Tatizo siyo Google kutranslate,shida unapatia ku translate.
Hii inaonekana huijui lugha ya asili,hili tatizo ndiyo maana unakosea. Ukiona wanakosea sana,soma vitabu vya asili,hili najua huliwezi.
Sina haja ya kufanya hivyo,ndiyo maana ulipo ileta nikaileta ya Kiswahili na marejeo ya Kiarabu yapo.
Aya imekuja wazi sana,na inataka jawabu lenye sharti,ndiyo maana ikasema "Ili....". Ukisoma aya ya kwanza ina kupa majibu ya sharti hilo.
Kadhalika katika dini kuna ofa si kwake tu Mtume bali mpaka kwetu sisi. Mtume alisamehewa madhambi yaliyo pita na yajayo,lakini kutokana na hilo hakubweteka,mpaka mke wake akastaajabu,ya kuwa iweje umesamehewa madhambi yaliyo pita na yajayo,lakini bado una simama usiku kufanya ibada mpaka miguu ina vimba ? Mtume akamwambia kwanini nisiwe mja mwenye kushukuru.
Ukarukia suala la kuharamisha yale aliyo halalisha Allah,ile ilikuwa ni jitihada yake mtume,ndiyo maana Allah akamkosoa,hili mpaka kwetu lipo,kwamba Allah ametusamehe kwa yale mambo yote tuliyo yafanya hali ya kuwa hatujui.
Hoja yako iko wapi ? Elezea wapi na ni lini mtume alifanya madhambi kwa makusudi kama mimi na wewe au lini alifanya dhambi ? Mtume alikuwa hakosei katika kufikisha ujumbe,ndiyo maana aliyo kuwa anakosea ni kwa kutokujua na alikuwa anakosolewa.
Kuna nukta nyingine umeigusia kuhusu Mtume kukopi kwa swahaba Umar,nitakuuliza ali nakilo vipi hali ya kuwa alikuwa hajui kusoma wala kiandika ? Ukiona ambacho kimesemwa na swahaba na kika kubaliwa au ukakikuta katika Qur'aan ujue Allah amekiunga mkono na akampa Mtume,kisha mtume akawasomea maswahaba. Soma sababu iliyo pelekea kuwekwa adhana,hii ilikuwa ni shauri la maswahaba,Allah akalipitisha,hii ni kwa sababu Allah amewaridhia maswahaba wa Mtume.
Sijakwepa swali,sababu maswalo yako ya kitoto,mepesi na ya kipuuzi pia,huonyesha ni kwa namna gani huijui Qur'aan bali huisomi.
"Ili" hili tamko la sharti,kuonyesha,ukifanya kadha utalipwa kadha au itakuwa kadha,tamko hilo limetanguliwa kabla yake sharti ya kuifanya "ili" iwe jibu. Halafu mjinga kama eti,uje uikosoe Qur'aan wakati Qur'aan ni fasaha. Sharti limetangulia na aya zilizofata zimefafanua sharti hili. Mfano wa jawabu la sharti ni lukuki sana,mathalani "....ili mpate kuwa Wacha mungu" sentensi hii imetanguliwa na sharti ambalo ni sababu ya tamko "ili" kuwa jibu la sharti hilo. Mfano mwingine ni "Nasoma sana ili nije kuwa fulani"' sharti ni "Nasoma sana" kisha "ili" ni jawabu la sharti likiambatana na ufafanuzi.
Hilo swali sijalielewa. Uliza vizuri.