Ndugu yangu
zed B,
Baada ya kupumzika muda wa chai naomba nichangie kidogo kuhusu shaka yako ya neno UTATU.
Dhana ya UTATU haimaanishi kueleza kwamba kuna Mungu Watatu.
Baadhi ya wanateolojia wanasema Mungu ni mmoja ila ana nafsi tatu.
Kwanza nao wanakosea, Mungu ana uweza wote, namaanisha anaweza kuwa na Nafsi zisizohesabika, mazillion ya Nafsi.
Walitakiwa waseme hivi, Mungu aliyejidhihirisha kwetu, amejidhirisha katika Nafsi Tatu.
Nafsi ni Utambulisho wa Uwepo wa Uhai flani wa peke yake.
Mimi = Nafsi ya kwanza umoja
Sisi = Nafsi ya kwanza uwingi.
Wewe = Nafsi ya pili umoja
Ninyi = Nafsi ya pili uwingi
Yule = Nafsi ya tatu umoja
Wale = Nafsi ya tatu uwingi
Turudi Kwenye Mada ya UTATU.
Kama nilivyosema hapo juu, Mungu wa kwenye Biblia ni mmoja TU.
ila amejitambulisha katika hali za Uwepo kwa aina tatu.
I. Roho Mtakatifu.
Huyo ndio Mungu Mwenyewe, yaani ndivyo alivyo, ni Roho Takatifu ila kwakuwa ndiye chanzo cha uhai anaitwa, Roho Mtakatifu.
Yohana 4:24
Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Mwanzo 1:2
Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
2. Baba.
Baba kwa Kiswahili wanaita ni Kivumishi yaani ni Sifa.
Biblia inampa Mungu sifa ya Ubaba.
Kama ndiye mzalishaji wa kila kiumbe hapa ulimwenguni, kilicho na uhai au kisicho.
Katika Biblia Baba ndiye anayezaa na sio mama. ( mama anajifungua tu)
Mathayo 1:1 Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.
Mathayo 1:2 Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake;
Mathayo 1:3 Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu;
Mathayo 1:4 Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni;
Mathayo 1:5 Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese;
Mathayo 1:6 Yese akamzaa mfalme Daudi.
Hivyo Basi Mungu anaitwa Baba.
Mathayo 6:8
Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.
Mathayo 6:9
Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,
Mathayo 6:10
Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.
Mathayo 6:11
Utupe leo riziki yetu.
3. Mwana
Hapa ndio panahitaji umakini kidogo.
Yesu ni Mwanadamu kama wewe,
Biblia inatuambia Mungu, yaani Roho Mtakatifu alishuka na kukaa ndani ya Yesu ili atufundishe kweli yake na kutuonesha maisha ya utakatifu yanavyopaswa kuwa.
Yaani yuleyule Roho Mtakatifu, alifanyika Mwili kama Yohana anavyosema.
Yohana 1:14
Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Ni lini basi Roho Mtakatifu alishuka kwa Kijana Yesu.
Mathayo 3:16
Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;
Luka 4:1
Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani.
Luka 4:18
Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
Je ni lini Roho Mtakatifu aliondoka katika mwili wa Yesu.
Marko 15:34
Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
Hapa tunaona kwamba Mungu Muumba Mbingu na Nchi amezungumza na Binadamu yaani na watu wake katika hali TATU.
BABA
Yeremia 31:9
Watakuja kwa kulia, na kwa maombi nitawaongoza; nitawaendesha penye mito ya maji, katika njia iliyonyoka; katika njia hiyo hawatajikwaa; maana mimi ni baba wa Israeli, na Efraimu ni mzaliwa wa kwanza wangu.
MWANA
Marko 2:3
Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne.
Marko 2:4
Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza.
Marko 2:5
Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.
Marko 2:6
Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao,
Marko 2:7
Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?
Marko 2:8
Mara Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu?
Marko 2:9
Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende?
Marko 2:10
Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (hapo amwambia yule mwenye kupooza),
Marko 2:11
Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako.
Marko 2:12
Mara akaondoka, akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata kuiona kamwe.
ROHO MTAKATIFU
Mwanzo 6:3
Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.
................................................................
Hapa sio kusema ni Mungu Watatu hapana.
Bali katika Biblia, Mungu kasema na Wanadamu akiwa katika hali tatu.
Au Nafsi TATU.
Kama Baba
Kama Mwana
Kama Roho Mtakatifu.
Mungu ni mmoja tu.
Hakuna Mungu watatu.