Hapa Yesu Kristo anatenda akiwa katika hali ya Ki-Mungu.
Hakuna Binadamu anaweza kutenda hivi hadi jamaa zake walishikwa na Butwaa.
Sembuse
Gavana,
Marko 2:5
Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.
Marko 2:6 Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao,
Marko 2:7 Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?
Marko 2:8 Mara Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu?
Marko 2:9 Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende?
Marko 2:10 Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (hapo amwambia yule mwenye kupooza),
Marko 2:11 Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako.
Marko 2:12 Mara akaondoka, akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata kuiona kamwe.
Mathayo 9:2
Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako.
Mathayo 9:3 Na tazama, baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru.
Mathayo 9:4 Naye Yesu, hali akijua mawazo yao, akasema, Mbona mnawaza maovu mioyoni mwenu?
Mathayo 9:5 Kwa maana rahisi ni lipi, ni kusema, Umesamehewa dhambi zako, au ni kusema, Ondoka, uende?
Mathayo 9:6 Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (amwambia yule mwenye kupooza) Ondoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako.
Mathayo 9:7 Akaondoka, akaenda zake nyumbani kwake.
Mathayo 9:8 Makutano walipomwona, walishikwa na hofu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu amri ya namna hii.
Mathayo 9:18 Alipokuwa akiwaambia hayo, tazama, akaja jumbe mmoja, akamsujudia, akisema, Binti yangu sasa hivi amekufa; lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, naye ataishi.
Mathayo 9:19 Akaondoka Yesu, akamfuata, pamoja na wanafunzi wake.
Mathayo 9:23 Yesu alipofika nyumbani kwa yule jumbe, aliona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo,
Mathayo 9:24 akawaambia, Ondokeni; kwa maana kijana hakufa, amelala tu. Wakamcheka sana.
Mathayo 9:25 Lakini makutano walipoondoshwa, aliingia, akamshika mkono; yule kijana akasimama.
Mathayo 9:26 Zikaenea habari hizi katika nchi ile yote.
( Leo
Gavana, na wenzake Maamuma, wakisikia habari za Yesu wanacheka sana, kama wapigafirimbi walivyomcheka sana Yesu ktk Mathayo 9:24 )