwenye huu uzi.
Alafu uje ku comment tena.
 
Inaonekana huwa unakariri hotuba.za Rais badala ya kuzielewa!
Kwahiyo unakanusha msimamo huu wa Mh.Rais kua hii nchi ni maskini nasio tajiri kama tunavyoambiwa na Mh.Rais?
 
Kenya Uganda na Rwanda hakuna mamalishe? Sasa hivi wanaishije?

Hiyo social distance unayoisema ipo?
Pamoja na level seat Dar inafanyika mchana tu usiku watu wanashika bomba kama kawaida. Na Arusha ndio usisiseme. Vipanya vinajaza mpaka kufunga mlango shida.

Mabaa na night club yanaendelea kama kawaida. Kuna mahali tulipita usiku na jamaa yangu akaniuliza kuna korona kweli au ni utani kwa jinsi watu walivyokuwa wamejaa.

Raisi anasema hatuwezi kufunga mipaka kwa sababu tunategemewa na nchi zingine. Kwani Kenya haitegemewi?

Unaongelea umakini tupe mfano wa umakini unaoutaka.

Nairobi kwa siku wanapima watu 350 sisi waziri anatuambia toka janga lilipoanza wamepima watu 600 na ushee.

Sio lazima kufanyike lockdown kama nchi zingine. Wanaweza kusimamia hiyo social distance seriously na usafi kwa nguvu zote. Kwa sababu serikali umelegeza masharti kuna watu wameanza kusema hiyo korona haipo mbona hatuoni? Na wanagoma kunawa mikono.

Korona haijaletwa na CCM sasa inajihami nini kwa kitu ambacho sio makosa yao?

Kosa ambalo ndio litakuwa la CCM na serikali yake ni kutokuchukua hatua madhubuti kudhibiti COVID 19 kusambaa zaidi.

Onyo. Kwa mtazamo wa haraka hao walio kada ya juu ndio watakaoanza kushambuliwa kama tulivyoona Uingereza Iran Ghana Ujerumani Kenya na kwingineko. Viongozi wameonja joto ya jiwe.

*KWA COVID 19 WEKA SIASA PEMBENI.*

Yohana hiki chama kinatatizo kubwa la kuwa na watu wasio uelewa. Wengi wao ni wahuni wahuni tu na walichobakiza sasa hivi ni matusi tu.
Hili janga ni baya sana linahitaji umakini na mikakati madhubuti kulidhibiti.
Wao wamekalili tu funga mipaka, weka lockdown, hawajui kuwa social distancing ni mojawapo ya njia ambayo mkiitumia vizuri mnaweza kufanikiwa. Waulize Mama lishe ambaye anapik vitumbua na mtaji wa elfu tano,ukimfungia ndani siku 30 ataishi vipi?
Sasa badala ya kuonyesha umoja na mshikamano wao wanaleta political conspiracy wakati ni janga la dunia.
Kuna mbunge alitoa hoja labda ikibidi hili li chama lifungiwe kabisa. Any way bora waliache life kwa kupigwa na wananchi mwezi October.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani Chadema hawaelewi maana ya lockdown ndio maana wanaishabikia bila kutafakari kwa mapana.

Tanzania haina uwezo wa kuwafungia watu ndani na kuwafanya waendelee kula ugali na maharage huku wakikosa uhuru wa kutoka nje pekee.
Huko Ulaya kwenye lockdown raia wanahakikishiwa kupata mkate wa kila siku baada ya kupoteza kipato kwa kutokwenda kazini, je hapa tutaweza?

Viongozi wanaweza kukaa ndani hata mwaka kwa sababu akaunti zao zimenona, je wamachinga wanajua hata akaunti ya benki.

Afrika inaweza kutafuta namna yake ya kuwatuliza watu majumbani ili kuepuka mikusanyiko lakini siyo lazima tuige utaratibu wa wazungu wale serikali zao zimeachilia matrilioni ya fedha kuwezesha hizo lockdown.

Hapa Karantini tu inatusumbua hiyo " standard" lockdown tutaiweza kweli?

Niwatakie Pasaka yenye baraka!

Maendeleo hayana vyama.
You are very right, we can have our own way! Let’s not make funny 😆 of it!
 
Kwa hali hii ya uelewa wa WanaCCM na Wana Africa waliowengi ni Haki wanachofanyiwa yuko China.

Hata katika ngazi ya Familia siwezi kuruhusu Watoto wangu kucheza na watoto wa Jirani wanaopenda kucheza kwenye Majalala au wasiozingatia Afya.
 
Kenya Uganda na Rwanda hakuna mamalishe? Sasa hivi wanaishije?

Hiyo social distance unayoisema ipo?
Pamoja na level seat Dar inafanyika mchana tu usiku watu wanashika bomba kama kawaida. Na Arusha ndio usisiseme. Vipanya vinajaza mpaka kufunga mlango shida.

Mabaa na night club yanaendelea kama kawaida. Kuna mahali tulipita usiku na jamaa yangu akaniuliza kuna korona kweli au ni utani kwa jinsi watu walivyokuwa wamejaa.

Raisi anasema hatuwezi kufunga mipaka kwa sababu tunategemewa na nchi zingine. Kwani Kenya haitegemewi?

Unaongelea umakini tupe mfano wa umakini unaoutaka.

Nairobi kwa siku wanapima watu 350 sisi waziri anatuambia toka janga lilipoanza wamepima watu 600 na ushee.

Sio lazima kufanyike lockdown kama nchi zingine. Wanaweza kusimamia hiyo social distance seriously na usafi kwa nguvu zote. Kwa sababu serikali umelegeza masharti kuna watu wameanza kusema hiyo korona haipo mbona hatuoni? Na wanagoma kunawa mikono.

Korona haijaletwa na CCM sasa inajihami nini kwa kitu ambacho sio makosa yao?

Kosa ambalo ndio litakuwa la CCM na serikali yake ni kutokuchukua hatua madhubuti kudhibiti COVID 19 kusambaa zaidi.

Onyo. Kwa mtazamo wa haraka hao walio kada ya juu ndio watakaoanza kushambuliwa kama tulivyoona Uingereza Iran Ghana Ujerumani Kenya na kwingineko. Viongozi wameonja joto ya jiwe.

*KWA COVID 19 WEKA SIASA PEMBENI.*

Sent using Jamii Forums mobile app
Mamalishe, wamachinga ,wauza nyanya huko kenya na Uganda wameishia kupigwa virungu na kudhalilishwa na polisi. Mpaka sasa kuna zaidi ya watu wanne wamefariki nchini kenya,hayo ndio maisha yao nafikiri wewe unaona ni sawa.Jana watu wawili wamekufa baada ya kukanyagana kwenye mgao wa chakula kilichotolewa na Laila Odinga
Huko Rwanda ni tabu tu watu wanalilia majumbani. Labda hayo ndio unataka yatokee hapa Tz.
Umakini ni kuzingatia kunawa mikono mara kwa mara na kukaa mbali na watu pamoja na kuzuia mikusanyiko isiyo ya lazima.
 
Bwashee unajua nini maana kutofautiana kiitikadi? Msimamo wa chama tawala katka kuendesha mambo ya kitaifa na kimataifa si lazima yawe ndiyo muongozo na msimamo pekee na wa vile vya upinzani. Kuwa na mawazo mbadala ni haki iliyowekwa kikatiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mawazo mbadala yawe ya kujenga sio kuangamiza jamii. Ukiwafungia watu ndani kwa lazima utaleta taharuki kuliko hiyo ya corona. Hakuna mzazi aliye tayari kuona mwanawe anakufa njaa hapo.
Watu wanatoka nje si kwamba wanapenda. Wenye uwezo walishafungia ndani familia zao muda tu. Ukienda kwa mbowe utakuta vyuku vimejaa kwenye friji, beef, pork na pombe za aina zote na vingine vipo stoo.
Fikiri kuhusu nama lishe, machinga, konda na dereva, muuza matunda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ccm ni chama bora Africa na kipo madarakani Tanzania toka uhuru.je ubora wa ccm ni kwenye nini? Kama Rwanda pamoja na Vita na kuuana wanaweza Mambo mengi kuliko sisi,sasa huo ubora wa ccm upo kwenye nini hasa?Kuiba kura au ufisadi?
Rwanda ni kama dar tu hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom